DOKEZO Uhalifu umezidi sana mji wa Tunduma, Serikali iingilie kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,334
14,271
Wapendwa habari za Jioni? Bila kupoteza muda, Mji huu wa Tunduma ni mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Sasa lengo la Uzi huu ni kuiomba Serikali yetu pendwa ya Mama Dkt.Samia Suluhu Hassani, kuwa kupitia vyombo vya Ulinzi na Usalama watusaidie, Mambo yenyewe yako hivi.

Watu wanatekwa na kupigwa vibaya na kisha kuporwa kila kitu, Wakati Mwingine Muhanga huachiwa majeraha mazito au kuaga Dunia Kabisa.

Kuna visa kadhaa, Mojawapo ilihusu mimi mwenyewe siku ya Jumapili ya tarehe 15/01/2023, mida ya saa tano usiku hivi nilivamiwa kukiwa kumebaki hatua chache kufika nyumbani na watu wawili, ambao walikuwa wamevalia Mask wakanipiga sana nikapiga kelele lkn wapi, Mungu ni mwema nikawaponyoka Baada ya purukushani kali.

Kuna Jamaa yangu alivamiwa hivyo hivyo na kundi kubwa la Vijana wakamdhuru na kumnyang'anya vitu vyake.Matukio ni mengi sana.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI
1. Tunduma ingepewa uangalizi maalumu kiusalama km ambavyo imefanyika huko Tarime, kwa kuundiwa Kanda maalumu. Hii itasaidia sana kuweka hali ya usalama kwani ni mji wa Kibiashara hivyo usalama mkubwa ni suala nyeti ili kuwaondole hofu Wafanyabiashara na hivyo kukuza biashara na Serikali kujikusanyia mapato mengi.

2. Iwekwe kambi ya jeshi km ilivyo kwenye mipaka mingi ya Kagera na Kigoma.

3. Ifanyike operasheni kabambe ya kuteketeza wahalifu km zilivyowahi kufanyika baadhi ya Operasheni siku za nyuma,Mfano mzuri ni ile Operesheni iliyoongozwa na Kamanda Saimoni Siro kule Kagera na Kibiti,Ambao wahalifu wengi walipata cha mtemakuni.

4. Wananchi wahamasishwe kutoa taarifa za Siri kwa jeshi la Polisi na kuwe na utaratibu kutunza taarifa hizo za Siri,na Kuwe na posho hata Kidogo kwa Wananchi wazalendo.

5. Serikali za mitaa ziwabaini vijana wanaoshinda bila kazi maalumu na kisha ziwabane ili kujua wanawezaje kumudu maisha ili hali hawana shughuli maalumu.

Mwisho tuzidi kuomba Mungu, atunusuru na hali hii maana hali si shwari kabisa.

Ni sisi Wananchi wanyonge wa Tunduma.
 
Yaani iwekwe kambi ya jeshi kwa sababu ya vibaka? Jeshi unalichukulia poa sana inaonekana.

Sema iundwe kanda maalum ya kipolisi. Hiyo ni kazi ndogo sana.

Hao vibaka ni mnaoshinda nao na labda hata kununuliana msosi.

Asilimia kubwa ya uhalifu wa hivyo hutekelezwa na wazawa wachache wa eneo husika.
 
Tunduma ni hatari sana usiku hapo. Manjagu usiku wanakua kwenye dili za kukamata magendo kwa hiyo kuona wakizunguka usiku mitaa ya makazi labda waanze kipindi hiki gari zao huwa zinategwa chini pale kuelekea bara bara ya Mpemba ili wapate ridhiki yao ya usiku.
 
Tunduma ni hatari sana usiku hapo...Manjagu usiku wanakua kwenye dili za kukamata magendo kwa hiyo kuona wakizunguka usiku mitaa ya makazi labda waanze kipindi hiki gari zao huwa zinategwa chini pale kuelekea bara bara ya Mpemba ili wapate ridhiki yao ya usiku...
Kuna wakati tulikuwa hapo silver stone Hotel, kuna jamaa alikuja alidai aliibiwa hela,sim na kipondo juu
Kwenye kuwafatilia jamaa walikuwa washavuka upande wa nakonde wenyewe chocho wanazijua

Ova
 
Yaani iwekwe kambi ya jeshi kwa sababu ya vibaka? Jeshi unalichukulia poa sana inaonekana.

Sema iundwe kanda maalum ya kipolisi. Hiyo ni kazi ndogo sana.

Hao vibaka ni mnaoshinda nao na labda hata kununuliana msosi.

Asilimia kubwa ya uhalifu wa hivyo hutekelezwa na wazawa wachache wa eneo husika.
Miji hii ya mipakani na ya kibiashara wezi huwa siyo wazawa.
 
Back
Top Bottom