UN: Vyakula vitokanavyo na mimea ni muhimu kuliko nyama katika kupambana na ongezeko la joto duniani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,513
9,309
Burger

Kubadili aina ya chakula kutoka nyama na kuingia kwenye vyakula vitokanavyo na mimea kunasaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. Ripoti ya wataalamu wa tabia ya nchi wa Umoja wa mataifa wameeleza.

Ripoti kubwa kuhusu matumizi ya ardhi na mabadiliko ya tabia nchi imesema matumizi makubwa ya nyama na maziwa katika nchi za magharibi yanachochea ongezeko la joto duniani.

Lakini wanasayansi na maafisa wametaka watu kuanza kutumia vyakula vya jamii ya mbogamboga zaidi.

Wamesema kwa kufanya hivyo watu wengi watakula,kutokana na matumizi madogo sana ya ardhi, kuliko wakiwa wanakula nyama.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na wanasayansi 107 inasema ikiwa ardhi itatumika vizuri zaidi, itaweza kupunguza hewa chafu inayozalishwa na binaadamu.
Hitimisho hilo lilitolewa baada ya mjadala uliofanyika, Geneva Uswisi.

''Hatuwaambii watu waache kula nyama kabisa.Baadhi ya maeneo watu hawana mbadala mwingine wa chakula. Lakini ni wazi kabisa kuwa katika nchi za magharibi tunakula nyama sana,'' alisema Profesa Pete Smith mwanasayansi wa mazingira kutoka chuo cha Aberdeen nchini Uingereza.

Tunapoteza chakula kingi sana pia. Jopo linakadiria kuwa karibu asilmia 8 mpaka 10 ya chakula huingia kwenye mapipa ya takataka.

Ripoti imetaka hatua zichukuliwe kupambana na uharibifu wa udongo na ukataji miti, mambo ambayo yanachangia mabadiliko ya tabia nchi.

Pia ripoti inaonya kuwa mipango ya baadhi ya serikali kupanda miti na kuichoma ili kuzalisha umeme itapambana na uzalishaji wa chakula, isipokuwa pale tu itakapodhibitiwa.

Mahusiano ya mabadiliko ya tabia nchi na chakula
Mabadiliko ya tabia nchi ni tishio kwa usalama wa chakula chetu. Kiwango cha juu cha joto, mvua kubwa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa yatakuwa na athari kubwa kwa mazao na mifugo.

Lakini uzalishaji wa chakula pia huchagia ongezeko la joto duniani.
Ufugaji huchagia ongezeko la joto kupitia gesi ya methane ambayo wanyama huzalisha, lakini pia kwa ukataji miti.

Madhara ya kimazingira kutokana na uzalishaji wa miti ni muhimu kwa wasiotumia vyakula vitokanavyo na wanyama na wale wanaotumia vyakula vya mbogamboga.
Kundi moja nchini Uingereza linalojiita #No Beef liliwashawishi wapishi kutoa nyama ya ng'ombe na ya kondoo kwenye orodha ya chakula cha wanafunzi.

Peter Stevenson, kutoka shirika la World Farming, alisema: ''Kupunguza matumizi ya nyama ni muhimu ikiwa tunataka kuondokana na tatizo la mabadiko ya tabia nchi.''

Lakini katika nchi nyingine, kwa mfano China matumizi ya nyama yanaongezeka. Hii ni pamoja na kuwepo na majaribio ya serikali ya China kupigia chapuo mlo wa asili.

Mabaki ya chakula yanaweza kupunguzwa?
I
Kampuni ya Partage hukusanya chakula kuwasaidia wenye uhitaji ..

Waandishi wa ripoti wamewashauri watu kuacha kutupa chakula- kabla au baada ya kuuzwa kwa wateja.

Mabaki ya vyakula wakati mwingine yanaweza kutumika kama lishe kwa wanyama au, kama kinafaa, kinaweza kutolewa kwa wahitaji kama msaada.

Taasisi moja nchini Uswisi iitwayo Partage hupokea vyakula ambavyo havikuuzwa na kutupwa kisha huvipeleka kwa familia mbalimbali.

Pia hukusanya mikate iliyolala na kuigeuza kuwa biskuti, hukausha matunda na mboga za majani. Hii husaidia kupunguza hewa ya ukaa ambayo huzalishwa wakati wa uzalishaji wa chakula.
Msitu

Dokta Katrin Fleischer anaonya kuwa katika baadhi ya maeneo upungufu wa madini ya phosphorus kwenye udongo-madini muhimu kabisa kwa ajili ya kukuza mimea pia huathiri ukuaji wa miti.

Alisema: ''Hii itamaanisha kuwa mvua zimeshafikia ukomo wake na hautaweza kufyonza hewa ya ukaa itakayozalishwa.
''Ikiwa hali itakuwa hivi, hali ya hewa itakuwa ya joto kwa haraka sana.''

Mimea hufyonza hewa ya ukaa kutoka hewani, lakini ukataji wa miti na mbinu duni za kilimo vinaweza kuharibu uwezo wa mimea kufanya hivyo.

hali ya mabadiliko ya tabia nchi huwa mbaya zaidi ikiwa udongo utaharibiwa, hivyo ni bora jamii ikafahamu vyema mbinu za kudhibiti uharibifu wa udongo ikiwemo kudhibiti idadi ya wanyama wanaofugwa, upandaji miti ambao husaidia kurutubisha udongo, na kusaidi kupunguza umasikini na kuongeza usalama wa chakula.

Matatizo haya yanaweza kupata utatuzi?
Kubadili namna binaadamu alivyozoea kutumia ardhi ni changamoto, haswa kama mabadiliko haya yanahusisha mabadiliko katika mbinu za kilimo.

Wanasayansi wanasema watu wanapaswa kufanya yafuatayo:
Kulinda misitu ya asili, hasa maeneo ya kitropiki
Punguza ulaji wa nyama nyekundu na mbogamboga zaidi
Sisitiza kilimo cha kuchanganya na miti
boresha kilimo cha mazao mchanganyiko
 
Back
Top Bottom