Uhalali wa muungano bila hati ya muungano

Paul Makonda

Member
Jul 8, 2011
97
186
Uhalali wa Bunge la Katiba Bila Hati halisi ya Muungano

Wajibu wa Vijana kwa Taifa ni Kuleta Tija kwa Taifa na Kuwezesha Vijana wengine wasio na fursa kulinganisha na fursa tulizo nazo. Wajibu wangu nikiwa Kijana ni kuhakikisha Taifa hili linaendelea kukua kiuchumi, kijamii na kisiasa bila kuathiriwa na historia mbaya yoyote lakini ikibebwa na historia yote nzuri.


Tanzania ni Jamhuri ya Muungano uliotokana na maungano ya nchi mbili Tanganyika (Tanzania Bara) na Zanzibar tarehe 26/04/1964. Mchakato wa muungano huu ulihusisha shughuli nyingi na matukio mengi kabla, ndani ya mchakato wakati wa kuunganika na baada ya kuunganika.

Historia ya mahusiano ya nchi hizi mbili inakwenda miaka mingi nyuma mwanzoni mwa 1800 enzi za biashara ya Utumwa. Mpaka mwaka 1860 dola ya Zanzibar ilikuwa ni dola tajiri kuliko zote Afrika Mashariki kutokana na biashara ya Watumwa na Pembe za ndovu. Watumwa na Pembe za Ndovu zilitoka maeneo ya Tanzania bara ya sasa. Harakati za kudai uhuru wa Zanzibar mwishoni mwa karne ya 19 (miaka ya 1950), Tanganyika ilihusika kwa kiwango kikubwa sana. Mfano katika Mkutano wa kuanzisha chama cha Afro Shirazi Party uliofanyika kati ya tarehe 1 hadi 5 February, 1957, mkutano huo ulifanyika nyumbani kwa Sheikh Abeid Amani karume na katika Mkutano huo alikuwepo Mgeni Mwalikwa Rais wa TANU, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Katibu Mkuu wa TANU Ndugu Zuberi Mtevu. Hii ni sehemu tu ya Historia ya mahusiano ya waasisi hawa wa Muungano tangu wakati Mataifa haya yakiwa bado ni makoloni.

Tarehe 10 December, 1963 Zanzibar ilipata Uhuru kwa ajili ya Sultan ambapo waafrika walio wengi waliendelea kuwa chini ya umangimeza wa kisultani hadi tarehe 12 January, 1964. (Waafrika walivumilia kwa mwezi mmoja) na walipofika hiyo siku wakafanya Mapinduzi Matukufu yaliyoiweka Zanzibar huru. Uhuru wa 1963 ulitolewa kwa ZNP/ZPPP. Vyama hivi viwili viliwakilisha tabaka la juu la wanyonyaji miongoni mwa matabaka ya watawaliwa. Vyama vilitetea kubaki usultani, kutambuliwa rasmi Sultan kuwa ni Mkuu wa Dola ya Zanzibar chini ya himaya ya Uingereza na havikupigania kuondoa matabaka na unyonyaji katika jamii. Ni ASP pekee ndiyo ilipinga kabisa kuendelea kuwepo kwa usultani baada ya Uhuru na kudai usawa katika nyanja za kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Uhuru Bandi kwa ZNP/ZPPP ulipelekea kuwepo chuki miongoni mwa wanachama wa ZNP jambo lilopelekea kuundwa kwa chama cha UMMA ambacho kilikufa baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na wanachama wake wote kujiunga na ASP. Hivyo ieleweke wazi, Mapinduzi ya mwaka 1964 yalikuwa dhidi ya SULTAN na WAAFRIKA VIBARAKA waliotumika Kuwanyanyasa Waafrika Wenzao wakiongozwa na Sheikh Muhammed Shamte (Waziri Mkuu). Historia ni ndefu tutatumia muda mrefu kueleza hayo.


Uwepo au Kutokuwepo kwa Hati ya Muungano kwa sasa hakuna Mantiki. Muungano huu ulitokana na mahusiano ya muda mrefu na changamoto za kiutawala na hatari iliyokuwa inaikabili Zanzibar baada ya Mapinduzi. pia Tanganyika ilikuwa ndiyo taifa limetoka kupata Uhuru kwa miaka mitatu tu. Hivyo yote yalifanyika kwa nia njema ya kulinda uswa na ustawi wa watu na mataifa yao.


Leo kudai hati, hakutaongeza wala kupunguza maana ya Muungano. Maridhiano ya makubaliano ya Muungano yalifikiwa kwa sheria namba 22 ya mwaka 1964 iliyosainiwa April, 25 na Marais wa Pande hizi mbili za Muungano. Sheria hiyo ilisainiwa kuafiki matendo yote waasisi hawa waliyoyafanya mfano


Utiaji wa Saini na Ubadilishanaji wa Hati za Muungano;
Uchanganyaji Udongo wa nchi husika
Mikutano mbalimbali ya viongozi hawa

Na yale yote waliyoafikiana kikanuni na kisheria sasa, kilicholeta uhai wa Muungano ni kukamilisha Dili kwa kuutangaza tarehe 26/4/1964.


Sote Tumeapa kwa huo Muungano na kwa tafsiri tu kuwa Muungano upo na ulikuwepo. Tunayoweza kujadili ni mambo yaliyoko katika Muungano na si Kujadili Makaratasi ya Muungano. Kwa uthibitisho wa kuwa matukio haya yalikuwepo, Tutaambatanisha na Picha kadhaa za Mwalimu Nyerere na Sheikh karume katika matukio mbalimbali kuelekea katika Utekelezaji wa masharti waliyoyaweka katika Muungano.


Mwisho! Niwaase wajumbe wenzangu, tuendelee na mjadala wa Katiba Mpya kwa Kutumia Rasimu, Kama kuna hoja ya msingi sana kuhusu Mchakato huu, basi iwekwe mezani si kuweka viashiria vya sababu.

Paul C. Makonda
Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM - 2014


[URL="https://www.facebook.com/photo.php?fbid=621737974579834&set=pcb.621738821246416&type=1"]


[/URL][URL="https://www.facebook.com/photo.php?fbid=621737974579834&set=pcb.621738821246416&type=1"]

[/URL]









Like · · Sh
 
Tunahitaji kuiona hiyo hati. Acha bla bla! Hatudanganyiki na UCCM wenu. We want back our lost Tanganyika
 
hii karatasi (Hati) ndiyo inayohitajika na wajumbe kule Dodoma ili ikajadiliwe upya, hivi mmeificha wapi?

Wana ndoa (watanganyika na wazanzibari) wanataka hati yao ili wayapitie upya maridhiano hayo - sasa gogoro nini wakuu?
 
Hatukutegemea hoja Mbadala kutoka kwako. Wewe ni "mchumia tumbo" kwa tiketi ya CCM na 'Mbwa hutikisa mkia akimuona bwana wake'. Unajua kuwa baada ya Muungano nchi iliitwa "The United Republic of Tanganyika and Zanzibar"?
 
Paulo Makonda, hati ya muungano ni muhimu katika jambo hili. Kwa taarifa yako hata ndoa inapofungwa Kanisani, Msikitini au Bomani (serikalini) picha uwa zinapigwa kweka kumbukumbu ya tukio hilo. Hata hivyo hati/cheti cha ndoa bado kinatolewa kwa wanandoa hao hata kama wameishi miaka mingi pamoja. Vivyo hivyo hati ya Muungano wa Tanzania ni lazima iwekwe mezani wajumbe waione. Vinginevyo huu ni muungano wa kimagumashi. The "Pandora" Box is now open.
 
Hivi ugumu wa kuleta hati mezani uko wapi? Kitendo cha kukataa kuileta mezani na kutokuwa na majibu ya kueleweka tu nahisi vingine
 
Hivi ugumu wa kuleta hati mezani uko wapi na majibu mnayotoa hayaeleweki
 
Acha kutuharibia siku we kijana mvivu wa kufikiri. Uko kwenye mijadala au uko jamii forum? Hiyo hoja sii uitoe huko bungeni? au unajisikia kuwashwa na JF ndomaana hutulii kikaoni?
 
Mbona umeandika Tanganyiga[Tanzania Bara] na (Zanzibar hujaandika Tanzania Visiwani)? au hulijui hilo?
 
Kwa hivo na leo ikitokea Kikwete na Kenyatta wakakaa na kunya uji wakiamua kuziunganisha Tanzania na Kenya poa tu?
 
Harakati za kudai uhuru wa Zanzibar mwishoni mwa karne ya 19 (miaka ya 1950), Tanganyika ilihusika kwa kiwango kikubwa sana.

Miaka ya 1950 ndiyo mwishoni mwa karne ya 19?

Nikishaona utumbo kama huu hapohapo naona muandishi anaweza kukosa umahiri anaojivika kuandika habari pana kama hii.
 
Tatizo hati ilifanywa kama mali ya watu fulan hv.
Mm naona nbora tuandae HATI MPYA na tuchanganye tena udongo.
 
Kwa umri wako na ufahamu wako dogo umejitahidi sana kutetea msimamo wa chama chako ila unakosea pale badala ya kutetea msimamo wa chama chako unataka kutuaminisha kuwa hati ni karatasi tu. hakuna partnership ya hivyo kijana kajipange upya safari hii mpaka kieleweke. Ingekuwa vema mkawa wazi kutetea misiamao ya vyama vyenu bila kujificha na kufanya mnatetea maslahi ya nchi.
 
Sawa kaka umesomeka.
Mm simfuasi wavma hivyo lakin napata kigugumiz ninapo sikia kuwa saini za baba wa taifa na katibu mkuu wa bunge kwa kipindi hicho zinatofautiana.
Hebu nieleweshe hapo.
 
Back
Top Bottom