UKAWA waelimisheni watu juu ya upigaji kura hususan kwa wabunge na madiwani wa UKAWA

C.K

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
394
162
Tofauti na chaguzi nyingine, mwaka huu UKAWA chini ya vyama vyake vinne (CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD) anasimamishwa mgombea mmoja tu katika kila ngazi - urais, ubunge na udiwani. Sina wasiwasi kwa upande wa kumpigia kura rais ila kwa wabunge na madiwani kunaweza kuwapo baadhi ya watu wasio na uelewa wa kutosha wampigie nani... Naomba uongozi wa UKAWA waone namna ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuwapigia kura wabunge na madiwani wa vyama vinavyounda UKAWA. Watu waeleweshwe kwamba wawapigie wagombea wa CDM, CUF, NCCR na NLD wote katika maeneo yao kwani mwingine anaweza kuacha kupiga kura kwa kukosa tu kumuona mgombea wa chama chake. Hivyo ni muhimu watu wakapewa elimu hiyo hususan vijijin ambako mwamko na uelewa kuhusu UKAWA unaweza kuwa chini kidogo ukilinganisha na mijini.
 
Na hao wagombea wahakikishe wanapita kwa kila mpiga kura ili wajulikane vya kutosha
 
MAKAMBA:LOWASA ALIFUKUZWA KAZI,
HAKUJIUZULU!
Katibu mkuu mstaafu wa CCM luteni mst Yussuf Makamba amesema kuwa aliyekua Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa alikua ameshafukuzwa kazi kabla ya kujiuzulu.
Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais za CCM katika kiwanja cha Kawawa mjini Kigoma.
Akifafanua suala hilo mzee Makamba amesema kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM katika kikao kilichokaa mjini Dodoma, baada ya kuridhika kuwa Lowasa alihusika na kashfa ya Richmond,iliteua watu watatu kwenda kumuona Rais Kikwete kumueleza kuwa kwa maslahi ya nchi na chama amfute kazi Waziri Mkuu wake Edward Lowasa kwakua kamati ya uongozi imeridhika kuwa alimuita na kashfa ya Richmond na kulifedhehesha taifa.
Watu hao watatu walikua katibu mkuu wa CCM wakati huo mzee Makamba, mzee Samuel Malecela na mama Anna Abdallah.
"Tulipofika kwa Rais Kikwete tulikutana na Lowasa nje akitokea ndani kwa Rais, tukaingia na kumkuta bwana mkubwa. Tukapewa kahawa. Kisha tukamueleza kuwa tumetumwa na kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kuwa Waziri mkuu amehusika na kashfa ya Richmond na kwa heshima ya CCM na taifa amfukuze kazi.
Rais Kikwete akatuuliza,
...hamjakutana nae hapo nje?
Tukajibu...tumekutana nae anatoka...
Akasema...nimekwisha kumwambia kuwa kwa heshima ya taifa na CCM hawezi kuendelea kuwa waziri mkuu tena na kwamba nateua waziri mkuu mwingine...
Makamba alisema kuwa baada ya Rais kumfukuza kazi Lowasa, kesho yake asubuhi Lowasa aliamkia bungeni na alipopewa nafasi ya kujitetea alisema tatizo nu uwaziri mkuu na kwamba amemuandikia barua Rais aachie ngazi.
"Ukweli ni kwamba Rais alishamfukuza kazi Lowasa usiku wa kuamkia siku aliyotangaza kiachia ngazi na kujiuzulu. Lakini tuliamua kumsitiri. Sasa kwakua kaamua kusema, nasi tumekuja kueleza akiba tuliyoweka."

Na Mwandishi wetu,
Kigoma
 
Back
Top Bottom