Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Ripoti ya Twaweza iliyozinduliwa leo tarehe 15.09.2016 inayotoa Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya Tano imekuja na matokeo kuwa 61% ya wananchi wanasema hawapati taarifa kuhusu masuala ya siasa nchini, huku idadi ndogo (4%) wakisema wanapata taarifa za kutosha. 35% wamesema wana taarifa kidogo kuhusu masuala hayo.
Miongoni mwa wale ambao wanasema wanapata taarifa za kutosha ama wana taarifa kwa kiasi fulani, 61% wanapata taarifa kuhusu masuala ya kisiasa kutoka kwenye radio, 15% wanapata taarifa kwa kusikia kwa watu na 14% kupitia kwenye luninga. 1% pekee wametaja mitandao ya kijamii.
Unadhani idadi hii ya wananchi wanafanya maamuzi sahihi iwapo hawapati taarifa za masuala ya kisiasa? Toa maoni yako.