TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

Maadui wa Demokrasia hadi leo wanajitetea

Kilimo cha kulima kura. Hivi uko nanenane mnafanya nini?
Hata Saba Saba walikuwepo, nikajiuliza 40 Dar es salaam International Trade Fair ni Kiingereza kigumu kwangu kuelewa au TV inanidanganya? Baadaye nikaja kuelewa, wafanyabiashara wote wanaoingiza Faida kuanzia 12b walipaswa kushiriki.
 
Kama hakutakuwa na tume huru ya uchaguzi ifikapo 2020, mimi nitapiga kampeni chama changu kisishiriki uchaguzi, pia nitapiga kampeni umma usishiriki uchaguzi...

Hiki kijiwe cha ccm kiitwacho tume ya uchaguzi kiishie hukohuko Lumumba
Mkuu, nitapata wapi kitabu chako kinachohusu Ujasusi? Nisamehe kwa kutoka nje ya mada...
 
Tume ya Uchaguzi kwenye shughuri za nane nane!!!!!

Anyway tunaomba pia ufuatilie kile kikao cha akina KAOGE zaidi ya 100 pale kinondoni wakimjadili Makonda (He said hivyo), vipi amechukua hatua?!!!!!
 
Wanabodi,

Hii ni TV Program Alert, ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi, inashiriki katika maonyesho ya kilimo ya Nane Nane katika uwanja wa Mwl. J.K Nyerere mjini Morogoro.

Ushiriki huo wa Tume ya Uchaguzi kwenye Maonyesho, ni fursa nzuri kwa wale wote wenye madukuduku kuhusu Tume kama ni tume huru, na uchaguzi, kama ulikuwa huru na wa haki.

Kwa vile sii wote wataweza kutembelea banda hilo huko Morogoro, kwa faida ya wengi, nimetembelea banda hilo, na nitarusha vipindi maalum vya banda hilo ndani ya Nane Nane na PPR.

Leo Waziri Mkuu ametembelea banda la Tume, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, Makamisha Mary Longway na Athina Omari, pamoja na msimamizi mbobezi, Spora Liana, watazungumzia uchaguzi uliopita.

Usikose kuangalia mfululizo wa vipindi vya Tume ya Uchaguzi kwenye Maonyesho ya Nane Nane, kipindi cha kwanza kinaanza leo saa 1:00-1:30 Star TV.

Kesho ni Channel Ten, keshokutwa ITV kisha TBC.

Karibuni msikie na kushuhudia jinsi ambavyo huwezi kudanganya matokeo ya uchaguzi!, msidanganywe na viongozi wa vyama kuhusu bao la mkono!, hakuna kitu kama hicho!.

Paskali
Hivi kwa nini Rais Magufuli hafuti hizi sherehe za 88 na 77 kama alivyofanya kwenye sherehe za Uhuru? Maana zinatafuna hela za huduma za jamii tu
 
Hongera kwa majibu yakufikirika na kusadidika!
echa alipofuta yale matokeo kinyume cha sheria, hakuna yeyote aliyepinga kitendo kile zaidi ya kupiga kelele tuu! .
Sio kwelikuwa hakuna yeyote aliepinga ila Sheria na Katiba kandamizi ndio iliowafunga watu kupinga kisheria. Maamuzi ya Tume ni ya mwisho na hayapingwi na chombo chochote kile!
Kitendo alichokifanya Jecha ni kitendo haramu, na batili, lakini haramu hiyo na batili hiyo kwa vile haikupingwa na yeyote, then huku tuu kutokupinga kumeihalalisha batili ile kuwa halali na zao la haramu ile ni uchaguzi halali!
Haramu ikithibitika haigeuziki kuwa halali hata siku moja. Shaba huwezi kuigeuza kuwa dhahabu hata ukin'garisha vipi!
Hivyo ndivyo uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ulivyokuwa. Jecha ni mbakaji wa Demokrasia, kitendo alichokifanya ni ubakwaji wa demokrasia mchana kweupe. Waliobakwa walipiga tuu kelele tunabakwa! tunabakwa!, lakini hawakuchukua hatua yoyote dhidi ya mbakaji wala ubakwaji ule.
Ulitaka watu watoke barabarani na kumshughulikia mbakaji na kuchukua hatua mikononi? Wabakaji waliokuwa wanaranda na vifaru, Bazooka mgongoni na doria za magari ya kuwasha, huku Mazombie wakiwanyamazisha watu kwa nondo za kichwa?Pascal unawapenda kweli wazanzibari au nawe ni mmoja wao?
Kumbe yule mwanamke alifurahia ubakaji ule na kwa ridhaa yake mwenyewe akaamua kuendelea kuishi na mbakaji yule na wakaowana kwa ndoa kabla mtoto hajazaliwa, hivyo mtoto alipozaliwa ni mtoto halali kwenye zao la ndoa halali japo ujauzito ulitungwa kwa zinaa ya ubakaji!
Pascal usipoteshe umma:-
1.hakuna ridhaa ya ubakaji. Tafsiri ya ubakaji ni tendo la kutumia nguvu katika ngono ambapo mbakaji anatumia nguvu kuonyesha ubabe wake(vifaru,bazooka,washawasha).
Inawezekana hata ndani ya ndoa kukatokea ubakaji.
2.Sijui kwa sheria zipi? za kishetani au za kiimani,lakini kwa mujibu wa mila za kizanzibari mtoto akitungwa nje ya ndoa na kuzaliwa ndani ya ndoa, mtoto huyo ataendelea kuitwa mwana haramu na hawezi hata kumrithi baba yake akifariki.

Pascal na Pasco ni majina yanayo fanana na inaonekana hata hulka na mitazamo yao inalingana. Haramu kuhalalisha kuwa halali ina chemka ndani ya mishipa ya damu yao.
 
Uchaguzi uliopita watu wa tume walibadili matokeo kidigital, kinachotumwa kinabadilishwa hewani na center nyingine ndio maana ata leo ukiwaambia turudie kuhesabu kwa kutumia form za vituoni, tume haitaki kabisa kusikia, pili katiba yetu mbovu, eti matokeo ya Rais hayapingwi mahakaman, that means tume ata ikimtangaza Rungwe ndio mshindi hakuna wa kupinga, poor this country
Ni kwanini kina Lowassa hawaweki hadharani hizo fomu za vituoni ili watu waone?
 
Usikose kuangalia mfululizo wa vipindi vya Tume ya Uchaguzi kwenye Maonyesho ya Nane Nane, kipindi cha kwanza kinaanza leo saa 1:00-1:30 Star TV.

Kesho ni Channel Ten, keshokutwa ITV kisha TBC.

Karibuni msikie na kushuhudia jinsi ambavyo huwezi kudanganya matokeo ya uchaguzi!, msidanganywe na viongozi wa vyama kuhusu bao la mkono!, hakuna kitu kama hicho!.

Paskali


Hivi wale vijana wa CDM wa IT wameshaachiwa? Msisahau kuwa onyeshaa kwenye Maonyesho iliwawasaidie kufanya Ufafanuzi wananchi waelewi vizuri.
 
Yaani kwa akili za kawaida tu, mtu aliyekuwa akituhumiwa kwa ufisadi kwa miaka zaidi ya saba, angekuja kuwa rais?. Tena akiwa na wale wale ambao walimuita fisadi kwa nguvu zao zote?, kwa akili zao zote? kwa maarifa yao yote?.

Kama angeweza kuwa rais basi nchi hii ingekuwa imeingia kwenye kumbukumbu ya kuwa taifa la walarushwa kuliko mataifa yote duniani. Nigeria na sifa yake ya kuwa ni nchi ambayo wagombea na wapiga kura wote huwa na lugha ya kuhongana, ingekuwa ni nchi ambayo hatujaifikia kwa uchafu wa rushwa. Ingekuwa aibu ya karne.
 
Sawa kabisa mkuu, unisamehe maana naona umeiva kwelikweli. Sababu haswa ya kuhoji kama ni huyu mayalla ninayemfahamu ndiye kaandika vitu kama hivi, nikaona zipo sababu nyingine binafsi, kumbe wakati ule wa Kiti Moto ulikuwa mdogo na sasa kwa kuipigia CCM debe umekuwa mkubwa. Hapa mada iko wapi, kwamba tume ya uchaguzi iko kwenye maonyesho ya Nanenane?
Mkuu Karumekenge naona inafanana kabisa na mwenye jina lake! , unauliza hiki, unajibiwa, ndipo unauliza kingine! . Subject matter inajieleza na inajitosheleza labda issue iwe ni kwenye kiwango cha uelewa. Karumekenge nenda shule, sio mpaka baba amuite mchinja mbuzi, ayanywe maji, yauzime moto, uichome fimbo imchape Karumekenge ndio aende shule! .

Paskali
 
Kubalance story ungewatafuta na wanaosema waiibiwa kura ili kujua waliibiwa vipi
MKuu Jambo Jema, he who allege must prove, yaani the burden of proof lies with the one who allege!, yaani ni jambo jema anae lalamika kuibiwa akaleta zile fomu za mawakala wake zenye hesabu zake za ushindi ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Tume haikutenda haki bali imepika matokeo.

Mkitembelea Banda La Tume ya Taifa ya Uchaguzi, mtathibitishiwa hakuna namna yoyote ya wizi wa kura kwa sababu hadi matokeo ya kura za urais yamebandikwa vituoni! . Hesabu za huyo mshindi aliyeibiwa ziko wapi to prove wizi wa Tume ? .

Tumeelezwa zile copy za matokeo zilizosainiwa na mawakala wa vyama vya siasa ndizo zimekuwa scanned na kutumwa kwenye tallying.

Chadema wanazo copy zao za matokeo yote toka kila kituo, kama nakala zao ni tofauti na kilichotangszwa na NEC, that is a very strong case to start with kuutangazia ulimwengu NEC walipika matokeo na wananchi watawaelewa.

Kura milioni 6 sii mchezo! , ndizo zilizomuingiza JK Ikulu ile 2010 naomba tuziheshimu kwa kuukubali ukweli, msiwaaminishe watu ushindi wa uwongo ili kujenga chuki kwa mshindi halali! . Asiyekubali kushindwa sii mshindani! .

Paskali
 
Paskali kuna mtu ameendelea kukulalamikia kuhusu uchaguzi? Una uhakika gani kwamba hayo wanayoonesha hapo 8-8 ndo yanayohalalisha uchaguzi kuwa huru? Huyo mwenyekiti wako wa tume yenu alipopelekewa malalamiko na mgombea wa UKAWA alijifungia chooni masaa karibia ma-3 ili tu asionane na mgombea wa UKAWA!! Eti akasema alikuwa anatangaza tu bila kujua anayemtumia ni nani? Pambafffff kabisa kale kazee!
Mkuu Job K. heshima ni kitu cha bure! . Hakuna aliyelalamikia uchaguzi uliopita ila kuna watu wanadanganywa fulani ndio alishinda akapokonywa ushindi, akatangazwa aliyeshindwa baada ya matokeo kuchakachuliwa.

Uwme ya Taifa ya Uchaguzi imekuja kwa wananchi kuwaonyesha ukweli halisi wa uchaguzi Mkuu uliopita kuwa ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki! .

Paskali
 
Paskali kwa nini Jamii Forum iliondolewa hewani wakati wa uchaguzi? Ukinijibu kwa ufasaha huenda nikayaamini hayo maonyesho yako ya kilimo cha kura huko nane8
Mkuu Safari_ni_Safari, sikuwahi kujua kuwa jf iliondolewa hewani!. Nirawasiliana na Mkuu Max kuhusu hili!. Kama jf inaweza kuondolewa hewani, then kuna siku jf itafungwa kabisa! .

Paskali
 
Mkuu Job K. heshima ni kitu cha bure! . Hakuna aliyelalamikia uchaguzi uliopita ila kuna watu wanadanganywa fulani ndio alishinda akapokonywa ushindi, akatangazwa aliyeshindwa baada ya matokeo kuchakachuliwa.

Uwme ya Taifa ya Uchaguzi imekuja kwa wananchi kuwaonyesha ukweli halisi wa uchaguzi Mkuu uliopita kuwa ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki! .

Paskali
Mkuu Paskali, kwani kuna mtu nimemvunia heshima hapo? Hako kazee si ndo kaliendaga kujifungia chooni mpaka mgombea wa UKAWA akakata tamaa ya kukasubiri ili akape barua ya malalamiko yake? Kalibanwa na BBC kakaropoka kwamba kenyewe kanatangaza jinsi kanavyoyapokea bila kujiridhisha kwamba yanayokuja yanatoka kwenye vituo vya uchaguzi kweli au yanatoka Mlimani City?
 
Back
Top Bottom