Ukipewa nafasi ya kuwa Kiongozi kwa siku moja ni kitu gani utabadilisha cha kwanza?

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
87
103
Ikitokea umepewa fursa ya kuwa kiongozi kwa siku moja, unapata nafasi ya kufanya mabadiliko katika sehemu uliyopo na kubalisha kitu kimoja kwenye sehemu uliyopewa uongoze.

Ikitokea ninafursa ya kuwa kiongozi kwa siku moja, ningependa kuwa kiongozi wa taasisi ya elimu, kama chuo kikuu. Elimu ni msingi wa maendeleo ya kitaifa na binafsi. Kipaumbele changu cha kwanza kingekuwa kuangalia upya mfumo wa elimu na kuhakikisha kuwa unaendana na mahitaji ya sasa ya jamii na soko la ajira.

Ningependa kuwekeza zaidi katika teknolojia na rasilimali za kufundishia ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora na inayokidhi viwango vya kimataifa. Kwa kufanya hivyo, ningewawezesha wanafunzi kufikia uwezo wao kamili na kujenga msingi imara kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Unatamani uwe kiongozi wa nini na wapi na ni kitu gani ungekipa kipaumbele cha kukifanya cha kwanza na kwa sababu gani?
 
Yaani nitaitisha kikao cha watumishi kwanza bila kusahau vyombo vya habari muhimu hasa miradi ayo, alafu hao watumishi kazi wanayo nitawasimanga vibaya sana.. hadi wajute

Mwisho nitamshukuru mama na kazi iendelee..
 
Nita react vigorously kwenye swala la usafi wa mazingira. Aisee nitakuwa mbogo hadi mtasema huyu mzee anavuta bangi. Majiji yetu ni machafu mno na kuna vitengo vya usafi na watu wanalipwa mishahara

1. Sikupi leseni ya biashara hadi nikupe kipande cha barabara mbele ya ofisi yako au duka lako upande maua, miti, usafishe mitaro papebdeze mno!

2. Makampuni makubwa sijui voda sijui tigo au crdb nawapa barabara nzima kwa mfano Nyerere Road au Mandela Road inakuwa ya kwako na ole wako nikute haipendezi. Ukitaka msaada wa serekali unapewa ila jukumu la usimamizi ni lako. Panda nyasi tena Canadian sio za hovyo hovyo na maua mazuri ya grade A.

3. Kuanzia chekechea ni lazima kuweka somo la house keeping. Watoto wakue huku wanaelewa kuchezea mazingira ni kujitafutia kwenda jela! Na haki mtu akizembea namfunga kweli.

4. Usafi ni pamoja na ku deal na boda boda. Hizi mburula zimegeuka ni jeshi la kipekee wanalojiamulia cha kufanya. Haki ingefika mahali wangebadilika maana cha moto wangekiona. Nisingewatoa barabarani ila ningetengeneza mkakati wangenyooka tu. Kwamba boda yeye taa nyekundu za barabarani hazimuhusu na anapita taa nyekundu traffic officer yuko hapo hapo anaongoza magari! Wangejua hawajui
 
Ikitokea umepewa fursa ya kuwa kiongozi kwa siku moja, unapata nafasi ya kufanya mabadiliko katika sehemu uliyopo na kubalisha kitu kimoja kwenye sehemu uliyopewa uongoze.

Ikitokea ninafursa ya kuwa kiongozi kwa siku moja, ningependa kuwa kiongozi wa taasisi ya elimu, kama chuo kikuu. Elimu ni msingi wa maendeleo ya kitaifa na binafsi. Kipaumbele changu cha kwanza kingekuwa kuangalia upya mfumo wa elimu na kuhakikisha kuwa unaendana na mahitaji ya sasa ya jamii na soko la ajira.

Ningependa kuwekeza zaidi katika teknolojia na rasilimali za kufundishia ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora na inayokidhi viwango vya kimataifa. Kwa kufanya hivyo, ningewawezesha wanafunzi kufikia uwezo wao kamili na kujenga msingi imara kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Unatamani uwe kiongozi wa nini na wapi na ni kitu gani ungekipa kipaumbele cha kukifanya cha kwanza na kwa sababu gani?
Nikipata urais kwa siku moja, natoa hotuba ndeefu yenye details za MARIDHIANO ya Kitaifa na kutangaza mchakato wa Katiba ya Wananchi wa Tanzania vile wanavyotaka utawala na maongozi ya nchi yawe vipi.

Nafanya mkutano na Mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao Tanzania, kuwaelezea lengo, dhima, nia na matakwa ya nchi yetu kufuata utawala wa sheria.

Kisha namteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuunda serikali ya mseto ya mpito kuelekea Uchaguzi wa Kwanza wa vyama vingi Tanzania
 
Kuongeza muda nikae zaidi ya siku moja....; Mabadiliko ni muendelezo huwezi ukafanya long term plans in short term...; Kwahio Viongozi inabidi watekeleze kilichoshapangwa na wadau sio kubadilisha au kufanya wanachotaka....

Zinahitajika systems / Taasisi za kuweka infrastructure rafiki ili wananchi waweze kujenga nchi yao (They are the really people who makes it happen) they only need an infrastructure and a good system; not necessarily a good leader...
 
Nitaweka kipaumbele kwenye Elimu Kwa masomo ya Sayansi, Hisabati, Computer, Kilimo na Ufundi...Somo la kilimo litafundishwa Kwa kuzingatia Fursa zilizopo katika Kanda husika...nitafuta masomo yote ya lugha na dini katika Elimu ya msingi na sekondari...badala yake nitaweka masomo ya falsafa, muziki, michezo na utamaduni wa mwafrika...Kila mwanafunzi lazima asome Somo la Ufundi na Ujasiliamali akiwa sekondari...mtihani wa Form Six utakuwa mgumu ajabu ili nipate cream tu ambayo serikali itawagharimia masomo Yao mpaka mwisho wa uwezo wao Kwa kupunguza manunuzi ya magari ya kifahari na mambo mengine yasiyo ya lazima...top cream ya hii cream nitawaingiza ile sekta nyeti ili waratibu mustakabali wa taifa lao...hapo ni kwenye Elimu tu...
 
Nita react vigorously kwenye swala la usafi wa mazingira. Aisee nitakuwa mbogo hadi mtasema huyu mzee anavuta bangi. Majiji yetu ni machafu mno na kuna vitengo vya usafi na watu wanalipwa mishahara

1. Sikupi leseni ya biashara hadi nikupe kipande cha barabara mbele ya ofisi yako au duka lako upande maua, miti, usafishe mitaro papebdeze mno!

2. Makampuni makubwa sijui voda sijui tigo au crdb nawapa barabara nzima kwa mfano Nyerere Road au Mandela Road inakuwa ya kwako na ole wako nikute haipendezi. Ukitaka msaada wa serekali unapewa ila jukumu la usimamizi ni lako. Panda nyasi tena Canadian sio za hovyo hovyo na maua mazuri ya grade A.

3. Kuanzia chekechea ni lazima kuweka somo la house keeping. Watoto wakue huku wanaelewa kuchezea mazingira ni kujitafutia kwenda jela! Na haki mtu akizembea namfunga kweli.

4. Usafi ni pamoja na ku deal na boda boda. Hizi mburula zimegeuka ni jeshi la kipekee wanalojiamulia cha kufanya. Haki ingefika mahali wangebadilika maana cha moto wangekiona. Nisingewatoa barabarani ila ningetengeneza mkakati wangenyooka tu. Kwamba boda yeye taa nyekundu za barabarani hazimuhusu na anapita taa nyekundu traffic officer yuko hapo hapo anaongoza magari! Wangejua hawajui
Naunga mkono hoja zote
 
Cha kwanza nafuta vyama vyote vya siasa wasajiri upya na jina lisijirudie kwa 99%.
Mali za vyama zinataifishwa zote!
Naunda kamati maalum ya wazee washauri kwa kuchota kada zote za kijamii, kuongoza kwa mpito kuelekea usawa na demokrasia ya kweli.
Siku hiyo inazaliwa Tanzania MOJA bila kura yoyote! Yan serikali moja, Bunge moja, Mahakama moja.
Siku hiyo hiyo nawakusanya walioficha pesa na mali nje tokana na kodi za raia wanasahini zirejee kwa nguvu au nawabanika hadharan (pesa kwenye akaunti maalum, mali kwenye custody maalum)
Magereza yote yanabaki hayana mtu, makosa ya jinai yaanze upya isipokuwa wauaji nawapa haki yao siku hiyo!
Mikataba yote mikubwa yenye maslahi makubwa kwa nchi inawekwa mezani kwa wazee kujua status ya faida na hasara baadae inapelekwa bungeni Dodoma( hata tu stoo kama hawatak kuipitia baadae).
HATA HIVYO, MLETA MADA JIZUIE KULETA MAZINGIRA YA KITOTO YA 'SIKU MOJA'
.........................lest count it a long day to sip wine in the White House staring at peacoks and glancing at legendary wall pictures, Nkrumah!!!!
 
Back
Top Bottom