#COVID19 Uchumi wa Kenya washuka sababu ya Coronavirus. Mzunguko wa Biashara wapungua

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,509
9,296
Ukuaji wa uchumi Kenya umeshuka kwa kiwango cha asilimia 0.3 mwaka 2020 kutokana na athari za janga la virusi vya corona, licha ya uchumi huko kukua kwa asilimia 5 mwaka 2019.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa na Waziri wa Fedha, Ukur Yattani, kiwango cha mfumuko wa bei kilipanda kutoka asilimia 5.3 mwaka 2019 hadi asilimia 5.4 mwaka 2020 kutokana na mikakati ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, iliyodumaza usambazaji wa bidhaa.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021 zinazoangazia mwaka 2020 kuhusu maendeleo ya uchumi Kenya, pato la taifa kutoka sekta ya utalii limepungua kwa asilimia 43.9 hadi shilingi bilioni 91.7 mwaka 2020 huku idadi ya wageni kwenye mahoteli ilipungua kwa asilimia 58.0 mwaka huo hadi watu milioni 3.8.

Idadi ya wageni waliowasili Kenya mwaka 2020 ilipungua kwa asilimia 71.5 hadi 579,600 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Kiwango cha biashara kilipungua hadi shilingi trilioni 2.29 huku thamani ya bidhaa zilizoingizwa Kenya ikiwa ni shilingi trilioni 1.64 wakati thamani ya bidhaa zilizosafirishwa nje ya nchi ikiwa ni shilingi trilioni 0.64.
 
Back
Top Bottom