Ufugaji wa Bata: Aina za bata, ujuzi, gharama, changamoto, faida na masoko

Asante mkuu kwa jinsi ninavyofahamu hawa bata wametofautiana,
kuna bata wanaitwa bata bukini ni wazuri kimuonekano na hata bei yake imechangamka. Ukifuga hao wanazaliana kwa wingi vilevile utauza kwa bei ya juu, hata hawa bata wetu wa kienyeji pia wanazaliana kwa wingi mno, kibongobongo hawa unaweza kupata masoko yake humuhumu uswahilini kwetu.
Wale bukini ukitaka kuuza inabidi usogee mjini kidogo huko utapiga ela ndefu.
 

Attachments

  • DSC_0830.JPG
    DSC_0830.JPG
    156.2 KB · Views: 206
1)Hivi nikifuga bata wa kawaida lazima niwatengenezee sehemu ya wao kuchezea maji?maana kuna eneo hapa nyumbani la wao kujiachia kwenye nyasi huku wakizila kama chakula ila sina hakika kama natakiwa niweke pia na bwawa la maji ili wacheze humo
2)Je bata sio waharibifu wa migomba?eneo ambalo ninampango wa kujenga banda lipo karibu na migomba na sitaki kuipoteza(i.e sitakuwa nawafungia kwenye banda muda wote,nitakuwa nawaachia nje,hawataratibu migomba?)
wenye uzoefu tafadhali mnijuze
 
1)Hivi nikifuga bata wa kawaida lazima niwatengenezee sehemu ya wao kuchezea maji?maana kuna eneo hapa nyumbani la wao kujiachia kwenye nyasi huku wakizila kama chakula ila sina hakika kama natakiwa niweke pia na bwawa la maji ili wacheze humo
2)Je bata sio waharibifu wa migomba?eneo ambalo ninampango wa kujenga banda lipo karibu na migomba na sitaki kuipoteza(i.e sitakuwa nawafungia kwenye banda muda wote,nitakuwa nawaachia nje,hawataratibu migomba?)
wenye uzoefu tafadhali mnijuze
Ni waharibifu wazuri tu, hasa kwa migomba midogo

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
UTANGULIZI

Habari zenu wanajamvi, kwanza napenda kudeclare interest mimi ni mfugaji mchanga wa Bata, na nilifikia uamuzi wa kufuga bata baada ya maradhi kuwapiga kuku wangu na wakafa wote. Nimepitia threads nyingi sana za humu na sijaona special thread inayoongelea bata na bila hiyana nimemua kuileta ili wafugaji bata na wataalam tukutane hapa kupeana ujuzi. Bata ni ndege mtamu nadhani kushinda hata kuku, watu wengi wanapenda kumla bata ila hawataki kabisa kumfuga kutokana na mazingira yake. Ufugaji wa bata una faida na unaweza kukufanya ukawa Tajiri ndani ya kipindi kifupi.

MAGONJWA YA BATA
Lazima tuelewe magonjwa anayopata kuku na jamii ingine ya ndege bata pia hupata, tofauti ya bata na ndege wengine wana uwezo wa kuhimili magonjwa, yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ya bata;

1. Duck Viral hepatitis.
Ugonjwa huu unawashambulia vifaranga vya bata ambavyo vipo chini ya wiki 6, utakuta vifaranga wanakosa nguvu ya kusimama, kutembea na hatimaye vifo.

2. Aflatoxins Poisoning
Ugonjwa huu ni pale unapompa kifaranga pumba yenye madonge madonge ambayo ukiichunguza utakuta tayari imeanza kuweka kijani, hii ni sumu kabisa na haichelewi kumuondoa bata.

3. Cholera
Ugonjwa huu ni hatari kwa bata wadogo, utakuta bata wanajinyonga shingo na kuanguka.

4.Bata pia hushambuliwa na wadudu (parasites) mbalimbali ambao hupatikana ndani na nje ya mwili wake mfano viroboto, utitiri, chawa, ukurutu n.k ndani ya mwili anaweza kupata minyoo ya kwenye utumbo na maini.

5.Yapo magonjwa mengine hatari ya bata kama Duck viral enteritis, Aspergillosis, Collibasillosis n.k. kwa wale tunaofuga unaeza ambiwa bata ana matatizo ya mifupa, mafua, Typhoid au hata Pneomonia.

Magonjwa mengi ya bata husababishwa na ukosefu wa Vitamins, Madini na bila kusahau uchafu.

DAWA ZA KUWATIBU

Zipo dawa nyingi sana ambazo zinaweza kusaidia/kuokoa au kuimarisha hasa maisha ya vifaranga vya bata.

1. DCP
Dawa hii imeonyesha uwezo mkubwa sana wa kuwakinga na kuwaimarisha bata katika miili yao hasa mifupa yao maana ina Calcium+Phosphorous. Matumizi yake unachanganya tu kwenye pumba.

2. Amin'total
Ni dawa moja nzuri sana inayosaidia absorption ya DCP ktk utumbo wa bata kwakuwa ina kiwango kikubwa cha D3. Dawa hii ni expensive kama una bata wachache si vema kuinunua kama unajiweza unaweza kuinunua.

3. Fluban (enrofloxaxin)
Imethibitika ni dawa nzuri sana hasa pale bata wanapopata typhoid. Ni dawa yenye nguvu na inatibu haraka.

4. Ivermectin
Ni dawa iliyoonyesha uwezo wa kuua wadudu wote wanaomdhuru bata ndani na nje kwa mkupuo.

5. Neoxychick
Ni dawa inayofanya vizuri hasa kukuzia bata wadogo, dawa hii ni antibiotics na ina Vitamins, na Minerals. Pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kama mbadala wa dawa hii ikiwa tu uchumi wako hauko vizuri, unamenya kitunguu swaumu, kitwange kisha changanya na maji, wape vifaranga siku3 za kwanza baada ya kuzaliwa.

6.Piperazine
Hapa wafugaji wa sungura watakuwa wamenielewa, hii ni dawa moja nzuri na inayoonyesha matokeo ya haraka. Ni dawa inayoua minyoo ya aina zote. Mimi binafsi napendelea kuitumia hii kwa bata wangu.

DAWA ZINGINE MUHIMU PALE UNAPOONA MABADILIKO YA BATA WAKO NI OTC, TYLOSIN, LIMOXIN, NA DOXCOL. Hizi zinatibu magonjwa mengi.

NADHARIA/IMANI/MISEMO
Kuna maneno mengi sana husemwa huko mitaani hasa kuhusiana na bata na kuna Imani zipo ktk jamii kwamba unapotaka kumchinja bata usimuonyeshe kisu kwani nyama yake itakuwa chungu sana, Wengine husema bata akitaga mayai yake anayahesabu na ukichukua mayai yake kila siku basi itafika kipindi atasusa kutaga na atapata stress ambazo zinaweza mfanya Asitage kwa muda mrefu, Wengine husema wakati wa kumnyonyoa bata haitakiwi kuongea maana mkiongea basi ataota tena manyoya mengine, Pia kuna wengine husema bata wa ukoo mmoja wakipandana inaweza kuwa chanzo hasa cha vifo vya bata wadogo, Yote kwa yote misemo ipo mingi tu inayoongelea bata japo mimi binafsi sitaki kusema lolote kuhusu hiyo misemo.

MUHIMU UNAPOFUGA BATA

1. Hakikisha maji wanayokunywa ni safi pia jitahidi kuwabadilishia maji mara kwa mara.
2. Hakikisha vyombo vya maji na chakula viwe safi muda wote.
3.Wape chakula safi na cha kutosha ili kuboresha ukuaji wao
4.Pia muhimu sana hasa kwa bata wadogo na wakubwa kuwachanganyia damu iliyokaushwa, chokaa, mifupa na mashudu ya alizeti ikiwezekana ili waweze kupata madini ya Calcium + phosphrus na trace Minerals. Pia itafanya bata wasiwe na hamu ya kula mayai. Na vilevile mchanganyiko huu unasaidia kupevusha mayai ya bata hivyo bata huwai kutaga mayai.
5.Vifaranga vikizaliwa unaweza kuvipa antibiotics kuzuia magonjwa na bacteria pia usiache kuwapa Vitamins ili kuwaongezea hamu ya kula na kinga ya magonjwa.
6. Unga wa sulphur umeonyesha matokeo mazuri hasa katika kuwalinda na bacteria.
7. Intensive System.. inashauriwa kama unajiweza ufanye ufugaji wa ndani wa bata hii itakupa matokeo mazuri na ya haraka.
8.Vifaranga vya bata havitakiwi kuoga au kunyeshewa na mvua kwa muda angalau wiki 10 za kwanza baada ya kuzaliwa.
9. Kipindi cha wiki 2 za kwanza vifaranga vya bata havitakiwi kupata baridi kama banda lako halina joto la kutosha unaweza kuwawekea majiko ya Mkaa ili kuwaongeza joto.
10.Hakikisha banda lako halina matundu yanayowawezesha panya kupita, Panya huwa wanawadhuru vifaranga wadogo hasa walio chini ya wiki mbili.
11. Changamoto kubwa ya bata ni chakula kwanza wanazaana kwa kasi, inabidi angalau uandae gunia la pumba pamoja na virutubisho vya kutosha. Pia bata wanakula sana majani hata kama unafugia ndani jitahidi siku moja moja uwe unawakatia majani hawa bata wa kienyeji ni sawa na kuku huwaga wanapenda kula majani.
12.Vifaranga wa bata hawatakiwi kula pumba iliyochanganywa na maji, kwa kufanya hivyo unawahatarishia maisha.

NB; MAGONJWA YOTE YA BATA YANAWEZA KUZUILIKA KWA USAFI TU. NA LAZIMA TUKUMBUKE BATA SIO MCHAFU ILA WEWE MFUGAJI NDIO MCHAFU.

AINA ZA BATA
Wapo bata wa aina mbalimbali ila hapa nitataja chache tu. Tukianza na bata wa kienyeji ambao kila mtu anawajua. Bata wengi wa kienyeji wanataga mayai 10 hadi 12 na mara nyingi wanataga alfajiri, bata hawa hutotoa watoto kuanzia 8+, wafugaji wengine wamebahatika kupata mbegu tofauti za hawa bata hivyo wanasema bata hawa wana uwezo wa kutaga mayai hadi 30.
Pia kuna bata wanaitwa Pekin, hawa asili yao ni china hapa Tanzania wapo ila sio wengi sana.
Aina ingine ya bata ni Bukini hawa sasa watu wengi wanawafuga kibiashara, na pia wana gharama hata kuwanunua kwake. Chakula Chao kikubwa majani.
Aina ingine ya Bata ni bata mzinga hawa ni gharama sana kuwafuga, tena wakiwa wanakua ndio balaa inatakiwa uwe na chakula cha kutosha ndani kwani wanakula mno, asilimia kubwa ya waliojaribu kuwafuga hawakufikia malengo yao kutokana na gharama ya chakula na magonjwa, bata mzinga hutaga mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza, akitaga kwa mara ya pili hutaga mayai 25 hadi 30, na analalia kwa siku 28, siku ya 29 hadi 31 ni siku ambazo mayai hutotolewa, ikifika siku ya 32 kama mayai yamebaki basi hayo ni ya kutupa.
Aina ingine ya bata ni mchovya hawa wana midomo ya njano, Tabia zao hazitofautiani sana na bata wengine.

MASOKO NA BEI
Maneno mengi husemwa kwamba bata mchafu wengine husema sio mtamu, basi tu ili mradi kila mtu anasema yake, bata wana masoko sana hasa wageni wanapenda sana bata, shida ya upatikanaji wake ndio imesababisha bata waonekane wana bei sana na kama chakula cha anasa, tufuge bata kwa wingi ili upatikanaji wake usiwe wa kusua sua. Na pia bata wakiwa wengi na bei ikiwa ya kawaida itafanya watu wale bata kwa wingi.

HITIMISHO
Kupitia thread hii wale wote wanaofuga au wanaotarajia kufuga bata tukutane kushea mambo mbalimbali yahusuyo bata. Pia natoa wito Kwa moderators wa JF waweke PIN hii posti iwe juu kwa ajili ya sisi wapenzi wa kula na kufuga bata. Wataalam wa mifugo wanakaribishwa kutoa mawazo yao mbali mbali yahusuyo mfugo huu adhimu.

NAWASILISHA.
Mkuu mie nahitaji kufuga njiwa, kama una elimu hiyo unaweza nipatia!
 
Wadau kama kuna mtu ana mbinu ya kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo mjini tupeane. Hii ni kikwazo kikubwa kwa wafugaji wa mjini pengine kuliko hata magonjwa.
Kwa ushauri wangu mimi kupunguza ama kuzuia wizi wa mifugo
1.Kujenga mabanda imara
2.Kuweka ulinzi kwa mifugo yako
3.Kutumia mfumo wa kufugia ndani na sio mfumo huria unawaruhusu wanyama wako kuzurula hapa na pale
 
Offcoz ni vizuri ukaweka sehemu ya wao kuchezea maji maana bata wanapenda maji maji na pia haina shida kuwafuga kwenye migomba we fuga tu
1)Hivi nikifuga bata wa kawaida lazima niwatengenezee sehemu ya wao kuchezea maji?maana kuna eneo hapa nyumbani la wao kujiachia kwenye nyasi huku wakizila kama chakula ila sina hakika kama natakiwa niweke pia na bwawa la maji ili wacheze humo
2)Je bata sio waharibifu wa migomba?eneo ambalo ninampango wa kujenga banda lipo karibu na migomba na sitaki kuipoteza(i.e sitakuwa nawafungia kwenye banda muda wote,nitakuwa nawaachia nje,hawataratibu migomba?)
wenye uzoefu tafadhali mnijuze
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom