Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,731
- 29,985
Umofia kwenu.
Mengi yamesemwa kuhusiana na hili sakata la upungufu wa dola nchini. Kimsingi Dola ya Marekani ndiyo inatumika kama fedha ya kununua bidhaa za kimataifa. Mojawapo ya bidhaa hizo ni pamoja na mafuta ghafi ambayo yanashikilia sehemu muhimu ya mfumuko wa bei nchini.
Nasema yapo mengi yamesemwa na wataalam na sisi wataalam pori wa michongo lakini naona katika yanayozungumzwa mengi ni lawama na kauli ambazo hazitoi mwelekeo wa kukabili changamoto hii. Tukiendelea kulaumiana tutaendelea kuathirika wote na kadhia hii.
Kwa nia njema, ninaleta kwenu Great Thinkers wa JamiiForums kwamba maoni na ushauri kuntu uelekeze namna ya kupita huu mkwamo. Inawezekana hoja zetu zikapuuzwa lakini tutakuwa tumetimiza wajibu wetu muhimu kupitia ibara ya 18 ya Katiba ya JMT (1977 na marekebisho yake).
MAONI

- BOT ianzishe hifadhi ya dhahabu haraka ili kukabiliana na tatizo hili, kwani dhahabu inatumika kufanya exchange ya forex kunapotokea nakisi
- Serikali itoe sapoti na msukumo kwa bidhaa zote za export hususan zile zilizopo kwenye mfumo wa Fair Trade ili wazalishaji waweze kuexport kwa wingi.
- Chakula chochote kinachonunuliwa kwa kusafirisha nje kinunuliwe kutoka ghala za serikali tena kwa dola. Hivyo serikali itenge fedha ya dharura kununua kutoka kwa wakulima ili all food crop export itoke kwenye maghala ya serikali.
- Serikali iichunguze kampuni ya forodha ya SILENT OCEAN hususan mwenendo wake wa biashara wa miezi 24 iliyopita kwani imenyooshewa vidole kusafirisga dola nje ya nchi kwa njia haramu.
- ............