Tumezindua Sera mpya ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake, 2023

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 8 Machi, 2024 Dodoma, Chamwino ambako pia TUMEZINDUA SERA MPYA ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya Mwaka 2023 mbadala wa ile ya mwaka 2000.

Sera hii ya Mwaka 2023 imezingatia maeneo mapya kadhaa (tutaendelea kuelimisha) na kubwa ni imejumuisha masuala ya maendeleo ya wanaume siyo wanawake tu kwani, imetambua kuwa, maendeleo na ustawi imara na endelevu ni ule unaogusa Jinsia zote kike na kiume.🤝

Ahsante Sana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe Rosemary Senyamule kwa ushirikiano wako.

Pongezi ziende kwa Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Wizara mpya na Sera mpya.

Ahsanteni Wadau wote na wananchi wote kwa ushirikiano wenu kwenye kutoa maoni kwa ajili ya kuandaa sera ya 2023, ahsante kwa jinsi ambavyo mmekuwa mkitoa ushirikiano wa maoni, mawazo na kutenda pamoja na Wizara yenu ya Jamii

Tuendelee kushirikiana tunapoelekea kuboresha sheria, mipango na mikakati ya kisekta ngazi zote, Ili iakisi sera hii mpya.

Shukrani View attachment 2928522View attachment 2928527View attachment 2928531View attachment 2928533View attachment 2928534

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Jinsia zingine za duniani nazo zimo? "LGBTQ"?
 
Haya mambo ya jinsia na usawa naona kabisa tumeparamia mtumbwi wa wamagharibi bila kuelewa jahazi linaelekea wapi.

Itafikia kipindi a male child will need social support to survive. Hii sio sawa kabisa.
Walipaswa kubaki kwenye Haki za wanawake na sio usawa wa jinsia...
Usawa WA jinsia most likely mwanaume anakandamizwa..

Kukitokea Vita evacuation inawahusu wanawake na watoto..
Wanaume mnaambiwa bakini mtetee nchi yenu...ikija Amani Tu ...mnaambiwa kaeni tayari Kwa usawa WA jinsia....
 
She believe in being strong when everything seems to be going wrong, she believe that happy woman are the prettiest woman's
 
Attachments

  • IMG-20240308-WA0003.jpg
    IMG-20240308-WA0003.jpg
    58.4 KB · Views: 2
Haya mambo ya jinsia na usawa naona kabisa tumeparamia mtumbwi wa wamagharibi bila kuelewa jahazi linaelekea wapi.

Itafikia kipindi a male child will need social support to survive. Hii sio sawa kabisa.
Mm sijaelewa hivyo, maana utekelezaji mtapanga wenyewe jamii, mm sijaona wapi humo kwenye sera kuna mwanya huo kinyume na mazingira yetu na Mila na tamaduni zetu kwamba tunachukua hela za bajeti tunapanga vitu tofauti.... Sijaona hilo lengo humo... Ahsante kwa maoni, maana kwa njia ya mijadala ndiyo tunapata fursa za kuelewana....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Walipaswa kubaki kwenye Haki za wanawake na sio usawa wa jinsia...
Usawa WA jinsia most likely mwanaume anakandamizwa..

Kukitokea Vita evacuation inawahusu wanawake na watoto..
Wanaume mnaambiwa bakini mtetee nchi yenu...ikija Amani Tu ...mnaambiwa kaeni tayari Kwa usawa WA jinsia....
Hao lazima wame kopi mambo ya sera za LGBTQ.
 
Walipaswa kubaki kwenye Haki za wanawake na sio usawa wa jinsia...
Usawa WA jinsia most likely mwanaume anakandamizwa..

Kukitokea Vita evacuation inawahusu wanawake na watoto..
Wanaume mnaambiwa bakini mtetee nchi yenu...ikija Amani Tu ...mnaambiwa kaeni tayari Kwa usawa WA jinsia....
Tangu enzi za kale wakina mama na watoto wakati wa mapigano walikuwa wanaokolea kwanza. Je sasa hivi unajua Dunia inao wangapi kwenye vyombo vya ulinzi na majeshi? Na unajua vita ya siku hizi ni aina ipi na inatumia zana gani ikiwemo za kidigitali zinazohitaji elimu elimu elimu....

Mijadala ni Bora na inajenga uelewa wetu sote. Ubarikiwe

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Tunahitaji kuwaona akinamama peke yao wakikatiza misitu ya DRC kuelekea Lubumbashi na Malori kutokea Tanzania.
Tunahitaji kuwaona akinamama kwa wingi wao wakiwa front line kwenye vikosi vya mizinga au infantry division.
Tunahitaji kuwaona akina mama kwa wingi wao kwenye machimbo ya madini huko underground wakishika mitalimbo.
Tunahitaji kuwaona akina mama baharini huko deep sea wakivua samaki.
Tunahitaji kuwaona akina mama wakipigwa na mawimbi deep sea huko kwenye cargo ships.
Tunahitaji kuwaona akinamama kwenye manowari za kivita na meli za kivita + ndege za kivita.
Tunahitaji kuwaona mamilioni yakinamama huko kwenye magerage mitaani wakishusha mengine na magearbox.

Kumuempower mwanamke awe Sawa mwanaume na hata kuwa juu ya mwanaume ni kuifanya dunia kuwa sehemu hatari na mbaya sana kuishi, mambo mengi hayatafanyika na duniani watu watakufa kwa njaa na majanga maana wenye uwezo wa kuzuia na kupambana nayo wamenyang'anywa hiyo mamlaka.
 
Mm sijaelewa hivyo, maana utekelezaji mtapanga wenyewe jamii, mm sijaona wapi humo kwenye sera kuna mwanya huo kinyume na mazingira yetu na Mila na tamaduni zetu kwamba tunachukua hela za bajeti tunapanga vitu tofauti.... Sijaona hilo lengo humo... Ahsante kwa maoni, maana kwa njia ya mijadala ndiyo tunapata fursa za kuelewana....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Pakia hiyo sera jamvini wadau wasome ili mjadala uwe na tija.
 
Itawafikia tu kwa kuwa kuna mpango wa elimu kwa jamii ambapo, wataalamu wote watakuwepo siku hiyo kujibu, kufafanua, kuelimisha. Mtaalikwa wanajamii wa makundi mbalimbali. Haiwezekani sera iandaliwe, ibebe kitu hasi halafu tena tushirikishe jamii.

Ratiba ya elimu kwa umma hadi online itatolewa kwani Iko kwenye mpango.

Ahsante kwa maoni.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 8 Machi, 2024 Dodoma, Chamwino ambako pia TUMEZINDUA SERA MPYA ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya Mwaka 2023 mbadala wa ile ya mwaka 2000.

Sera hii ya Mwaka 2023 imezingatia maeneo mapya kadhaa (tutaendelea kuelimisha) na kubwa ni imejumuisha masuala ya maendeleo ya wanaume siyo wanawake tu kwani, imetambua kuwa, maendeleo na ustawi imara na endelevu ni ule unaogusa Jinsia zote kike na kiume.🤝

Ahsante Sana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe Rosemary Senyamule kwa ushirikiano wako.

Pongezi ziende kwa Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Wizara mpya na Sera mpya.

Ahsanteni Wadau wote na wananchi wote kwa ushirikiano wenu kwenye kutoa maoni kwa ajili ya kuandaa sera ya 2023, ahsante kwa jinsi ambavyo mmekuwa mkitoa ushirikiano wa maoni, mawazo na kutenda pamoja na Wizara yenu ya Jamii

Tuendelee kushirikiana tunapoelekea kuboresha sheria, mipango na mikakati ya kisekta ngazi zote, Ili iakisi sera hii mpya.

Shukrani View attachment 2928522View attachment 2928527View attachment 2928531View attachment 2928533View attachment 2928534

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Naam,,,,na mipango yenu ikawe kile mkitakachoo
 
Nchi zilizo endelea walianza hivi hivi kuwaweka wanawake juu kabisa ..
Halafu kilichofata ni "watu wa jinsia moja" kuja juu ya wanawake...
Wanawake walitumika kama "chambo" now mpaka Kanisa Katoliki liko mbele kabisa ....kuwapa Haki zaidi watu wa jinsia moja ...halafu ndo wanafata wanawake...
Wanaume wanakandamizwa...ukioa ukiacha nusu ya Mali zako zinaenda..
Kumtongoza mwanamke Tu unaweza shitakiwa Kwa sexual harassment...
Na ombea mwanamke asimzidi kipato,cheo mwanaume ndani ya familia
Mwanamke atampanda mwanaume mpaka atajua hiki nini

Ova
 
Naona ulimwengu wa sasa mwanamke,mwanamke anapambana kweri kweri awe sawa na mwanaume,mpaka kwenye kutoa maamuzi ndani ya nyumba

Ova
Mwanamke anajipambania mwenyewe. Sasa kama wanaume mmekaa mnasubiri wengine wawapambanie madhara yake mtayaona miaka ya hivi karibuni.
 
Tuendelee tu kumeza haya mambo kama yalivyoanzishwa na wazungu pale Beijing na kuyashadadia huku Africa.

Mwanaume ni mwanaume tangu Mungu alivyoumba ulimwengu, na mwanamke ni mwanamke toka ulimwengu ulivyoumbwa.
Kuvimba shingo na hizi 50/50 kutakuja kutuletea shida sana duniani hasa pale dunia itakapoamua kwa dhati sasa iwe 50/50 sidhani kama itafika 5yr kabla Mwanamke hajasurrender.

Mwanaume ndio mhimili wa dunia, akianguka Mwanaume na dunia ndio imeishia hapo, Akinaa mama wanapokimbia nafasi yao waliyoumbiwa ni kusaliti uumbaji na matokeo yake ni mabaya Sana.
Mwanamke sahv anataka awe ngoma draw na mwanaume

Ova
 
Na ombea mwanamke asimzidi kipato,cheo mwanaume ndani ya familia
Mwanamke atampanda mwanaume mpaka atajua hiki nini

Ova
kwanza imebidi nitabasamu tu. Hivi kweli hizo za kutoheshimu nafasi ya baba kwenye familia siyo tabia tu za mtu mwenyewe? Kwamba hadi awe na kitu ? Siyo kwamba alikuwa nazo tu hizo tabia fiche?

Back
Top Bottom