Unapopata nafasi ya kuwa karibu na Viongozi zingatia haya

Nov 6, 2016
83
216
UNAPOPATA NAFASI YA KUWA KARIBU NA KIONGOZI/ MTU ANAYEKUZIDI KIPATO/ MAARIFA/ DARAJA/ CHEO, ZINGATIA HAYA

Na Comrade Ally Maftah

Ukitaka kufanikiwa ni lazima ujenge ukaribu na watu kadhaa wanaokuzidi maarifa/ elimu / kipato / kipawa / ushawishi / mvuto / cheo, kwa lengo la kupata nafasi ya kujifunza mambo kwake.

Kwa bahati mbaya binadamu wengi tukipewa nafasi na hao watu huwa tunaanza kuwakosea, kuwanyima raha, kuwaomba hela, kuwadharau na kuwazungumzia vibaya. kuna wakati napita vijiweni unamzungumzia mtu fulani mwamba, kuna mjinga anaibuka " huyo ni fala tu mbona hata namba yake mimi ninayo, namjua sana hana lolote, nilisoma nae, nilikunywa nae, nilishatembea nae, na meeengi yanamtoka mtu, najiuliza ina maana yule jamaa asingempa ukaribu huyu asingechafuliwa.

ZINGATIA HAYA UNAPOPEWA NAFASI YA UKARIBU NA MTU MWENYE DARAJA JUU YAKO
1. USIWE UNAMPIGIA PIGIA SIMU KILA WAKATI
Hakikisha una jambo la msimgi la kuzungumza naye kabla ya kumpigia, na ukimpigia mara moja hajapokea usiendelee kumpigia mtumie mesage, halafu ukimpata eleza shida yako usianze lawama lawama

2. USIMUOMBE HELA
Unapopata ukaribu na tajiri usianze kuwa kero, kumwomba mwomba pesa bila mipangilio, unamkera kwa sababu na yeye anayo mipango yake, acha apende kukupa yeye mwenyewe.

3. USIPENDE KUMPIGIA UNAPOKUTWA NA MATATIZO MADOGO MADOGO
Unapopewa nafasi na kiongozi na hasa aliyepo kwenye nafasi za ulinzi na usalama wa nchi, usiwe unampigia wakati either umekamatwa na polisi kwa makosa yako au umeonewa sahemu, jitahidi kupambana na hiyo changamoto na suala la kumpigia liwe ni pale unapokuwa umetumia njia zote zimefeli.

4. JIEPUSHE KUMUONGELEA UKIWA NA WATU
Usianze kuwa katibu wake kila unapokuta anaongelewa wewe unaanza kububujikwa na maneno kumuelezea, jua kwamba si kila taarifa uliyonayo kuhusu yeye angependa na wengine wajue, kuna mambo yake binafsi hayo unayajua wewe ila hapendi wengine pia wajue, unaweza kumuingiza kwenye hatari

5. JIEPUSHE KUMSHAURI SHAURI, UNAANZA KUJIFANYA MSHAURI TENA WA MAMBO YA KIFAMILIA NA KIBIASHARA
Subiri akuombe umshauri sio wewe unakurupuka tu ooh bosi nataka nikushauri, wewe hujui misingi ya imani yake, itikadi na mifumo yake unakuja kwenye maisha yake unaanza kulazimishia mifumo yako kwenye maisha yake ni kero.

NIKUTAKIE SIKU NJEMA YA MUUNGANO

NDIMI
Comrade Ally Maftah
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Mjumbe Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
Mwandishi Vitabu na Mdau wa Maktaba ya Taifa
Msanii, Mtunzi, na Mdau wa BASATA
Mwanzilishi na Mmiliki wa CAM STORE (DUKA KUU)
JITU LA MIRABA
CHALINENEE
 

Attachments

  • 1713887328029.jpg
    1713887328029.jpg
    245.5 KB · Views: 2
Upo sahihi lakini mi naamini afanyaye hayo yote ni yule aliyekosa utimamu wa akili tu
 
Upo sahihi, hakuna kitu kibaya kama Kila shida unamlilia MTU bali pambani labda yeye asikie Kwa watu baki
 
Una fixed mindset - hasa nyie vijana wa vyama vya siasa.

Jitahidini ku-grow hao viongozi ni WATU Kama nyie isipokuwa nyie mmeamua kuwa wafuasi na wao wameamua kuwa viongozi.
 
Unaanzaje kujibebisha mkuu? Kwanini uwe Kero kwa mtu Mwingine Kisa tu kakuzidi mamlaka? Yaan em fikiria mwenyewe kama ni mtu uliyetimia kwanini umnyime amani mtu mwingine eti kwa sababu tu kakubali muwasiliane...maana kuwa karibu na mtu Mwingine si kigezo cha kupewa ruhusa ya kuwasiliana nawe...anaweza akamute tu
 
Back
Top Bottom