Uchambuzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuhusu 'Video ya Gwajima' unatia shaka sana!

Ngosha Mchambuzi

New Member
May 25, 2019
2
15

1107661

Mrejesho/Mapitio ya uchambuzi ulifanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuhusu video inayodaiwa ni ya Aksofu Gwajima
Utangulizi:
Nimesoma taarifa/report inayojieleza kwamba ni uchambuzi uliofanywa na wataalamu wa uchambuzi wa usalama wa mifumo ya kompyuta na mitandao (Cyber Security Experts) wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Sina hakika kama taarifa hii imeingia mitandaoni kwa bahati mbaya au kwa makusudi (tazama kiambatanisho kwenye uzi huu), lakini kwa vyovyote vile, kwa kuwa imeoneshwa kwamba ni kazi ya kitaalamu, basi kazi hiyo inawajibika kupitia uchambuzi na mrejesho wa kitaaluma kutoka kwa wasomaji na wataalamu.

Aidha, kwa kuwa jambo hili limekuwa kwenye mjadala wa kitaifa kwa wiki kadhaa sasa, mimi nitatoa mrejesho kwa lugha ya Kiswahili ili watanzania walio wengi wasio na uelewa na kiingereza waweze kusoma. Pia, nitajitahidi kutumia lugha nyepesi kupunguza makali ya lugha za kitaaluma ambazo wakati mwingine tunazitumia kuficha mambo kwa wasio wanataaluma.

ANGALIZO: Mrejesho huu haulengi kusema iwapo video husika ni ya aliyeshutumiwa ua la bali unajikita katika sayansi ya uchambuzi kama inavyoonekana kwenye ripoti husika. Hitimisho la uhalisia wa video sio jukumu langu!

Mrejesho/Mapitio ya uchambuzi
Naomba nijikite kuchambua kilichoandikwa kwenye ripoti hii kwa misingi ya kuhoji makusudi ya uchuambuzi huu, methodolojia ya uchaumbuzi, Ushahidi uliotumika, hitimisho la wachambuzi husika, na uwasilishwaji wa uchambuzi.

Lengo la uchambuzi:
Kilichoandikwa:
Ripoti hii inaonesha kazi ya uchambuzi ilifanyika kama mwitikio wa Jeshi la Polisi kuthibitisha uhalisia wa video iliyodaiwa ni ya Askofu Gwajima.
Tatizo/Mrejesho: Inafariji kuona kuwa vyombo vyetu (kama ni kweli) vinatumia wataalamu tulio nao katika kutafuta ukweli wa mambo yenye maswali magumu ya yasiyoweza kutatuliwa bila Ushahidi wa kisayansi. Hili ni jambo jema sana.

Methodolojia:
Kilichoandikwa:
Wachambuzi wameanza kazi yao kwa kutoa utangulizi unaoonesha uhasi au ubaya wa mitandao ya kijamii (walikuwa so negative mapema kabisa). Utangulizi wao unaonesha uchambuzi umefanywa kwa fikra kwamba intaneti na mitandao ya kijamii ni eneo hatari na kunahitaji jeshi la kukabiliana nayo. Tumbuke malengo ya uchambuzi huu hayakuwa ‘Matumizi ya mitandao ya kijamii’ bali ni ‘Uhalisia wa video inayodaiwa kuwa ya Askofu Gwajima’.
Tatizo/Mrejesho: Haya ni makosa makubwa sana kitafiti. Moja, huwezi kuanza utafiti ukiwa tayari una majibu ambayo yameegemea upande mmoja unaoutaka. Pili, katika uwasilishaji wa kazi ya kisayansi huwezi kutoa utangulizi wa jambo ambalo siyo lengo la kazi ya utafiti uliyofanya. Video hii bado ingeweza kupatikana bila mitandao ya kijamii na mitandao ya kijamii siyo teknolojia ya kutengeneza video feki bali ni njia ya mawasiliano/usambazaji. Mchambuzi angejikita katika kuueleza umma juu ya sayansi ya kutengeneza video feki.

Njia:
Kilichoandikwa:
Wachambuzi wameanza kazi yao bila kutuambia waliongozwa na nini katika uchambuzi ili kumsaidia msomaji aweze kufuatilia kinachofuata.
Tatizo/Mrejesho: Uchambuzi wa kisayansi lazima kuwe na vitu vinavyokuongoza.
  • Moja ni lazima kuwepo na swali au lengo. Kwenye uchambuzi huu lengo liko wazi.
  • Pili lazima ujikite kwenye mambo mahsusi yanayolengwa na uchambuzi maana huwezi kutafiti kila kitu.
  • Tatu, lazima uoneshe nini kinatumika kama kipimo (metrics) kurejea na kusema majibu uchambuzi yakoje.
  • Nne, lazima useme kwanini kipimo hicho ndio sahihi kwa uchambuzi huo na sio vinginevyo. Kwa mfano, kwenye uchambuzi huu, wataalamu wangetakiwa waseme kitalaamu nini kinathibitisha kwamba video au picha ni feki au halisi na kwanini. Pia watuambie njia za kuthibitisha ni zipi, za aina ngapi, na kwanini wao wamechagua vipimo waliyotumia.
Vipimo
Kilichoandikwa:
Hata hivyo kunaonekana vigezo vitatu walivyotumia kama vigezo vya uchambuzi wao, navyo ni:
  • Mtizamo wa mchambuzi kwa watu wanaonekana kwenye video (content);
  • Sauti zinazoikika (sound), na
  • Picha mnato walizochukua kwenye video.
cap2.PNG

Uchambuzi:
  • Kigezo cha kwanza cha mtizamo ni very subjective maana kinategemea maoni na fikra zinazomwongoza mchambuzi.
  • Tatizo: Mwanzoni tumeshaona mchambuzi ana fikra gani katika kazi yake hivyo tayari alishatuonesha atatoa hitimisho gani kwenye kinachoonekana kwenye video.
  • Kigezo cha pili cha sauti (sound). Mchambuzi katumia mawimbi/masafa (frequencies) ya sauti zinazosikika kwenye video kama kigezo cha kupima iwapo video imetengenezwa au ni halisi.
  • Tatizo: Mchambuzi anatoa hitimisho kwamba katika muda tofautitofauti wa tukio kulikuwa na sauti zinazotofautiana ukumbwa wa mawimbi. Sijajua mchambuzi katumia sayansi gani lakini hakuna mtu anayetoa sauti yenye masafa yanayofanana muda wote. Mawimbi ya sauti yanachoonesha nguvu iliyotumika kutoa sauti husika. Hivyo nikiongea taratibu mawimbi yatakuwa madogo na nikiongea kwa sauti kubwa mawimbi yatakuwa makubwa pia. Nikiongea kwa kupunguza na kuongea sauti mawimbi nayo yataonesha kupanda na kushuka. Sasa ni kwa namna gani mchambuzi anataka kutuminisha kuwa sauti za wahusika zilitakiwa ziwe na mawimbi yanayofanana muda wote? Kwani walikuwa wanaimba kwaya inayoratibiwa utoaji wa sauti? Pili, mchambuzi anatumbia kwamba pitch au ukali wa sauti unaotolewa haufanani na ukali wa sauti ya Gwajima. Hata hivyo hajatuambia sauti ya Gwajima ina pitch ya aina gani na kwanini Gwajima awe na pitch inayofanana muda wote anapotoa sauti.
  • Kigezo cha tatu (picha mnato): Mchambuzi kachukua picha mnato za video na kujaribu kuzichambua akitumia uzito wa muonekano wa rangi(colour intensity) na tofauti ya rangi hizi katika objects zinazochunguzwa.
  • Tatizo: Mchambuzi hajatuambia kwanini kutumia picha mnato wa video ni njia sahihi ya kupima iwapo video sio halisi. Pili, hajatuambia kwamba sayansi, ushahidi wa kitafiti na matakwa ya kifaa alichotumia kufanya uchambuzi vinasema kwamba kwenye picha moja yenye objects tofautitofauti, ni lazima colour intensity ifanane kwa kila object. Tatu, hata kama ni hivyo sayansi haikubaliani na hitimisho hilo kwani uzito wa muonekano wa rangi kwenye images unategemea vitu vingi. Mojawano ni ukweli kwamba kila object iliyoko kwenye picha ina rangi yake, texture, na muonekano wake tofauti na vingine. Mwanaume aliye juu ya mwanamke ana ngozi tofauti kimuonekano na texture yake pia. Hivyo hawawezi kufanya reflection au kuakisi rangi zinazopafana kwenye mionzi inayotumwa na kamera iliyokuwa inachukua video. Nne, sio kweli kwamba tofauti ya rangi inaonekana kwenye wata pekee. Ukitazama images mchambuzi alizozitumia, utaona uzito wa rangi zinazotoka kwa manamke ni tofauti na za mwanaume na ni tofauti na za mazingira (ukuta/mapazia). Pia katika object moja kuna rangi tofautitofauti kutokana na ukweli kwamba hizo sio flat objects. Miili ina mikunjo. Hata ukitazama picha ya tano na ya nne kwa object/mtu huyohuyo, bado utaona zinatofautiana uzito wa rangi kwenye eneo hilohilo maana mchambuzi kazichukua wakiwa kwenye movements za tendo walilokuwa wanafanya hivyo ni wazi kinachokua reflected kwenye camera kitatofautiana pia.
Uwasilishaji wa uchambuzi
Taarifa/ripoti ya uchambuzi huu wa kisayansi umejieleza kwamba umetolewa na Kitengo cha Uchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Kinachoshangaza kidogo hakuna jina la mtu au watu waliofanya utafiti!

caps.PNG

Tatizo: Katika kazi za kisayansi, hakuna utafiti au kazi kitafiti inayofanywa na taasisi. Hufanywa na watafiti ndani ya taasisi. Uwajibikaji wa kazi ya kisayansi hauendi kwa taasisi bali kwa mtafiti aliyefanya kazi husika. Kwa mfano, iwapo kuna swali la kisayansi kuhusu kazi hii, watu hawawezi kumuuliza mkuu wa chuo wala kila mwalimu kwenye kitengo husika. Anatakiwa kuulizwa aliyefanya utafiti na kutoa ripoti hata kama inawakilisha taasisi. Kitendo cha watafiti kutoa ripoti na kuficha utambulisho wao, tayari kinaleta maswali kitafiti. Pia kinaleta maswali juu ya umakini wa taasisi iliyokubali aina hii ya uwasilishaji wa kazi ya kisayansi.

Hitishimo la Mrejesho:
  • Uchambuzi huu umefanywa na mchambuzi au wachambuzi ambao tayari walikuwa wana majibu ya wanachotaka kuwaeleza waliowapa kazi au wasomaji wao. Mtizamo wao ni hasi kuanzia mwanzo. Badala ya kujielekeza katika sayansi ya uchambuzi wa picha (image processing and analysis) wao wamejielekeza kwenye siasa na vita dhidi ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
  • Pili, uchambuzi huo hauko wazi ulikuwa unatazama vitu gani mahususi vinavyokubalika na kuthibitika katika sayansi husika kupima uhalisia wa video. Badala ya uchambuzi wa video na teknolojia husika, wamechambua picha waliyopiga kwenye video. Mchambuzi katumia kifaa cha kuchambua picha mnato kuthibitisha uhalisia wa video (picha mjongeo)
  • Tatu, mchambuzi hajatoa vigezo au vipimo (metrics) vinavyotumika kisayansi kuthibitisha uhalisia wa video.
  • Nne, hitimisho la mchambuzi kuhusu matokeo ya uchambuzi wake vimeegemea upande aliotaka na amejiepusha na kujikita kwenye ukweli wa kisayansi unaonekana kwenye uchambuzi aliyofanya yeye mwenyewe. Mchambuzi anatoa mahitimisho yasiyopata support/ushahidi wa anachochambua.
Mwisho:
Katika historia ya ulimwenngu na maendeleo yake, wanataaluma na hasa wanazuoni walio katika Vyuo Vikuu wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye maendeleo hasa ya ukuaji wa sayansi na teknolojia. Hawa ndio wanatakiwa kuwa mboni ya jicho na kimbilio kwa Taifa hasa katika mambo yanayohitaji utaalamu, ushahidi na ushauri unaotolewa katika misingi ya ukweli na kuthibitika kisayansi/kitafiti.

Ni vema wanazuoni wakakumbuka wajibu wao kila mara wanapofanya kazi zao ili kuendelea kuipa jamii imani kwamba kazi zao zinalindwa na misingi ya taalamu na utafiti na sio vinginevyo. Wanataaluma wanatakiwa kuwa wakweli muda wote. Hata inapotokea wamepewa au wanatakiwa kufanya utafiti lakini hawana uwezo na uatalamu husika, wanategemewa kuwa wazi kusema hivyo bila uoga na sio vinginevyo. Hii inaeleweka na kukubalika kabisa hasa kwa taaluma ngumu kama ya sayansi za kompyuta. Pia ni vema wakumbuke, kazi za kitafiti zinawajibika kwa kila mtafiti na sio amri ya kumi na moja kwamba wanachosema ndio hitimisho.

Kuna msemo uliozoeleka kwamba “kazi ya kitafiti inapimwa na utafiti mbadala”. Pamoja na kauli hii kuwa na sehemu ya ukweli, lakini haina ukweli wote. Ukweli wote ni kwamba kazi ya utafiti inaweza kupimwa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na maana na lengo la utafiti wenyewe; njia au methodolojia iliyotumika na inavyoshabihiana na lengo la utafiti; matokeo ya utafiti inayoonesha nini; na nini tafsiri ya mtafiti katika matokeo ya utafiti wake. Habari ya kufanya utafiti mbadala kama kigezo cha kutofautiana na anachosema mtafiti, ni hatua ya mbali sana na ni iwapo tu, vigezo nilivyotangulia kuvitoa havioneshi iwapo kuna shida katika kilichowasilishwa.

Angalizo: Mrejesho huu umetolewa kwa mtizamo kwamba ripoti husika imetoka Chuo Kikuu cha Dodoma hivyo unastahili mrejesho wa kitaluma. Hata hivyo sijaweza kuthibitisha chanzo hasa cha ripoti hii; iwapo haijatoka UDOM basi uchaumbuzi wangu unamjibu yeyote aliyehusika kuandaa ripoti hii na kuamua kujificha nyuma ya jina la chuo cha UDOM.

Naitwa Ngosha Mchambuzi (Niandikie kupitia ngoshamchambuzi@gmail.com)
 
Attachments

  • Bishop Gwajima-Analysis.pdf
    577.4 KB · Views: 74
Embu weka video ya gwajiboy uno feni mbovu tuone anavyotia mavituuuuzzz
 
View attachment 1107661

Mrejesho/Mapitio ya uchambuzi ulifanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuhusu video inayodaiwa ni ya Aksofu Gwajima

Utangulizi:

Nimesoma taarifa/report inayojieleza kwamba ni uchambuzi uliofanywa na wataalamu wa uchambuzi wa usalama wa mifumo ya kompyuta na mitandao (Cyber Security Experts) wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Sina hakika kama taarifa hii imeingia mitandaoni kwa bahati mbaya au kwa makusudi, lakini kwa vyovyote vile, kwa kuwa imeoneshwa kwamba ni kazi ya kitaalamu, basi kazi hiyo inawajibika kupitia uchambuzi na mrejesho wa kitaaluma kutoka kwa wasomaji na wataalamu.

Aidha, kwa kuwa jambo hili limekuwa kwenye mjadala wa kitaifa kwa wiki kadhaa sasa, mimi nitatoa mrejesho lugha ya Kiswahili ili watanzania walio wengi wasio na uelewa na kiingereza waweze kusoma. Pia, nitajitahidi kutumia lugha nyepesi kupunguza makali ya lugha za kitaaluma ambazo wakati mwingine tunazitumia kuficha mambo kwa wasio wanataaluma.

ANGALIZO: Mrejesho huu haulengi kusema iwapo video husika ni ya aliyeshutumiwa ua la bali unajikita katika sayansi ya uchambuzi kama inavyoonekana kwenye ripoti husika. Hitimisho la uhalisia wa video sio jukumu langu!

Mrejesho/Mapitio ya uchambuzi

Naomba nijikite kuchambua kilichoandikwa kwenye ripoti hii kwa misingi ya kuhoji makusudi ya uchuambuzi huu, methodolojia ya uchaumbuzi, Ushahidi uliotumika, hitimisho la wachambuzi husika, na uwasilishwaji wa uchambuzi.

Lengo la uchambuzi:

Kilichoandikwa:
Ripoti hii inaonesha kazi ya uchambuzi ilifanyika kama mwitikio wa Jeshi la Polisi kuthibitisha uhalisia wa video iliyodaiwa ni ya Askofu Gwajima.

Tatizo/Mrejesho: Inafariji kuona kuwa vyombo vyetu (kama ni kweli) vinatumia wataalamu tulio nao katika kutafuta ukweli wa mambo yenye maswali magumu ya yasiyoweza kutatuliwa bila Ushahidi wa kisayansi. Hili ni jambo jema sana.

Methodolojia:

Kilichoandikwa:
Wachambuzi wameanza kazi yao kwa kutoa utangulizi unaoonesha uhasi au ubaya wa mitandao ya kijamii (walikuwa so negative mapema kabisa). Utangulizi wao unaonesha uchambuzi umefanywa kwa fikra kwamba intaneti na mitandao ya kijamii ni eneo hatari na kunahitaji jeshi la kukabiliana nayo. Tumbuke malengo ya uchambuzi huu hayakuwa ‘Matumizi ya mitandao ya kijamii’ bali ni ‘Uhalisia wa video inayodaiwa kuwa ya Askofu Gwajima’.

Tatizo/Mrejesho: Haya ni makosa makubwa sana kitafiti. Moja, huwezi kuanza utafiti ukiwa tayari una majibu ambayo yameegemea upande mmoja unaoutaka. Pili, katika uwasilishaji wa kazi ya kisayansi huwezi kutoa utangulizi wa jambo ambalo siyo lengo la kazi ya utafiti uliyofanya. Video hii bado ingeweza kupatikana bila mitandao ya kijamii na mitandao ya kijamii siyo teknolojia ya kutengeneza video feki bali ni njia ya mawasiliano/usambazaji. Mchambuzi angejikita katika kuueleza umma juu ya sayansi ya kutengeneza video feki.

Njia:

Kilichoandikwa:
Wachambuzi wameanza kazi yao bila kutuambia waliongozwa na nini katika uchambuzi ili kumsaidia msomaji aweze kufuatilia kinachofuata.

Tatizo/Mrejesho: Uchambuzi wa kisayansi lazima kuwe na vitu vinavyokuongoza.
  • Moja ni lazima kuwepo na swali au lengo. Kwenye uchambuzi huu lengo liko wazi.
  • Pili lazima ujikite kwenye mambo mahsusi yanayolengwa na uchambuzi maana huwezi kutafiti kila kitu.
  • Tatu, lazima uoneshe nini kinatumika kama kipimo (metrics) kurejea na kusema majibu uchambuzi yakoje.
  • Nne, lazima useme kwanini kipimo hicho ndio sahihi kwa uchambuzi huo na sio vinginevyo. Kwa mfano, kwenye uchambuzi huu, wataalamu wangetakiwa waseme kitalaamu nini kinathibitisha kwamba video au picha ni feki au halisi na kwanini. Pia watuambie njia za kuthibitisha ni zipi, za aina ngapi, na kwanini wao wamechagua vipimo waliyotumia.
Vipimo

Kilichoandikwa:
Hata hivyo kunaonekana vigezo vitatu walivyotumia kama vigezo vya uchambuzi wao, navyo ni:
  • Mtizamo wa mchambuzi kwa watu wanaonekana kwenye video (content);
  • Sauti zinazoikika (sound), na
  • Picha mnato walizochukua kwenye video.
View attachment 1107663

Uchambuzi:
  • Kigezo cha kwanza cha mtizamo ni very subjective maana kinategemea maoni na fikra zinazomwongoza mchambuzi.
  • Tatizo: Mwanzoni tumeshaona mchambuzi ana fikra gani katika kazi yake hivyo tayari alishatuonesha atatoa hitimisho gani kwenye kinachoonekana kwenye video.
  • Kigezo cha pili cha sauti (sound). Mchambuzi katumia mawimbi/masafa (frequencies) ya sauti zinazosikika kwenye video kama kigezo cha kupima iwapo video imetengenezwa au ni halisi.
  • Tatizo: Mchambuzi anatoa hitimisho kwamba katika muda tofautitofauti wa tukio kulikuwa na sauti zinazotofautiana ukumbwa wa mawimbi. Sijajua mchambuzi katumia sayansi gani lakini hakuna mtu anayetoa sauti yenye masafa yanayofanana muda wote. Mawimbi ya sauti yanachoonesha nguvu iliyotumika kutoa sauti husika. Hivyo nikiongea taratibu mawimbi yatakuwa madogo na nikiongea kwa sauti kubwa mawimbi yatakuwa makubwa pia. Nikiongea kwa kupunguza na kuongea sauti mawimbi nayo yataonesha kupanda na kushuka. Sasa ni kwa namna gani mchambuzi anataka kutuminisha kuwa sauti za wahusika zilitakiwa ziwe na mawimbi yanayofanana muda wote? Kwani walikuwa wanaimba kwaya inayoratibiwa utoaji wa sauti? Pili, mchambuzi anatumbia kwamba pitch au ukali wa sauti unaotolewa haufanani na ukali wa sauti ya Gwajima. Hata hivyo hajatuambia sauti ya Gwajima ina pitch ya aina gani na kwanini Gwajima awe na pitch inayofanana muda wote anapotoa sauti.
  • Kigezo cha tatu (picha mnato): Mchambuzi kachukua picha mnato za video na kujaribu kuzichambua akitumia uzito wa muonekano wa rangi(colour intensity) na tofauti ya rangi hizi katika objects zinazochunguzwa.
  • Tatizo: Mchambuzi hajatuambia kwanini kutumia picha mnato wa video ni njia sahihi ya kupima iwapo video sio halisi. Pili, hajatuambia kwamba sayansi, ushahidi wa kitafiti na matakwa ya kifaa alichotumia kufanya uchambuzi vinasema kwamba kwenye picha moja yenye objects tofautitofauti, ni lazima colour intensity ifanane kwa kila object. Tatu, hata kama ni hivyo sayansi haikubaliani na hitimisho hilo kwani uzito wa muonekano wa rangi kwenye images unategemea vitu vingi. Mojawano ni ukweli kwamba kila object iliyoko kwenye picha ina rangi yake, texture, na muonekano wake tofauti na vingine. Mwanaume aliye juu ya mwanamke ana ngozi tofauti kimuonekano na texture yake pia. Hivyo hawawezi kufanya reflection au kuakisi rangi zinazopafana kwenye mionzi inayotumwa na kamera iliyokuwa inachukua video. Nne, sio kweli kwamba tofauti ya rangi inaonekana kwenye wata pekee. Ukitazama images mchambuzi alizozitumia, utaona uzito wa rangi zinazotoka kwa manamke ni tofauti na za mwanaume na ni tofauti na za mazingira (ukuta/mapazia). Pia katika object moja kuna rangi tofautitofauti kutokana na ukweli kwamba hizo sio flat objects. Miili ina mikunjo. Hata ukitazama picha ya tano na ya nne kwa object/mtu huyohuyo, bado utaona zinatofautiana uzito wa rangi kwenye eneo hilohilo maana mchambuzi kazichukua wakiwa kwenye movements za tendo walilokuwa wanafanya hivyo ni wazi kinachokua reflected kwenye camera kitatofautiana pia.
Uwasilishaji wa uchambuzi

Taarifa/ripoti ya uchambuzi huu wa kisayansi umejieleza kwamba umetolewa na Kitengo cha Uchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Kinachoshangaza kidogo hakuna jina la mtu au watu waliofanya utafiti!

View attachment 1107665

Tatizo: Katika kazi za kisayansi, hakuna utafiti au kazi kitafiti inayofanywa na taasisi. Hufanywa na watafiti ndani ya taasisi. Uwajibikaji wa kazi ya kisayansi hauendi kwa taasisi bali kwa mtafiti aliyefanya kazi husika. Kwa mfano, iwapo kuna swali la kisayansi kuhusu kazi hii, watu hawawezi kumuuliza mkuu wa chuo wala kila mwalimu kwenye kitengo husika. Anatakiwa kuulizwa aliyefanya utafiti na kutoa ripoti hata kama inawakilisha taasisi. Kitendo cha watafiti kutoa ripoti na kuficha utambulisho wao, tayari kinaleta maswali kitafiti. Pia kinaleta maswali juu ya umakini wa taasisi iliyokubali aina hii ya uwasilishaji wa kazi ya kisayansi.

Hitishimo la Mrejesho:
  • Uchambuzi huu umefanywa na mchambuzi au wachambuzi ambao tayari walikuwa wana majibu ya wanachotaka kuwaeleza waliowapa kazi au wasomaji wao. Mtizamo wao ni hasi kuanzia mwanzo. Badala ya kujielekeza katika sayansi ya uchambuzi wa picha (image processing and analysis) wao wamejielekeza kwenye siasa na vita dhidi ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
  • Pili, uchambuzi huo hauko wazi ulikuwa unatazama vitu gani mahususi vinavyokubalika na kuthibitika katika sayansi husika kupima uhalisia wa video. Badala ya uchambuzi wa video na teknolojia husika, wamechambua picha waliyopiga kwenye video. Mchambuzi katumia kifaa cha kuchambua picha mnato kuthibitisha uhalisia wa video (picha mjongeo)
  • Tatu, mchambuzi hajatoa vigezo au vipimo (metrics) vinavyotumika kisayansi kuthibitisha uhalisia wa video.
  • Nne, hitimisho la mchambuzi kuhusu matokeo ya uchambuzi wake vimeegemea upande aliotaka na amejiepusha na kujikita kwenye ukweli wa kisayansi unaonekana kwenye uchambuzi aliyofanya yeye mwenyewe. Mchambuzi anatoa mahitimisho yasiyopata support/ushahidi wa anachochambua.
Mwisho:

Katika historia ya ulimwenngu na maendeleo yake, wanataaluma na hasa wanazuoni walio katika Vyuo Vikuu wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye maendeleo hasa ya ukuaji wa sayansi na teknolojia. Hawa ndio wanatakiwa kuwa mboni ya jicho na kimbilio kwa Taifa hasa katika mambo yanayohitaji utaalamu, ushahidi na ushauri unaotolewa katika misingi ya ukweli na kuthibitika kisayansi/kitafiti.

Ni vema wanazuoni wakakumbuka wajibu wao kila mara wanapofanya kazi zao ili kuendelea kuipa jamii imani kwamba kazi zao zinalindwa na misingi ya taalamu na utafiti na sio vinginevyo. Wanataaluma wanatakiwa kuwa wakweli muda wote. Hata inapotokea wamepewa au wanatakiwa kufanya utafiti lakini hawana uwezo na uatalamu husika, wanategemewa kuwa wazi kusema hivyo bila uoga na sio vinginevyo. Hii inaeleweka na kukubalika kabisa hasa kwa taaluma ngumu kama ya sayansi za kompyuta. Pia ni vema wakumbuke, kazi za kitafiti zinawajibika kwa kila mtafiti na sio amri ya kumi na moja kwamba wanachosema ndio hitimisho.

Kuna msemo uliozoeleka kwamba “kazi ya kitafiti inapimwa na utafiti mbadala”. Pamoja na kauli hii kuwa na sehemu ya ukweli, lakini haina ukweli wote. Ukweli wote ni kwamba kazi ya utafiti inaweza kupimwa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na maana na lengo la utafiti wenyewe; njia au methodolojia iliyotumika na inavyoshabihiana na lengo la utafiti; matokeo ya utafiti inayoonesha nini; na nini tafsiri ya mtafiti katika matokeo ya utafiti wake. Habari ya kufanya utafiti mbadala kama kigezo cha kutofautiana na anachosema mtafiti, ni hatua ya mbali sana na ni iwapo tu, vigezo nilivyotangulia kuvitoa havioneshi iwapo kuna shida katika kilichowasilishwa.

Angalizo: Mrejesho huu umetolewa kwa mtizamo kwamba ripoti husika imetoka Chuo Kikuu cha Dodoma hivyo unastahili mrejesho wa kitaluma. Hata hivyo sijaweza kuthibitisha chanzo hasa cha ripoti hii; iwapo haijatoka UDOM basi uchaumbuzi wangu unamjibu yeyote aliyehusika kuandaa ripoti hii na kuamua kujificha nyuma ya jina la chuo cha UDOM.

Naitwa Ngosha Mchambuzi (Niandikie kupitia ngoshamchambuzi@gmail.com)
Mkuu nakutumia document yangu kwenye email yako

Kwa upande wangu binafsi nilijaribu kufanya analysis zangu na kufanya documentation

By profession nina utaalam wa kutosha kwenye mambo ya DIGITAL FORENSICS INVESTIGATION

Nimetumia tools ambazo zinatambulika na kusajiliwa na mahakama (sijataja mahakama za nchi gani kwa sababu maaalum) kwenye kufanyia video forensics

Nimefanyia rejea kupitia tools za nchi kama india, japana

Note: india kwenye swala zima la digital forensics wapo vizuri mno kidunia na tools zao zinatumika kwenye nchi nyingi sana za dunia ya tatu(africa) na kwingineko,

Nakutumia utafiti wangu, naamini maswali yote uliojiuliza hapo utapata majibu yake kupitia document yangu

Uwe na usiku ulio mwema
 
Weka hapa na sisi tusome mkuu!
 
hawa udom kwanza nani kawatuma kufanya hii kazi? ni course work ya darasani? ni Research paper ya mwanafunzi/chuo. hii report imetumia shs ngapi za wapiga kura? Kodi tunalipa kwa mbinde halafu unaona inachezewa tu, jamani inauma mtuhurumie walipa kodi.
 
Uchambuzi mzuri mleta mada.

Kwa kusoma tu utangulizi wa ile ripoti, lugha iliyotumika ikiendana na makosa dhahiri ya grammar vinatosha kumfanya mtu aliyesoma maandiko ya kisomi ya kweli kuidismiss from the outset. Inasomeka kama kazi ya mwanafunzi.

Granted it's probably not the kind of work a self respecting academic worth his salt would take on, it is still a bad look on the university.
 
Hahaha Ngosha Mchambuzi, umejiunga leo ili ulete report ya uchambuzi uchwara? Hongera nawe kwa kazi yako, labda wahusika watauona uzi huu na kukujibu.
 
Watanzania hivyo wanavyoamini kuhusu huyu mtu na ile video ndio hivyo hivyo. Hata msemeje
 
Mkuu nakutumia document yangu kwenye email yako

Kwa upande wangu binafsi nilijaribu kufanya analysis zangu na kufanya documentation

By profession nina utaalam wa kutosha kwenye mambo ya DIGITAL FORENSICS INVESTIGATION

Nimetumia tools ambazo zinatambulika na kusajiliwa na mahakama (sijataja mahakama za nchi gani kwa sababu maaalum) kwenye kufanyia video forensics

Nimefanyia rejea kupitia tools za nchi kama india, japana

Note: india kwenye swala zima la digital forensics wapo vizuri mno kidunia na tools zao zinatumika kwenye nchi nyingi sana za dunia ya tatu(africa) na kwingineko,

Nakutumia utafiti wangu, naamini maswali yote uliojiuliza hapo utapata majibu yake kupitia document yangu

Uwe na usiku ulio mwema
Tuma mkuu naisubiri
 
Yaani km ndio uchambuzi wa hivi.... Ndio chuo kikuu cha DODOMA.

basi kazi ipo aisee....

Mtiririko wa ripoti.. Mpangilio hadi uwasilishaji ni mbovu kuwahi kutokea aisee.
 
Una hoja ingawa sijaielewa. Utafiti na ripoti ya utafiti ni vitu viwili tofauti. Nimeiona ripoti ya UDOM. Kwahiyo, ulivyoiona na kwa uchambuzi wako huu, unataka kutuaminisha kuwa video ya Gwajiboy ni yenyewe? Vitu vingine visitumalizie muda.
 
Back
Top Bottom