Uingereza na Ufaransa wanaandamana kwa ugumu wa maisha, Lissu na CHADEMA changamkieni tenda ya kutengeneza Katiba Mpya kule

Katiba inaruhusu lakini maza akiamua maandamano yasifanyike yeanasakizia polisi tu, kama alivyokuwa anafanya jiwe na hakuna kitu cha kumfanya.
Sasa tofauti yetu na wenzetu sio katiba nzuri tu, maana hata hiyo katiba nzuri imepatikana kutokana na aina ya watu wao wenyewe. Sasa kama sisi bado hatuja staharabika hatuheshimu katiba ndio tutegemee hiyo katiba mpya ndio itatubadili hivi tulivyo au ina maajabu gani ambayo itazuia isiathiriwe na huku kutokustaharabika kwetu na kutokuheshimu katiba?
 
Miye kiliochangu ni bando tuu tangu Nape apewe rungu tunaibiwa tuuu alafu yeye anatukejeli kama siye watoto. Hata kuweka bando mtu afanye application ya kazi tuu bando la buku mbili halimalizi dk 20 ukiwa umefungua tuu browse ya ajira portal. Hawa jamaa wenye vitambi wajifikiri upya wanatupeleka kubaya hata kama nikuiba Kwa nafasi zao huku kumezidi. Kwani ma v8 hayawatoshi kuzurura nayo mpaka mje mtunyonye siye wa chini huku unakuta siku imekatika umetumia zaidi ya 5000 kwenye bando mtu mmoja kwenye familia kweli tutafika……mwaka jana tuu nilikuwa nikiweka 10,000 bando karibia mwezi namaliza….. mtu wangu alivyoanza onja asali sikuizi hata siku mbili simalizi…..
 
Hao wajinga wakubwa wasiojua kwanini katiba mpya iwepo na wenye kujua kwa nini katiba mpya iwepo unadhani ni kundi gani ndio wako wengi?
Wengi hawajui hata katiba ina maana gani. Mazwazwa wakubwa hao! Upo wapi yakhe!
 
Sasa tofauti yetu na wenzetu sio katiba nzuri tu, maana hata hiyo katiba nzuri imepatikana kutokana na aina ya watu wao wenyewe. Sasa kama sisi bado hatuja staharabika hatuheshimu katiba ndio tutegemee hiyo katiba mpya ndio itatubadili hivi tulivyo au ina maajabu gani ambayo itazuia isiathiriwe na huku kutokustaharabika kwetu na kutokuheshimu katiba?
Walau watu watashitakiwa wakitoka madarakani watakuwa na hofu kufanya uzembe tofauti na sasa. Rais ana immunity akiamua kufukuza kazi watumishi wote hakuna kitu mtamfanya.
 
Hello Wadau,

Binafsi naunga mkono Katiba Mpya ila siungi mkono Katiba Mpya ya kuondoa wahuni wa CCM na kuleta wahuni wa Chadema,nataka Katiba Mpya ambayo ni takwa la Wananchi na mda ndio utaileta watake au wasitake.

Baada ya huo utangulizi, Lisu na Chadema wamekuwa wanawadanganya watu kwamba Katiba Mpya ndio suluhisho na muarobaini wa matatizo Yao ya kiuchumi na kwamba Wao wanapigania Hilo Ili watu wapate neema.

Wamefika mbali wanasema maharage kuwa Juu ni sababu ya Kisiasa kwamba Katiba Mpya itatatua Ugumu wa Maisha, mfumuko wa bei nk.

Sasa huko Uingereza na Ufaransa kwenye Katiba Mpya na Bora watu Wanaandamana Kwa sababu za Ugumu wa Maisha uliosababishwa na mfumuko mkubwa wa bei za chakula na nishati kiasi kwamba uchumi ni mgumu.

Kwa kuwa kina Lissu na Chadema ndio mabingwa wa Katiba za kuleta Maisha Bora Kwa Wananchi,nitoe wito kwao wakachangamkie tenda huko Ufaransa na Uingereza au hata Kenya.

Za kuambiwa changanya na zako,kataa wahuni ogopa matapeli wa Kisiasa👇

Kumbe na wewe ni wale wale!
 
Upumbavu katika hili swali ni sawa na mtoto anayelalamika amefeli kwa sababu shule haikuwa na walimu wa kutosha, vitabu, chakula na madawati ya kukalia halafu mzazi wake anamuambia mbona mwenzake kwenye shule hiyo amefaulu sawa na waliopo Feza na mbona wengine wa Feza wamefili pia kama yeye.
Kuna hoja ya kwamba kila kitu kinahusiana na katiba na hivyo matatizo yetu yanahusiano moja kwa moja na katiba, ndio maana huu uzi unahoji vp kwa hao wenzetu kwamba nao katiba zao zimepungua nini?
 
Wengi hawajui hata katiba ina maana gani. Mazwazwa wakubwa hao! Upo wapi yakhe!
Halafu hapo hapo mnasema hao wasiojua hata katiba ina maana gani ndio mnasema wanataka katiba mpya ila waoga kudai katiba mpya, inawezekanaje hiyo?
 
Upumbavu katika hili swali ni sawa na mtoto anayelalamika amefeli kwa sababu shule haikuwa na walimu wa kutosha, vitabu, chakula na madawati ya kukalia halafu mzazi wake anamuambia mbona mwenzake kwenye shule hiyo amefaulu sawa na waliopo Feza na mbona wengine wa Feza wamefili pia kama yeye.
Ndio umeandika nini?
 
Back
Top Bottom