Toyota wanawezaje kutengeneza magari zaidi ya Milioni 9.2 kwa mwaka?

Alejandroz

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
328
378
Kichwa cha uzi cha husika
Nimesoma sehemu kuwa kampuni ya Toyota wanatengeneza zaidi ya magari 9.2M kwa mwaka na wana viwanda 67 vya utengenezaji duniani kote,, nikapiga hesabu kama ifuatavyo;
Kwa mwaka magari 9.2M
9.2M ÷ (Miezi 12) =766,667 kwa mwezi
766,667÷(siku 30) = 25,556 kwa siku
25,556 ÷ (Viwanda 67) = 381 kwa kiwanda
Maana yake kiwanda kimoja kinatengeneza zaidi ya magari 381 kwa saa 24,, hii inawezekanaje?
Ni kweli kwamba wanatumia robots n.k lakini hii idadi imenishangaza

Huenda kuna kitu sijakielewa,, karibu tupeane ufafanuzi
 
Toyota wana Plants Nchi zaidi ya 16. Huo uzalishaji rahisi sana kutokana na wingi wa Plant zao Mkuu
 
Kwa mfano nchini ujerumani mwaka 2019 yalitengenezwa jumla ya magari million 6.9 hii ni idadi ya magari Kwa makampuni yote ya ujerumani na 2022 idadi ya uzalishaji ulishuka Hadi milioni 4.3..
Kama Toyota pekeyake wanaweza kutengeneza magari milioni 9 Kwa mwaka basi watakuwa wanatisha Sana kwenye mauzo sipati picha Kwa idadi ya makampuni yote ya Japan itakuaje Kwa mwaka
 
Toyote wana viwanda vingi duniani vya kuunganisha magari (assembly) na pia wanatengeza wenyewe parts nyingi kama engine, gearbox, body na pia wana suppliers wazuri sana kwa parts zingine kama brake system, ABS, suspensions, safety belts n.k.
Pia muhimu sana Toyota wana process ya LEAN. Hii ni siku zote ni bidii endelevu ya kuongeza ufanisi katika kazi zao na kupunguza upotezi au hasara katika vyombo/miundombinu, wafanyakazi, wakati wa kuunda gari. Wanahesabu wakati waku kuunda gari mpaka sekunde. Sababu gari fulani ikipoteza muda kattika assembly line basi magari yote yalio katika msururu yatachelewa.
Pia moja ya kauli mbiu yao ni make it right first time. Yaani unda sawa mara moja, hakuna kazi ya kurudia kurekebisha.
 
Back
Top Bottom