george aloyce
JF-Expert Member
- Aug 22, 2017
- 1,293
- 1,964
Sawa inatokea umesababisha ajali umeua binadamu mwenzako umekimbia kukwepa kwenda jela na umebahatika hakuna aliyekuona. Huko nyumbani kwako utaishije? Unaingia mtandaoni unaona maelfu ya watu wanalia kwa kuondokewa na mpendwa wao ambaye wewe ndio chanzo.
Huwezi kuwa na amani, utaishi uraiani lakini bado nafsi na roho yako vitaishi maisha ya jela, kiufupi ni utateseka maisha yako yote. Wapo watu wengi wa aina hii mtaani tunaishi nao, watu ambao walisababisha ajali walipoona wameua wakakimbia na mpaka leo hawajagundulika, wapo wengi mioyo yao imebeba hukumu nzito zinawatafuna.
Tujitahidi kuwa na hofu ya Mungu, ajali haina kinga lakini tunapojaaliwa kumiliki usafiri wetu au tunapoendesha jitahidini kuwa makini, usijali roho yako tu beba na roho za watu wengine, inaumiza sana kuondoa uhai wa binadamu mwenzako ambaye ni tegemezi kwa familia yake.