Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 551
- 748
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS) Ni Idara ambayo inamajukumu ya kukusanya, kuchunguza na kuchambua Taarifa na shughuli zote zinazohusiana na Usalama wa Taifa. Ikiwa ni pamoja na kubaini matishio yote dhidi ya Tanzania lakini pia kushauri wizara zote juu maswala ya ulinzi na Usalama, Hivyo Tunaweza kusema idara hii ni idara ya muhimu na ya msingi katika uhai wa nchi yetu.
Katika kutekeleza majukumu yake idara inatumia mifumo na njia mbalimbali, Tufahamu yakuwa tupo katika dunia ya mabadiliko makubwa, Hivyo ni muhimu kwa idara yetu ya usalama wa taifa kuwa na mfumo wa kidigitali yaani tovuti ambayo raia wanaweza ingia na kuona taarifa mbalimbali lakini pia kuwezesha raia kutoa taarifa mbalimbali zitakazo saidia idara katika ufanyaji kazi.
Faida zitakazo tokana na uwepo wa tovuti hii sii tu wananchi kupata taarifa kutoka kwa idara bali pia idara kupokea taarifa kutoka kwa wananchi. Tukumbuke kuwa usalama wa Taifa unaanza na mwananchi, Hivyo ni muhimu kwa idara kuwa na mfumo utakao unganisha na kukuza mahusiano ya moja kwa moja na wananchi kwa kufanya hivi tutakuwa tumewavuta karibu wananchi na hivyo kuwa na mfumo shirikishi kati ya serikali na wananchi
MUUNDO WA TOVUTI
Napendekeza mfumo wa tovuti hii uwe na sehemu zifuatazo:-
SEHEMU YA HISTORIA YA IDARA
Katika sehemu hii idara iweke historia yake toka kuanzishwa kwake lakini pia viongozi waliowahi kuhudumu katika nafasi za ukurugenzi wa idara na historia zao, Lakini pia maono ya idara pamoja Na dira yake yaelezwe Kwa ufupi.
SEHEMU YA TAARIFA KUTOKA IDARA.
Sehemu hii iwe ni sehemu ambayo mwananchi akiingia ataona taarifa mbalimbali kama tahadhari za nchi zenye machafuko na nchi ambazo zina matishio ya ugaidi taarifa hizi idara itapokea kutoka kwa mabalozi wa Tanzania walio katika nchi mbalimbali na mara moja idara itaweka taarifa hizo katika tovuti yake hii itasaidia Wafanyabiashara, Watalii pamoja na Wanafunzi katika kupanga ratiba zao.
SEHEMU YA TAKWIMU.
Sehemu hii iwe na takwimu mbalimbali za Tanzania lakini pia takwimu za nchi nyingine za kijiografia, Kisiasa, Kiuchumi, biashara zinazofanywa na nchi nyingine. Mfano Mtanzania akitaka kujua ni maeneo gani katika nchi ya Rwanda biashara ya kuuza vitunguu ni kubwa moja kwa moja anaweza pata taarifa hizo kwenye tovuti ya usalama wa taifa taarifa za kweli na zenye uhakika.
SEHEMU YA NUKUU, VIPEPERUSHI NA MAKALA.
Hapa kuwekwe nukuu mbalimbali za viongozi wa nchi pamoja na nukuu za wakurugenzi wa idara ambazo zinahusiana na maswala ya ulinzi na usalama lakini pia vipeperushi na Makala ambazo zitakuwa zinaelezea umuhimu wa wananchi kushiriki na kutoa michango itayosaidia ukuaji mzuri wa nchi yetu, Makala za uelimishaji juu ya hatari za Rushwa, Ufisadi na ugaidi.
SEHEMU YA WANACHI KUTOA TAARIFA
Hii ni sehemu ya muhimu kwani hapa idara inaweza kukusanya taarifa mbalimbali za kiusalama kupitia wananchi sehemu itaruhusu wananchi kutoa taarifa ambapo mwanachi akiingia mfumo utamlinda na Hivyo kutoa taarifa zinazohusu ugaidi lakini pia kutoa taarifa juu ya viashiria vyovyote ambavyo ni hatari kwa taifa Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na Kidini.
Tukumbuke kuwa idara ina jukumu nzito la kuilinda Tanzania dhidi ya matishio ya aina yeyeto Hivyo basi suala la kuwahusisha wananchi juu ya ulinzi na usalama kwa nchi yao si suala la kupuuzwa.
FAIDA ZA MFUMO KWA UJUMLA
CHANGAMOTO ZA MFUMO
Njia nzuri ya kupambana na changamoto hizo kwanza ni kuundwa kwa tovuti yenye ulinzi na usalama wa hali ya juu ambao utakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kuzuia shambulio lolote la kujaribu kudukua mfumo lakini pia pale ambapo mwananchi anataka kutoa taarifa mfumo utamtaka ajaze taarifa zake binafsi na aruhusu mfumo kuweza kufikia taarifa zake za chombo anachotumia kuwasiliana na idara. Hii itasaidia wananchi kuogopa kutoa taarifa za uongo hivyo kuondoa usumbufu kwa idara,
Pia kuundwe kwa sheria ambayo endapo itabainika mwananchi ametoa taarifa za uongo kwa nia ovu ya kusumbua serikali hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
HITIMISHO
Tunatambua idara inafanya kazi zake kwa usiri mkubwa, Hivyo taarifa ambazo idara itakuwa inatoa ni taarifa ambazo hazina madhara dhidi ya usalama wa Tanzania. Pia nashauri idrara kupitia upya mifumo yao ya kuajiri na kuboresha idara ili iakisi dunia ya sasa.

- Kutoa nafasi ya wananchi kushiriki katika ulinzi na usalama wa nchi yao Hivyo kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali na wananchi.
- Wananchi kujua historia ya nchi yao lakini pia kupata nafasi ya kujifunza maswala mbalailmbali na kwa kufanya hivi idara itakuwa inakuza na kufundisha uzalendo kwa wananchi hali hii itasaidia kuondoa Ukabila, Udini na Ukanda kwani tutategema idara kupitia tovuti yake kuweza kukemea na kuelimisha jamii. Hii itasaidia sio tu mahusiano ya wananchi na serikali lakini pia itaudumisha uhusiano huo.
- Idara kuwa na wingi wa taarifa kutoka kila kona ya Tanzania na Hivyo kuifanya idara kuwa na utajiri wa taarifa ambazo idara itazitumia katika kutekeleza majukumu yake.
CHANGAMOTO ZA MFUMO
- Ufikshwaji wa Taarifa za uongo, Watu wenye nia ovu wanaweza tumia tovuti kufikisha taarifa za uongo kwa idara jambo ambalo litaleta usumbufu kwa idara.
- Kudukuliwa kwa mfumo, Hii ni dunia ya utandawazi watu wenye nia ovu wanaweza dukua mfumo na kupata taarifa ambazo wananchi wamezitoa kwa idara.