Tetesi: Rwanda yanunua madini kwa siri nchini Tanzania na kuyauza tena kwa kampuni ya Apple

Mwenyewe niliuza chuma kutoka karagwe na tulikua tunauzia remera kigali, shinyanga na geita na kigoma hadi mpanda na sumbawanga wanyarwanda humiliki ardhi kubwa ya kilimo tena walinunua kihalali japo wako rwanda na kila mavuno wao hua na uhakika wa chakula na kuuza congo ya mashariki, mbona niliwahi kuandika hapa majuha yakapotezea note: mtutsi anayeishi tanzania ana haki na uraia wa rwanda pia na kwao hupiga kura kama mnyarwanda nashangaa serikali inapinga uraia pacha wakati watusi wana uraia wa tanzania na rwanda ukiwacheck viongozi wa bongo unaona hawa mazezeta kweli, maana mtu yuko runzewe, katoro, geita, ushirombo, kahama, mwanza, ngara, kakonko, kasulu, kibondo na ana uraia wa rwanda safi kabisa wao huku hua nawachek kama uhamiaji nawaona mazezeta tu
 
Acha umbea ..biasharano chain..wewe unachimba muuzie mnunuzi na mnunuzi nae anaenda kumuuzia mnunuzi mwingine na mnyororo wa thamani huwa hivyo mpk unamfikia mlaji wa mwisho. Kwenye maisha haya huwezi kuhodhi kila kitu
Kwanini wauze Rwanda.
 
Kuna tetesi madini yamekuwa yakinunuliwa kwa kasi ktk mikoa ya Geita na Shinyanga na wafanyabiashara wasio wazalendo.

Wafanyabiashara hao hupewa mitaji na serikali ya Rwanda japo wao ni watanzania.
Wanachofanya ni kununua almasi na dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na kuiuza nchini Rwanda kimagendo kwa siri kubwa sana. Jengo la ununuzi lipo jijini Kigali na Rushwa hutumika pakubwa kuwazima mamlaka za mipakani.

Inadaiwa wafanyabiashara hawa hufanya biashara nyingine halali kati ya kanda ya ziwa na Rwanda huku lengo fiche ikiwa ni madini ya Tanzania.

Haikubainika ikiwa kampuni ya APPLE ambayo huyanunua madini hayo kutoka serikali ya Rwanda kama inayo habari kuwa madini hayo hutoka nchini Tanzania.

Source: Wachimbaji wadogo Geita na Shinyanga.
kama mtanzania hajazulumika, amelipwa pesa yake, huoni kama Rwanda imekuwa soko kwa wachuuzi wetu? labda icho kipande cha magenzo kama anakwepa kodi, ila ukiondoa kodi, Mtanzania amedhulumika nini? mimi nitoke Rwanda na pesa yangu, ninunue madini yako, wewe unaondoka na pesa, kuna shida gani hapo? na hadi wauze kwa rwanda ujue pengine ndio wanaona kuna bei kubwa. na afterall, siukute wala sio rwanda, ila wazungu wamekuja pale kigali wanafanya hiyo biashara.
 
Haya wanunuzi wa dagaa wanyarwanda na waganda wako visiwa vyote na hawalipi royalty for export yaani wanavusha dagaa nje ya nchi lakini wanapewa vibali vya mikoani na dagaa zao hupitia pale magarini na kasenda yaani mamlaka zinatoa macho kwenye hiyo tozo Kwa mzambia na mmalawi tu lakini mnyarwanda na mrundi wao ni free, wanapoteza mapato mengi Kwa ujinga wao wenyewe
 
Nchi ya Tanzania ni shamba la bibi mtu anajipigia anavotaka tu, hakuna mtu wa kulinda rasilimali za nchi, acha wajipigie tu hakuna namna, saa nyingine unawaza hawa wajuba usalama wa taifa wanalewa tu au wanakazi gani au hao uhamiaji hata kufika visiwani kukagua uhalali wa watu hakuna wapowapo tu
 
Huyu Mama tunajiendea tu. Na Ukifika hadi 2030 warahi hii nchi itakuwa ishagawiwa yote. Tutampa kazi Rais ajae kuvunja mikataba na kurudisha Mali zilizopolwa.
 
kama mtanzania hajazulumika, amelipwa pesa yake, huoni kama Rwanda imekuwa soko kwa wachuuzi wetu? labda icho kipande cha magenzo kama anakwepa kodi, ila ukiondoa kodi, Mtanzania amedhulumika nini? mimi nitoke Rwanda na pesa yangu, ninunue madini yako, wewe unaondoka na pesa, kuna shida gani hapo? na hadi wauze kwa rwanda ujue pengine ndio wanaona kuna bei kubwa. na afterall, siukute wala sio rwanda, ila wazungu wamekuja pale kigali wanafanya hiyo biashara.
Ukwepaji kodi, serikali haiingizi kitu kwa rasilimali zake.
 
Waulize wizara ya uvuvi kua tozo ya royalty to export ya dagaa za Rwanda na Burundi ambazo hupitia kasenda na magarini na murusagamba, kabanga, muhange, kobero, mabamba, au kasulu wanapata shilingi ngapi Kwa mwezi wakikujibu niite muongo, yaani wanapoteza mapato mengi Kwa ujinga wao wa kiboya maana ni maboya
 
Back
Top Bottom