Unapoongea na simu kuwa makini na nyakati hii

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,744
7,098
Leo sina mambo mengi kabisa yaan,,ni hivi wakati muhimu kabisa wa kujua siri za mzungumzaji upande wa pili wa simu ni pale mnapomaliza mazungumzo na kukata simu.

Yaan mda huo kama utaagana na mtu kwenye simu basi kawia kidogo usikate simu mapema yaan hapo utasikia kitu fulani ambacho hujategemea,,,kama ni mwanamke ndio yupo upande wa pili wa simu na yupo na wenzake utasikia " huyu bwege anajifanya ananipenda lkn mbakhiri kweli" au "angejua anavyo niboa na simu zake yaan basi tu"

Kama ndio mwanaume yupo upande wa pili wa simu na ukakawia kukata simu mapema utasikia " huyu malaya ananiona mimi kama ATM" au " huyu demu hivi ananichukuliaje hela zangu anazipenda ila mzigo hatoi"

Ninachotaka kusema hapa,kama wewe ni msema hovyo baada ya mazungumzo ya simu basi usiongee chochote mpaka uhakikishe simu imekatwa ndio ubwabwaje la sivyo utachafua hali ya hewa.

Na

Kama wewe unataka kusikia mazungumzo muhimu baada ya habari,,basi usikate simu mapema huenda ukasikia yatakayo kushangaza.

Huwa nikimuona mtu baada ya mazungumzo hakati simu huwa sipendi ujinga naamua kuikata chap,,,sio kwamba huwa naongea baada ya kukata simu laa ila najua huyu ni mmbea anataka kusikia lolote kutoka kwangu


Ni hayo tu!
 
Kuna ishu ya kazi niliunganishwa kipindi fulani,nikafanyiwa interview kwenye simu,,,sasa inaelekea wale jamaa ni wapigaji katika hiyo kampuni

Nikaulizwa kazi yako ya mwisho kwanini uliiacha,,,nikasema niliacha kwakuwa niliambiwa nichague kazi au kuswali,,,yan muajiri wangu hakutaka mimi niswali nikamwambia kuswali kwangu ni muhimu sana,,ndo akaniambia chagua moja ima kazi au swala,,nikamwambia nachagua kuswali basi tukamalizana mda ule ule

So inaelekea jamaa wakaona huyu sio mtu wa dili hatufai nikasikia akisema mbele ya wenzake "hatufai huyu" na ni kweli sikutafutwa tena
 
Binadamu tunacheka nao ila nyuma ya pazia ni zaidi ya manyamera! Kuna siku nilikua naongea na bro wangu kabisa nimeweka simu loud speaker!!

Simu Iko mezani Mimi Kuna kazi napiga baada ya maongezi akasahau kukata nikaskia anaongea na watu pembeni kwa kunisema vibaya nikarekodi
Kwamba Mimi ni mchawi sina maana yoyote anajuta kuzaliwa na Mimi na maneno machafu kisa tu nilitoka kununua pikipiki mpya siku Moja kabla
Nilichokifanya nikamtumia ile voice what's app
Tunaenda mwaka wa sita huu hatuongei
 
Umenikumbusha kitu miaka 14 way back nadhan ilikuwa 2010 bado chalii mdogo nimeondoka kwa boss nimejitegemea nimepanga geto halafu nipo mji sina mwenyeji sasa nikaugua ghafla nikalazwa nikasema ngoja nimpgie nimjulishe tu ex boss wng ajue tu kwabwa nimelazwa...

bwn bwn nikamvutia waya.. oy maza naumwa niko hoi nimelazwa hosptal flani! pole wee ni nan? mimi issaa! pole tutakuja kukuona mwanangu... haya mama asante... sikukata sim nikalala zangu nilikuwa kwenye dripu!

nikaanza kusikia wakinijadili yeye na binti yake, ooh huyu huyu flani alieondoka hapa kwa mikogo haya si majaribu? mama wala hata tusiende! dah nilifura na hasira nikasema niwapigie nin niwaambie wasije maana sikuhitaji msaada wao wa kifedha ila tu nilitaka wajue maana nje ya uboss alikuwa ni ndugu kbs yan ndugu yetu!

kweli bhn mpaka napata nafuu naondoka hapo hosptalini hawakuwahi kukanyaga hata kunipgia sim ya kinafiki

tangu siku hiyo mpaka leo nipo kwangu nina familia mke na watoto watatu sijawahi kukanyage kwake tena! Mungu ni mwema
 
Binadamu tunacheka nao ila nyuma ya pazia ni zaidi ya manyamera! Kuna siku nilikua naongea na bro wangu kabisa nimeweka simu loud speaker!!

Simu Iko mezani Mimi Kuna kazi napiga baada ya maongezi akasahau kukata nikaskia anaongea na watu pembeni kwa kunisema vibaya nikarekodi
Kwamba Mimi ni mchawi sina maana yoyote anajuta kuzaliwa na Mimi na maneno machafu kisa tu nilitoka kununua pikipiki mpya siku Moja kabla
Nilichokifanya nikamtumia ile voice what's app
Tunaenda mwaka wa sita huu hatuongei
Aisee huyo bro yako Ni snitch kinoma noma
 
Nilikua naongea na mama, sasa tumesogoa wee, ile tumeagana ckukata cm nkaweka pembeni coz kuna kitu nlikua nafanya, namsikia mama anasema

"ila huyu kichaa nisingemzaa ningekufa na kansa ya kizazi sio kwa usumbufu huu." Nilicheka kwa sauti, mama akashtukaa. Tukalianzisha tena kusogoaa. Yaan ilikua balaa.

 
Back
Top Bottom