Tetesi: Ubalozi wa Tanzania Uturuki unashirikiana na jeshi la polisi la Uturuki kuwadeport Watanzania

kijanamtanashati

JF-Expert Member
Aug 22, 2014
516
890
Balozi kazi yake ni kutetea raia zake lakni ubalozi wetu wa Tanzania uliopo Uturuki haufanyi kazi hii badala yake umekuwa ukishirikiana na jeshi la polisi la Uturuki kuwaondosha watanzania nchini umo na kuwarudisha Tanzania.

Mchezo upo hivi Mtanzania akikamatwa na polisi kama hana makaratasi anapelekwa kituoni akifika kituoni polisi wanapiga simu ubalozini wanaongea nao kituruki sijui wanaongeaga nini baadae wanakupa sim unaongea na ubarozi.

Ukiongea na ubalozi unakuchombeza unakufariji mtu unafarijika unazani ukimaliza kuongea na ubalozi polisi watakutoa kumbe ndo imekula kwako hiyo kesho unatumiwa passport unarudishwa Tanzania utake usitake.

Ubalozi aukutetei ndo kwanza wanashirikiana na polisi. Vijana wengi wanaoishi Uturuki ambao awana makaratasi awatoki nje wanaogopa kukamatwa na polisi.

Ukikamatwa ujue ndiyo safari ya Tanzania imewadia na ubarozi aukutetei. Kama ubalozi unashindwa kutetea raia zake kazi ya ubarozi inakua nini?
 
Mkuu hapo ubalozi hawana mamlaka. Cha kukusaidia ni hiyo kurudishwa salama bila kupelekwa mahakamani kwa uzamiaji.

Huku Tanzania wasomali kila siku wapo mahakamani.

Cha kufanya fanya juu chini usikamatwe na ukidakwa ujue pa kutokea.

Kwanza kataa wewe sio mtanzania

Pia la kujiuliza. Unasema unatumiwa passport? Inatoka wapi?
 
Umezamia nchi za watu Kiharamu.

Ubalozi unaongea na wewe kwa kukubembeleza huku wanakusikilizisha nyimbo za Ali Kiba, unakupokea, unakupatia documents ili urudishwe nyumbani kwenu na wala huko nyumbani ukifika haufunguliwi kesi ya kutoroka nchini kinyume na sheria

Unataka ubalozi ukufanyie kipi hata uone umekutetea?

Kitendo cha mamlaka za Turkey kupiga simu ubalozini na kuwataarifu kuhusiana na wewe, hilo pekee unapaswa kuupongeza ubalozi.
 
Nimesoma maelezo ya mtoa mada nimeogopa kumsema ana akili kama za lastborn😃

mkuu ukienda nchi yoyote yafaa uwe n nyaraka zote muhimu mfano passport na visa kama nchi uloingia unaingia kwa visa na kama unafanya kazi tafaa uwe na nyaraka za kaz za nchi husika. Ukikamatwa ilihal nyaraka zote zimetimia na huna kosa la jinai ubalozi yafaa ukutetee na wakishindwa kufanya hivyo tunakila sababu ya kumlaumu balozi aloteuliwa .

Tusiwe watu wa lawama sana mpaka vitu viko wazi namna hii. Tushakuwa watu wazima wakuu zangu
 
Back
Top Bottom