Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Habari Mheshimiwa!

kabla ya yote ningependa kukushukuru kwa muitikio wako na kujali maoni mbalimbali.

Swali langu , katika watu wenye makundi maalum kuna hawa waliopo kweny utumishi wa umma .. Je , serikali inawawezesha vipi ili kukabiliana na mazingira ya kazi .

Kuna ticha mmoja namuona anapambana sana anaitwa Yusuph Hamisi , bahati mbaya alipoteza mguu wake ila bado anapiga kazi haswa na ile morali ya juu , anapendwa sana yupo na mwenzio naye sio mlemavu anaitwa Yusuph Pangoma.

Nimeandika hii kwa sababu baadhi ya taasisi zinatoa posho kwa walemavu wote kama motivations ..Sasa sijajua kwa level za Tamisemi inakuwaje!? .Maana hata walemavu pamoja na hali zao bado wanaweza kuajiriwa kama wana vigezo

CC Dkt. Gwajima D
 
Hongera sana Dkt Gwajima.

Ila wale wasiasa chafu wasuje kukwambia unashinda mitandaoni😅. Tunafurahi kutumia jukwaa hili.

Zaidi nakupongeza umekuwa ukitumia social media kwa ufasaha kuweka mambo sawa kwa baadhi ya matukio. Huo ndiyo uongozi wa kisasa, sio habari za desk top review. Sizipokuja huna jambo.
 
Niombee ndugu yangu 😚
 
Ndugu yangu salaam. Awali ya yote pole Sana kwa kadhia hii. Pia hongera Sana kwa hekima, utulivu na ujasiri wa kuleta hoja yako hii. Haya kesho nitumie ujumbe kwenye sms namba 0765345777 nitaweza kuisoma na kukupa ushauri. Haya usiku mwema. Shukrani

Sent from my CPH2207
Heshima yako mheshimiwa waziri na Pole kwa majukumu,ulinipa namba ili nikutumie msg inayoelezea changamoto niliyonayo ya mgogoro wa kifamilia na changamoto niliyopata baada ya kulifikisha jambo hili ustawi wa jamii na mahakama inayohusika na masuala ya watoto,nimejaribu kutuma msg hiyo siku ya nne leo kwa namba uliyonipa lakini namba haikubali kupokea msg,
 
Dada mheshimiwa , ukifanya hili la kupigia chapuo la uraia pacha diaspora watapata nafasi , nakuleta chachu kwenye maendeleo ya Tz kwa ujumla wake,kwenye kila nyanja.
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
mheshimiwa,mimi ninanyanyaswa sana,nilibebeshwa mimba na afisa mtendaji wa kata baada tu ya kumaliza form four,baada tu ya kubeba mimba mwenzang akabadirika mimi sikuhitaj anioe maan sikumuona kama anafuture yoyote,nilihitaji tu nipate matunzo lakini sikupata mpaka nikajifungua mtoto wa kiume na sasa anamiaka mitatu na nusu sipati msaada wowote toka kwa mzazi mwenzangu nahangaika kumlea pekeang mtoto nimefika mpaka ustaw nipate walau hata hel ya sabuni lakin nilioshia kupewa namba za simu ili nikipata shida niwapigie.naomba nisaidie mwanangu apate haki.Natumaini utanisaidia
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Ahsante sana kwa nafasi hii
Ninauliza Wizara ina mikakati gani madhubuti ya kutibu tatizo la single mothers na Single Fathers maana tunakoelekea inakuwa kama utamaduni
 
Heshima yako mheshimiwa waziri na Pole kwa majukumu,ulinipa namba ili nikutumie msg inayoelezea changamoto niliyonayo ya mgogoro wa kifamilia na changamoto niliyopata baada ya kulifikisha jambo hili ustawi wa jamii na mahakama inayohusika na masuala ya watoto,nimejaribu kutuma msg hiyo siku ya nne leo kwa namba uliyonipa lakini namba haikubali kupokea msg,
Mbona nimejibu sms zote kwenye namba zote 2? Angalia kama sijajibu maana siyo rahisi kutambua kuwa hii ndiyo yako maana najibu hoja tu.
 
Mbona nimejibu sms zote kwenye namba zote 2? Angalia kama sijajibu maana siyo rahisi kutambua kuwa hii ndiyo yako maana najibu hoja tu.
Hongera kwa ishu ya DED wa Mafia...

Uwajibikaji wako ni wa kupigiwa mfano kwenye kupinga haya mambo ya kuonekana ubakaji ni jambo la kawaida tu.
 
Wanajamvi habari za kazi!!

Naomba tusaidiane kuitambua hii video ilipoatokea,maana inazagaa kwenye magroup ya whatsupp,ila hatujui imetokea wapi.

Ahsanteni!!
 
Mh. Waziri karibu sana humu jf, niende moja kwa moja kwenye point yangu.
Wizara ya kilimo imepambania sana maafisa kilimo walioko katani kuwezeshwa usafiri wa pkpk na tunaona kwa sasa mambo yanaenda, vp wizara yako inashindwaje kuwapambania maafisa maendeleo ya jamii wa ngaz ya kata japo wakapatiwa pkpk? Maafisa hawa wapo wachache lakini serikali haijawawezesha na kuwatumia ipasavyo, wengi tunawaona wanatumika kwenye marejesho ya mikopo ya 10% tu wakati kaz zao ni mtambuka katika jamii.
NAPENDEKEZA
1. Pambania bajeti ya wizara yako iongezeke
2. Agiza idara ktk halmashauri nchini kuwatumia wataalamu hawa kwenye kuhamasisha jamii mambo mbali mbali.
3. Wataalamu hawa wachache katani watumike maeneo mengine yenye majanga kama mafuriko na imani potofu kutokana na mila na desturi kwa kupelekwa na serikali maeneo yenye changamoto hata kwa wk 1 tu, utaona changes
4. Waangalie maafisa maendeleo kwenye stahiki zao.
Kwa leo niishie hapo, watumishi hao ukiwaona wanatia huruma tumechoka kuwapa au kuwaazima boda zetu. Nawasilisha kwako Mh. Wazir, over
 
Ahsante Sana. Mwaka jana tulinunua na Mwaka huu tutanunua. Kuna mpango wa bottom up unaohusisha kuimarisha wataalamu wa wizara zote za kisekta kwenye kila kata.

Ahsante kwa maoni mazuri 🤝
 
Kuna maswali machache huwa najiuliza pasipo kupata majibu

Kwamfano.

Kunafaida gani kumfunga mume au baba wa watoto aliye shindwa kutimiza mashart/mkataba alio wekewa na afisa ustawi wa jamii?

Huenda Labda anashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kipato kidogo alicho nacho au mazingira magumu kikazi anayo yapitia

hatimaye anashindwa kutimiza masharti Kisha anafikishwa mahakamani na kufungwa Sasa ninge penda kujua kwamba je! huwa mnajilidhisha vipi Kama ameshindwa kwa makusudi mpaka mna mfunga kwa kosa la kushindwa?

Kingine ninacho jiuliza nikwamba

je! kumfunga huyo baba kuna wa saidia Nini watoto watakao Baki na mama yao au watoto na mama huku nje ya jera?

Kwa jinsi ninavyo fahamu Mimi hakuna baba anaye weza kuishi kwa amani wakati huku nyuma watoto wake wanatembea uchi,Wana lala njaa, nk haiwezekani Labda Kama amepaka ziwa anaweza kuya tenda hayo

Sasa je!

Kuna hasara gani huyo baba akiachwa huru lakini aka ambiwa kwamba ajitahidi kufikisha mahitaji kadri mungu atakavyo mjaria

je! hili halita kuwa Bora kuliko lile la kumfunga??

Kuna Jambo lingine siku hizi limekuwa Kama biashara kwa wake zetu/wanawake

Kwamba ana kuchunguza kuhusu kazi na kipato chako akishajua aka jiridhisha kwamba kunafaida ataingiza kutoka kwako

Ana amua kuzaa na wewe baada ya kuzaa nawewe Ana Anza kuleta ugomvi wa makusudi ili mgombane/muachane

baada ya kuachana anakimbilia ustawi wa jamii anakuingiza mkataba kisha anaenda kuwinda mwanaume mwingine

Nahuyo mwingine nayeye ana mfanyia hivyo hivyo"

na Hawa ndio wake wanawake ambao Kila mtoto ana baba yake
Sasa nilitaka kujua kwamba je mnalijua hilo
na mna kabiliana nalo vipi ili kuepusha hizi single parents family?

Je! Ni Nini hatima ya watoto kulelewa na mzazi mmoja?

Na mnapo mfunga baba kwa kushindwa naomba ni rudie Tena kwakushindwa sio kwa makusudi kuhudumia familia yake

Huwa mna fikilia kuhusu Nini hatima ya upendo wa baba kwa watoto ambao alipelekwa jera kwa ajiri yao?

Lingine ni kwamba je mna fahamu kwamba wanaume Wana nyanya Sika na wanawake?

na hata huko mnako waambia waende hawasaidiwi zaidi ya kuchekwa?

Mwisho niulize kwamba

Je! hakuna namna nyingine ya kunusuru kizazi chetu na malezi ya mzazi mmoja zaidi ya hii iliyopo?
 
Kuna maswali machache huwa najiuliza pasipo kupata majibu

Kwamfano.

Kunafaida gani kumfunga mume au baba wa watoto aliye shindwa kutimiza mashart/mkataba alio wekewa na afisa ustawi wa jamii?

Huenda Labda anashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kipato kidogo alicho nacho au mazingira magumu kikazi anayo yapitia

hatimaye anashindwa kutimiza masharti Kisha anafikishwa mahakamani na kufungwa

Sasa ninge penda kujua kwamba

je! huwa mnajilidhisha vipi Kama ameshindwa kwa makusudi mpaka mna amua kumfunga kwa kosa la kushindwa?

Kingine ninacho jiuliza nikwamba

je! kumfunga huyo baba kuna wa saidia Nini watoto watakao Baki na mama yao au watoto na mama huku nje ya jera

Je Kuna fungu mnalitoa Kama serikali kwa ajiri ya kuwasaidia mama na mtoto/watoto kipindi ambacho baba yao mme mpeleka jera?

Kwa jinsi ninavyo fahamu Mimi hakuna baba anaye weza kuishi kwa amani wakati huku nyuma watoto wake wanatembea uchi,Wana lala njaa, nk

haiwezekani Labda Kama amepaka ziwa hao watoto anaweza kuya tenda hayo

Sasa je!

Kuna hasara gani huyo baba akiachwa huru lakini aka ambiwa kwamba ajitahidi kufikisha mahitaji kadri mungu atakavyo mjaria

iki wezekana hata kwa kutishiwa kitaaramu

je! hili halita kuwa Bora kuliko lile la kumfunga??

Kuna Jambo lingine siku hizi limekuwa Kama biashara kwa wake zetu/wanawake

Kwamba ana kuchunguza kuhusu kazi na kipato chako akishajua aka jiridhisha kwamba kunafaida ataingiza/kutengeneza kutoka kwako Kama mwanaume

Ana amua kuzaa na wewe baada ya kuzaa nawewe Ana Anza kuleta ugomvi wa makusudi ili mgombane/muachane

baada ya kuachana anakimbilia ustawi wa jamii anakuingiza mkataba kisha anaenda kuwinda mwanaume mwingine

Nahuyo mwingine nayeye ana mfanyia hivyo hivyo"

na Hawa ndio wale wanawake ambao Kila mtoto ana baba yake"

Sasa nilitaka kujua kwamba je mnalijua hilo
na mna kabiliana nalo vipi ili kuepusha hizi single parents family?

Je! Ni Nini hatima ya watoto kulelewa na mzazi mmoja?

Na mnapo mfunga baba kwa kushindwa naomba ni rudie Tena kwakushindwa sio kwa makusudi kuhudumia familia yake

Huwa mna fikilia Nini hatima ya upendo wa baba kwa watoto ambao alipelekwa jera kwa ajiri yao?

Lingine ni kwamba je mna fahamu kwamba wanaume Wana nyanya Sika na wanawake?

na hata huko mnako waambia waende hawasaidiwi zaidi ya kuchekwa?

Mwisho niulize kwamba

Je! hakuna namna nyingine ya kunusuru kizazi chetu na malezi ya mzazi mmoja zaidi ya hii iliyopo?

ahsante
 
Salaam Mh. Waziri Dkt. DG
Maoni:

Katika makundi maalum kuna kundi ambalo binafsi naona linahitaji kuongezwa, kama tayari lipo nitafurahi kupata taarifa. Tuna vijana kwenye familia zetu ambao huwezi kusema wanachangamoto za kutumia madawa ya kulevya au matatizo ya akili kwa kiwango cha kuwapeleka kwenye vituo maalum.

Vijana hawa ni ama kutokana na malezi yenye upungufu wa ushiriki wa wazazi wote wawili na athari za makundi rika wanaonekana kushindikana.

Utakuta shuleni wameshindikana, nyumbani wameshindikana na kila wanakopelekwa wanakuwa mzigo. Nina case ambayo naendelea kuihudumia baada ya kusoma kitabu cha 'Helping people change: coaching with compassion for lifelong learning and growth' cha Richard Boyatzis (2019).
Maendeleo kwa case yangu ni mazuri kwani baada ya kijana huyo kushindikana katika maeneo mengi kwa muda mrefu niliamua kubeba jukumu na sasa naona kuna dalili za matumaini kwamba anabadilika. Kitabu nilichotaja hapo juu kilinisaidia kunipa mwanga wapi nianzie na tunaendelea vizuri.

Kutokana na hilo nikajikuta napata wazo, nchini kwetu wapi unaweza kumpeleka kijana anayepitia katika hali hiyo hata kwa miezi sita au mwaka mmoja akafundishwa kwa huruma na upendo na yeye mwenyewe akajitafuta mpaka akajipata (kwa lugha ya vijana) na akafundishwa na kupata ujuzi kumsaidia kuendesha maisha yake. Kama vituo vipo nitafurahi kufahamu. Kama havipo nilete pendekezo hili kwako uone namna linavyoweza kufanyiwa kazi ili tuwasaidie vijana wa namna hii wajitafute kupitia mikononi mwa waliopata mafunzo ya kusaidia watu kubadilika wenyewe pale wanapowafundisha kwa huruma na upendo.
 
Back
Top Bottom