Ujue mgogoro kati ya Elon Musk na Serikali ya Brazil hadi Brazil kutishia kuwafunga wafanyakazi wa x (Twitter).

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,340
Siku chache zilizopita kumeibuka mgogoro wa kimahusiano kati ya mmiliki wa mtandao wa X ama Twitter Bwana Elon Musk na Serikali ya Brazil.

Mgogoro huo umepelekea serikali ya Brazil kupitia Jaji wa Mahakama Kuu Bwana Alexandra Morales kutishia kuwaweka ndani wafanyakazi wa X na kuipiga X fine iwapo itashindwa kutimiza amri za mahakama.

Mgogoro huo ulianza baada ya mahakama kuu ya Brazil kupitia kwa Jaji Morales kuagiza mtandao wa X kufungia akaunti za wabunge kadhaa na waandishi wa habari na watu wengine maarufu nchini Brazil ambao wanaikosoa Serikali ya Rais Lula.

Awali mtandao wa X ulitii amri ya mahamaka ya kufungia na kufuta baadhi ya machapisho ya hao watu walioorodheshwa kwenye amri ya mahamaka. X iliweka wazi kwamba imechikua hatua hizo kutii amri ya mahamaka lakini watafuatilia kujua amri hiyo ilitolewa kwa lengo gani na hao watu wamekosea nini hadi mahakama iamue wafungiwe.

Hivyo X kupitia kwa wanasheria wake ikataka ipewe sababu za amri ya mahamaka na kujua vitungu vya kisheria ambavyo hao watu wamevunja hadi wafutiwe akaunti zao wa X. Mahakama ikasema X iwaambie tu hao watu kwamba wamevunja sheria za matumizi ya mtandao(yaani mtandao una kanuni zake ama policy ambazo ukizivunja wanaweza kukufungia, kufuta hiyo andiko lako na kukupa onyo ama watakavyoona wao inafaa).

Mahakama ikaemda mbali zaidi ikasema mtandao wa X usiseme kwamba ni amri ya mahamaka (wakisema hivyo hao jamaa watakaofungiwa watataka hiyo amri ya mahamaka na kujua kwa nini wafungiwe). Mahakama ikataka X ndio iwafungie nyenyewe na isitaje ni amri ya mahamaka na jaji gani kaitoa.

Baada ya Elon kupewa hayo majibu akakataa, akasema hao watu ni watu maarufu na pia wenye ushawishi kwenye jamii mfano wabunge, kuwafungia kwa sababu za uongo kwamba wamevunja kanuni za X wakati sio kweli haiwezekani.

View: https://twitter.com/elonmusk/status/1777383330993914227?s=19

Elon akaamuru akaunti zote zilizofungwa zifunguliwe na akasema ataweka wazi ni kwa namna gani serikali ya Brazil kupitia Jaji Morales inakiuka katiba ya nchi na sheria za nchi kwa kuonea watu, kuwapa tuhuma za uongo na kuwanyamazisha kwa mlengo wa kisiasa.

Baada ya siri hiyo kutolewa wazi, kwanza Mahakama ikatishia kumchunguza Bwana Elon Musk na pia kutishia kuwatia ndani wafanyakazi wote wa X Brazil. Elon amesema atawaondoa wafanyakazi wote wa X nchini Brazil.

Haikuishia hapo, Mwaka jana Serikali ya Brazil na Elon Musk waliingia mkataba wa Elon kutoa huduma ya Internet kwa shule zote za vijiji. Sasa serikali inatishia kwamba haitalipa. Elon amesema wasipolipa yeye atatoa huduma ya Internet kupitia kampuni yake ya Starlink kwa shule za vijiji bure.

Sasa Bunge la Brazil baada ya kujua kwamba wanahujumiwa na Bwana Alexandra Morales, bunge la seneti limeanzisha mchakato wa kumuondoa Morales mapema iwezekanavyo.

View: https://twitter.com/elonmusk/status/1778054291183358439?s=19
 
Siasa !!!😂🤣🤣
Lula kaingia mwaka jana anataka kunyamazisha wapinzani wake wote kwa kulazimisha mitandao ya kijamii na vyombo habari kutowapa nafasi ya kuongea kwa kutumia mahakama.

Mbaya zaidi anaitumia mahakama. Mahakama ambayo ndio mtetezi wa sheria za nchi wao ndio wanavunja sheria za nchi.

Kuna mwandishi mmoja kafungiwa mitandao yote, akaamua afungue akaunti mtandao wa OnlyFans (Mtandao wa Ngono wa kulipia) lakini pia huko amefungiwa kwa kosa la kwenda kinyume na sheria za matumizi(Policy)😂 wakato hajachapisha hata andiko moja.

Elon kawarudisha wote X waendelee kutoa maoni yao bila bugudha na ameahidi hata kama mtandao wa X utafungiwa Brazil sawa tu acha ufungwe.
 
Pesa ina nguvu na jeuri.
Tushukuru Elon anatumia pesa zake kutetea uhuru wa kujieleza kwenye mtandao wake. Hata humu JF Melo amewahi kulala lupango kutetea sisi wanachama wake baada ya serikali kukomaa inataka mawasiliano ya watumiaji wa JF ikawakaange lockup.
 
Lula kaingia mwaka jana anataka kunyamazisha wapinzani wake wote kwa kulazimisha mitandao ya kijamii na vyombo habari kutowapa nafasi ya kuongea kwa kutumia mahakama.

Mbaya zaidi anaitumia mahakama. Mahakama ambayo ndio mtetezi wa sheria za nchi wao ndio wanavunja sheria za nchi.

Kuna mwandishi mmoja kafungiwa mitandao yote, akaamua afungue akaunti mtandao wa OnlyFans (Mtandao wa Ngono wa kulipia) lakini pia huko amefungiwa kwa kosa la kwenda kinyume na sheria za matumizi(Policy)😂 wakato hajachapisha hata andiko moja.

Elon kawarudisha wote X waendelee kutoa maoni yao bila bugudha na ameahidi hata kama mtandao wa X utafungiwa Brazil sawa tu acha ufungwe.
Siasa mchezo mchafu, madaraka yanalevya.
 
Back
Top Bottom