True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

01
Tumezaliwa watoto 3 katika familia ya mzee Faida Bhuhabi, mimi pamoja na dada zangu wakubwa wawili, katika mkoa wa geita, wilayani geita vijijini, mwaka 2009 nikamaliza elimu ya msingi, basi wakati nasubiri matokeo nikawaomba wazee niende kwa babu kizaa baba kijijini, siku ya safari mama akanifungashia vitu vya kumpelekea babu, sukari, unga wa ngano, mchele, mafuta ya kupikia, chumvi na hela kiasi, mzee pia alinipa laki 1, kwa mgao wa babu apate 40 elfu, bibi 30 elfu na mimi 30 elfu, 10 elfu ningetumia kama nauli, nikainza safari, ilikuwa december mwanzoni, nikapanda basi saa 1 asbuhi kutoka katoro geita kuelekea nyankumbu, dakika 35 zilipotea kufika nyankumbu, kisha nikapanda gari jingine kuelekea bukoli geita, baada ya saa 1 nikashuka bukoli {ikina} kisha nikachukua daladala (baiskeli} kuelekea mbogwe vijijini kwa babu na bibi, mahali ambako ndo chimbuko la mkasa wangu lilikoanzia, basi midi ya saa 11 jioni nilifika kijijini pale, watu wote walionekana wamekusanyika uwanjani....!
 
Tuendelee
Saa 11 nafika kijijini pale tunaona watu wamejazana uwanjani, nikajua pale kuna boli linatembea, nikawaza, hapa ndo penyewe sasa, basi tukiwa pale senta, (tupaite isonda sio jina rasmi) tukamwona binti kabeba ndoo ya maji, tulimsalimia kisha tukamwuliza kwa mzee bhuhabi ni wapi? Yule binti akastuka, akanitazama kisha akauliza ahabhalogi gete? (kwa wale wachawi?) sikujibu, tukatazamana na wale wakimbiza daladala, walikuwa wawili, mmoja alibeba mizigo, mwingine alinibeba mimi! Basi yule binti alituelekeza kisha tukashika njia kuelekea kwa babu, tulifika pale ikiwa saa 12 kasoro dkika 6. Tulipokelewa na bibi ambae alionekana kuchangamka sana, huku nikiwa na aibu na hofu iliyotokana na kuambiwa ninapokwenda ni wachawi wa kupindukia, nilitamani wale daladala waondoke mapema ili kukwepa aibu ile, kwani kila tukikutanisha macho tu, nilihisi wananiogopa hata mimi, duh! Nakweli licha ya bibi kuwasihi wale waendesha daladala wasubiri apike haraka msosi waligoma na kuaga wakaondoka....!
 
Tunaendelea
Bibi aliingia jikoni akiniacha nimekaa kwenye kivuli cha mwembe, nyumba moja kubwa mgongo wa tembo yenye chumba na sebule, nyumba mbili ndogondogo kulia na kushoto mwa ile nyumba kubwa iliyokuwa imejengwa ikiangalia magharibi, huku zile nyumba mbili ndogo zikitizamana, yakwanza slopu ya bati kama 8 hivi, imepigwa lipu kwa nje hii ilitizama kusini, na nyingine ya ukubwa kama huo ila ya nyasi ikitizama kaskazini, humu ndio bibi aliingia na mda kidogo nikaona moshi unafuka juu nyumba kuashiria moto umewashwa kwa ajili ya msosi,
Basi nikiwa nashangaa mazingira pale bibi alitoka jikoni akanambia njoo hapa mme wangu, basi nikasogea, huku akielekea nyuma ya ile nyumba ya nyasi, tulipofika nyuma ya nyumba, kulikuwa na mahindi yamelimwa kuizunguka mji wote ule,
Ndipo bibi akasema nisaidie kumkamata yule jogoo mwekundu, dah! Mate yalinidondoka palepale ilihali bibi aliona kitendo kile, akasema, usijali mme wangu, yaani hapa nataka mpaka usahau kurudi kwa mama mkwe, kuwa na amani..!
 
Tunaendelea
Basi nilimkimbiza yule jogoo ndani ya shamba la mahindi, jogoo alikuwa na kasi sana, huku akipiga kelele alikimbia mpaka nyumba jirani, sikutaka kumwacha nikamfata, alipofika kwenye ule mji wenye nyumba 3 za nyasi zote, alikimbilia ndani moja kwa moja, kulikua na binti aliekua anaanua maharagwe, haraka alisimama na kuniangalia, tukakutanisha macho yetu, dah! Bonge la binti, mzuri, mtoto akanikazia macho, haraka nikamsalimia,
Habari za jioni mchumba
Akajibu natamanile(sijui)
Dah! Ikabidi niongee kikabila kwani nilikuwa nakijua vizuri tu kisukuma, basi nilimwambia naitwa nzehe, nimgeni wa mzee bhuhabi, hivyo naomba unikamatie huyo jogoo,
Basi binti akaingia ndani, mashalah! Huko nyuma mtoto kajaliwa kiasi! Basi alimleta yule kuku kisha nikaaga nakuondoka, nimepiga kama hatua 15 nikageuka kumwangalia nikidhani huenda atakua ananiangalia, hola, binti alikua na hamsini zake anakusanya maharagwe,
Nilifika kwa bibi nikamkabidhi jogoo, akasema chukua kisu pale kwenye uchanja....!
 
Tuendelee
Basi bwana, nilimchinja jogoo yule, nilirejea nakupiga hodi jikoni, lakini bibi hakuitikia,
Nikawaza huenda kaenda msalani, basi nikaingia jikoni na kumweka yule jogoo kwenye sufuria, nikatotoka nje,
Kama dakika mbili hivi kupita bibi alikuja akiwa ameongozana na binti mmoja aliyeoneka mcheshi sana,
Samahan mme wangu nilitoka kidogo bila kukuaga, alitania bibi,
Nami nikamwambia wala asijali, basi yule binti alinisalimia kirafiki kabla hawajaingia jikoni na bibi, zilipita kama dakika 5 bibi akatoka akiwa kabeba mzigo kichwani, akanambia ngoja nikuache kdg mme wangu nikimbie mashneni, mikajibu sawa bibii
Naomba uchukue kuni pale uwashe moto hapo kwani baridi limeanza, alinionesha sehemu wanapowashaga mto (shikome)
Basi nikachukua kuni zilizokuwepo pale nikazipanga vizuri, kisha nikaenda jikoni kuchukua mtoto, nilimkuta yule binti aliekuja na bibh akimwondoa manyoya yule kuku, nilimwomba anipatie makaa mawili ya moto ili niwashie moto, binti yule kwa uchangamfu alinipatia moto nikaondoka....!
 
.....!
Niliwasha moto pale nje(shikome) kisha nikachukua kiti na kukaa karibia na moto, muda kidogo alikuja yule binti akiwa kabeba rufuria na kisu, ndani ya sufuria kulikua na yule kuku alienyonyolewa manyoya, basi binti kwa ustaarabu akaniomba nimshikie ili amkate vipande vipande yule kuku kwani anakazi nyingine ya kufanya nyumbani kwao,
Nilimshikia akaianza kazi ile mara moja.
Unaitwa nani? Aliniuliza yule binti huku anaendelea na kazi yake,
Naitwa Buhabhi jina la babu, ila nitapenda ukinita nzehe, nilijibu,
kwanini unapenda jina la nzehe (mzee) aliuliza tena,
Napenda jina hilo kwa sababu ndo jina ambalo mama hupenda kuniita kwa kuhofia kulitaja jina la baba mkwe wake (babu kizaa baba) nilimjibu.
Nikweli sio vizuri kutaja jina la mkwe, alisema yule binti na kuongeza,
Sasa mbona hujaweka kuni kubwakubwa (shitinde) kwenye moto wako? Aliuliza huku akinitazama usoni,
Mie sijui bwana, nilimjibu,
Kuni kubwa ndo uhai wa moto ule, yani bila hizo moto hautodumu, basi nilisogeza magogo mawili makubwa nikachochea
 
.....!
Wewe unaitwa nani?
Nilimwuliza,
Naitwa yunge, alijibu,
Unamiaka mingapi yunge? Nilimwuliza,
Aah mimi ni dada yako kabisa, yaani unanifata mara mbili na nusu, alijibu na kutania kidogo huku akiinuka na kuelekea jikoni,
Nilijichekesha na kuingizia utani kdogo, hata ingekua nakufata mara 10 poa tu, ila wewe pekee ndo mchumba wangu,
Aligeuka kwa haraka nakunitazama, kisha akasema, hujamuona yunge mdogo ndo maana unasema hivyo, ila ukimwona hutanikumbuka hata mie niliekufundisha kukoka moto (shikome) alijibu huku akiingia jikoni,
Nikawa nawaza huyo yunge mdogo ndo nani? Bila shaka ni binti mzuri sana, japo kwa umri wangu miaka 19 nilikuwa sijawahi kujihusisha na mapenzi, japo utani wa hapa na pale shuleni, sikuwa na demu bado, wala sikua na mpango wa kuanzisha mahusiano yoyote, lengo langu ilikuwa nimwombe babu majaruba kadhaa nilime mpunga, na lengo langu ilikuwa nikipata gunia 5, itapendeza sana...!
 
...!
Muda kidogo bibi akatokea, huku mzigo alokua amebeba wakati anaondoka kwenda mashneni ukiwa umepungua sana, nikajiongeza, atakua alienda kukoboa mpunga, kwa hiyo leo ni wali kuku, dah! Uchu ukawa unanizidi!
Ulipita muda kidogo yunge akaaga kuondoka, alikubaliwa na bibi, kisha akaniaga mimi pia, nkamkubalia,
Kwahio hunisindikizi hata kidogo? Aliuliza yunge,
Eti msindikize mwenzio basi, ila usimfikishe nyumbani kabisa, mama mkwe mkali mno, alisema bibi.
Niliinuka na kumsindikiza yunge kwani giza lishaingia sasa,
Nzehe nikwambie mdogo wangu, kuwa makini sana kwa mabinti wa kijiji hiki mdogo wangu, utapotea, nakutahadharisha mapema japo sijui utakaa hapa kwa muda gani! Ila kama mdogo wangu nakusihi jiweke mbali na wasichana wa hapa, tena uwe makini sana,alisema yunge,
Niliogopa sana, nikamwambia sina mpango na mademu, kililichonileta hapa ni kumsalimia bibi na babu yangu, kingine kama ntapata jaruba za kulima ntakua nashinda majarubani kupanda mpunga, nilimjibu,
Mhh? Tutaona...!
 
Niliagana na yunge huku akiniahidi atamwomba mama yake kuna majaruba matatu yamebaki, kuliko yabaki bila kulimwa bora wanipatie niyalime mimi, ikizingatiwa familia zile mbili walikua na ukaribu sana,
Nilirudi mpaka pale nyumbani kwa babu ambae niliambiwa aliondoka asubuhi kwenda mnadani kununua mbuzi,
Nilikaa pale nje nikiota moto mpaka bibi aliponiambia nichukue maji kwenye mtungi nikaoge,
Nilioga kisha nikaingia ndani ya ile slopu, kulikuwa na kitanda kizuri tu cha futi 4×6, nilitoa mafuta ndani ya begi langu na kujipaka, nikabadili nguo huku onyo la yunge likiwa kila mara linajirudia kichwani mwangu, nikikumbuka nimemwambia sikuja pale kwa ajili ya mademu, bali nimekuja kwa mambo muhimu tu,
Huku akinijibu tutaona,
Pia ile kauli ya binti tuliemwulizia kwa babu mara ya kwanza kabisa kule senta na kutustua kwa kusema mnaenda kwa wale wachawi? Dah! Niliogopa, saa2
Nkiwa naota moto pale nje mara ghafla nikasikia kelele kule senta, ambapo umbali wa kutoka pale kwa babu kufika senta ni kama daki 5 hivi..
 
Tuendelee
Nikiwa nimekaa pale nje naota moto, ghafla nikasikia yowe kali, watu walipiga kelee kwanguvu, yowe lilikuwa kali sana, fisiii, fisiii, dah! Bibi alitoka jikoni haraka huku ameshika kiuno,
Leo mapema tu? Mhh? Alisema bibi huku akitega sikio kusikiliza kwa makini,
Kwani vipi tena bibi? Nilimwuliza,
Kuna fisi anatusumbuaga sana, anakamata mifugo usiku watu wakiwa wamelala, ila leo naona amefata windo lake mapema tu, alijibu bibi,
Sasa bibi unaonaje nikielekea huko nikaone kinachoendelea maana si vyema kukaatu ili hali nimesikia yowe na watu baadhi wameniona, hivyo haitapendeza nikae tu, nilimtahadhalisha bibi,
Hee! Wewe kumbe umekua babu yangu, siamini kama maneno hayo unayaongea wewe, alitania bibi na kuongeza, baki hapa usiku huu uende wapi? kaa hapo ule, naona njaa inataka kukuua,
Sawa bibi, nilimjibu huku nikirudi kukaa kwenye kiti. Bibi aliingia jikoni na kuleta maji kwenye birika kubwa la shaba, glasi mbili za shaba (bilauli) na kikalai kidogo kwaajili ya kunawia mikono,
Karibu chakula mme wangu
 
Bibi alileta chakula pale pale, akaleta kimkeka akakaa, tulianza kushambulia wali uliokua kwenye sinia kubwa, huku bibi akiwa kaniwekea minyama lundo kwenye kibakuli kidogo cha udongo, yaani paja, filigisi na kidali humohumo, dah! Nilikula huku nikijiwazia eee kwa hali hii ntarudi nyumbani kibonge kweli!
Wakati tunamalizia kula bibi akachombeza, unamuwaza mchumba?
Mchumba tena? Hapana bibi, nawaza ya fisi kuiba mbuzi mapema tu hii, nilimjibu,
Wewe unashangaa hivyo tu? Wanatokeaga hata mchana wanabeba wanacho kitaka, hivyo kuwa na amani ni mambo ya kawaida tu huku na utayazoea, alisema bibi,
Hodi hapa, ilisikika sauti ya kiume, karibuu, aliitikia bibi,
Babu yako huyo amerudi! Nilinyanyuka na kumpokea bab baiskeli aliyokuwa anasukuma, huku kwenye karia amefunga karai na mbuzi dume kwa ndani yake!
Oooh! Umefika mzee mwenzangu? Karibu sana babu, alinichangamkia mzee bhuhabi,
Asante babu nshakaribia,
Basi nilifungua karai na kumtoa yule mbuzi dume aliyehasiwa (maksai) mzito na amenona sana.
 
Bibi alileta chakula pale pale, akaleta kimkeka akakaa, tulianza kushambulia wali uliokua kwenye sinia kubwa, huku bibi akiwa kaniwekea minyama lundo kwenye kibakuli kidogo cha udongo, yaani paja, filigisi na kidali humohumo, dah! Nilikula huku nikijiwazia eee kwa hali hii ntarudi nyumbani kibonge kweli!
Wakati tunamalizia kula bibi akachombeza, unamuwaza mchumba?
Mchumba tena? Hapana bibi, nawaza ya fisi kuiba mbuzi mapema tu hii, nilimjibu,
Wewe unashangaa hivyo tu? Wanatokeaga hata mchana wanabeba wanacho kitaka, hivyo kuwa na amani ni mambo ya kawaida tu huku na utayazoea, alisema bibi,
Hodi hapa, ilisikika sauti ya kiume, karibuu, aliitikia bibi,
Babu yako huyo amerudi! Nilinyanyuka na kumpokea bab baiskeli aliyokuwa anasukuma, huku kwenye karia amefunga karai na mbuzi dume kwa ndani yake!
Oooh! Umefika mzee mwenzangu? Karibu sana babu, alinichangamkia mzee bhuhabi,
Asante babu nshakaribia,
Basi nilifungua karai na kumtoa yule mbuzi dume aliyehasiwa (maksai) mzito na amenona sana.
Mkuu andika sehemu ya ngapi ili iwe rahisi kukumbuka tumeishia wapi sawaa
 
Baadae nilipata kujua yule mbuzi alinunuliwa kwa ajili ya kitoweo weekend ilokuwa inafata kwani babu alikua amealika watu wengi kwa ajili ya kuja kumsaidia kupanda mpunga, (kijini watu hualikana ktk shughuli mbali mbali kama kulima, kupalilia, kupanda, mpunga pia wakati wa mavuno)
Tulisalimiana na babu kwa bashasha, kisha akaenda kuoga, muda kidogo akarejea pale penye moto akakaa na kutengewa chakula, alikula huku akiniuliza habari za nitokako ilikuwa kwema na wote niliowaacha nyumbani hali zao zipoje?
Hawajambo wote na wanakusalimieni tu,
Alimaliza kula babu vile vyombo nikaviondoa pale, bibi alikuja na kukuta vyombo nimetoa,
Basi bab akasema, nenda kapumzike mjukuu wangu, mie narudi senta kuna uvamimzi umetokea, fisi kakamata mtoto na kutokomea kusikojulikana,
Hah? Mtoto tena? Nilistuka sana,
Ndo hivyo mzee mwenzangu, wewe kapumzike, kesho tutaongea, alisisitiza babu,
sawa babu, ila nina mzgo wako humu ndani,
Nilimwambia babu,
Hee! Mzigo? Ebu tuone,
Babu alinichangamkia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom