Tatizo la Takwimu: CCM imekataliwa japo inapendwa; CHADEMA inapendwa lakini...

Mimi ningekuwa kiongozi wala sihitaji kuzungumzia hayo.........nachukua bei ya unga, sukari, mafuta ya taa, umeme, na gesi nalinganisha na miaka mitano iliyopita halafu nachukua takwimu kutoka nchi yenye mazingira ya kwetu kama Rwanda, Angola Msumbiji halafu naawambia wananchi kwanini sisi isiwezekane. Nawaambia vijana wanaosoma kuwa nitaongeza wigo wa ajira kwasababu umri wa kustaafu ukifika sitaruhusu ajira za mkataba, rare professions kama udaktari, etc hawatafanya kazi za siasa, nitaondoa wakuu wa wilaya kwa kufanya hivyo nitasaave kiasi X kwa mwaka ambacho nitatumia kujenga madarasa mapya kila mwaka..........jamani CDM rudini chini mzungumze lugha ya watu ya kila siku......siasa za juu ya helikopta zafaaa kwa msisimmko tu ambao hudumu kitambo kidogo tu..........


Dah! yaani hapa umepiga mulemule, CDM wasipofanya hivi wasahau kuongoza Nchi.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji haya madata umeyazoa kwenye ile website ya Tume ya uchaguzi inayofanya kazi kwa matakwa ya ccm? Mbona 2010 Dr slaa alishinda kwa kishindo!!!!! Nenda kakusanye data zilozokuwa kwenye vituo vya kupigia kura siyo kwenye hizo website za ccm....

Mlishinda bila wabunge serikali mngeendesha vipi sasa.?!au wabunge pia mlichakachuliwa?!
 
Watu msimchukie Mzee Mwanakijiji bure badala yake tupambane na ukweli. Mimi mwenyewe nayajua majimbo zaidi ya 20 ambayo vyama vingine havikuwa na mawakala kabisa sasa hizi mnazoita "reliable data" nyie mmezipata wapi wakati kwenye maeneo mengi ambayo kulikuwa hakuna wagobea toka kwenye vyama vingine zaidi ya CCM kulikuwa hakuna mawakala wa vyama hivyo?

Hivi ni Madiwani wangapi wa CCM na wabunge walipita bila "Kupingwa" na kwenye majimbo hayo CHADEMA ilikuwa na mawakala kama haikuwa na mawakala takwimu za majimbo hayo wanazipata wapi? Wagombea ubunge wa CHADEMA na udiwani walikuwa ni asilimia ngapi ya wagombea wote. kwa mfano wagombea udiwani wa CHADEMA nchi nzima walifika hata asilimia 50?

Katika vitu ambavyo vyama vingine hawavipiganii vibadilishwe kimojawapo ni hili la mgombea kupita bila "Kupingwa". Madhara ya tukio hili ni kwa wananchi wa eneo husika kutokuwa katika mtiririko sawa wa uhamasikaji kushiriki kwenye uchaguzi kwa sababu wao tayari hawana "uchaguzi" badala yake inakuwa ni kazi ya mteule aliyepo kumpigia debe mgombea urais wa chama chake.
 
Last edited by a moderator:
Nilivyoelewa Mwanakijiji anatamani sana CDM ifanye zaidi ya inavyofanya sasa na bahati nzuri anaona uwezo huo CDM inao ila ''uzembe '' fulani unawafanya wawe hivyo. Kifupi anasema CDM inaweza kufanya zaidi, na yeye anatamani ifanye zaidi. Vinginevyo kwa nini awape mbinu za ushindi watu asiowapenda. Wengine wanaona kama anabeza hapana, ni kwasababu ya uchungu alionao. Takwimu alizozitoa ni ''facts'' ndizo zilizopo hawezi kujenga hoja kwenye takwimu ambazo haziko wazi.

Kweli kuna watu wengi sana mfano kada fulani ya wafanyakazi wa serikali hawaipendi kabisa CCM, lakini wao ni rahisi sana kurudisha mapenzi CCM kuliko CDM kwa sababu wananufaika na mfumo uliopo wa ''kiujanjanja serikalini''. Sasa CDM ikitaka kuwavutia watu kama hawa sio kwa kutumia M4C hawa wanahitaji mkakati wa tofauti kabisa ambao utawapa UHAKIKA kuwa wataweza kuishi kwa uhakika na kipato halali chini ya serikali ya CDM. Sijaona hata siku moja CDM inavyozungumzia mbadala wake kuhusu mambo ya ajira. Mfano, ajira nyingi kushikwa na wageni, soko la ajira EAC, umri wa kustaafu, ajira za mkataba baada ya kustaafu........mambo ni mengi sana. Mengine hayahitaji hata mikutano ya hadhara.......yanahitaji makongamano, na mijumuiko ya ndani ambako wangeweza kutoa sera zao. Shida naona kuna obsessession na siasa za majukwaani na kulipua mabomu.......mtoto wa kigogo akutwa na madawa ya kulevya.......inasadia nini kama wewe mwenyewe huwezi kumtaja kwa uwazi. CDM wavuke hatua ya kuwa chama cha kujibu mapigo bali wawe chama cha kutoa elimu na sera mbadala.

Mimi ningekuwa kiongozi wala sihitaji kuzungumzia hayo.........nachukua bei ya unga, sukari, mafuta ya taa, umeme, na gesi nalinganisha na miaka mitano iliyopita halafu nachukua takwimu kutoka nchi yenye mazingira ya kwetu kama Rwanda, Angola Msumbiji halafu naawambia wananchi kwanini sisi isiwezekane. Nawaambia vijana wanaosoma kuwa nitaongeza wigo wa ajira kwasababu umri wa kustaafu ukifika sitaruhusu ajira za mkataba, rare professions kama udaktari, etc hawatafanya kazi za siasa, nitaondoa wakuu wa wilaya kwa kufanya hivyo nitasaave kiasi X kwa mwaka ambacho nitatumia kujenga madarasa mapya kila mwaka..........jamani CDM rudini chini mzungumze lugha ya watu ya kila siku......siasa za juu ya helikopta zafaaa kwa msisimmko tu ambao hudumu kitambo kidogo tu..........
Kwa bandiko lako hili atakayekupinga usibishane naye hata kidogo!!
 
Hizo zilikuwa hoja za msingi, lakini Mzee Mwanakijiji kwakuwa anatumika kisiasa, na anakula pande mbili huku na kule anajitahidi kuwa neutral japo ukweli anaujua.

......
Nilisema hapa na hata kamanda Matola Mungi,na TUMBIRI, walisema MMJ atakuja na maneno mengi/ makala ndefu,
mpaka point unaitafuta kujua anamaanisha nini.

Simple, mfano hizo takwimu, ni figures ungeweza kabisa kutumia Table ikawa rahisi kuchambua na kueleweka,
siyo kukaa unajigonga gonga tu, mara uende kulia mara kushoto...(Unafanya makusudi)

Makusudi mengine-
Mbona huweki wazi takwimu za jinsi chadema kinavyokuwa? Uchambuzi unafanya general mwishoni unakiuwa chadema,

Tuambie Chadema kilikuwa na wabunge wangapi, 1995, 2000,2005,2010?
Tuambie Chadema kilikuwa na viti maalum vingapi 1995, 2000,2005,2010?
Tuambie Chadema kilikuwa kinaongoza halmashauri ngapi, 1995, 2000,2005,2010?
Tuambie Chadema kilikuwa madiwani wangapi, 1995, 2000,2005,2010?
Tuambie Chadema kilikuwa madiwani wangap viti maalum 1995, 2000,2005,2010?

Ukishamaliza linganisha kukuwa kwa Chama "kasi yake" kisha sema kuhusu chama 2015

Tofauti na hivyo utakuwa unabwabwaja tu, ndio maana siku hizi tunavyutiwa sana na uchambuzi wa Mchambuzi,
Siyo wewe maneno mengi.

ushauri wangu kwako mkuu Mzee Mwanakijiji kwa sasa unazeeke, ni vema ukajikita kwenye kuandika vitabu vya Riwaya zako za Mapenzi, huko ndio kunakufa, siasa huwezi tena.
 
Watu wameamua kuidekeza CDM kama mtoto apendwaye kwa sababu akifokewa analia, akigombezwa ananuna na akikaripiwa hulalamika kuwa hapendwi! Huku kudekezwa kwa CDM (kama kule kwa CCM) kuna hatari kwa taifa. Kwa upande wangu naamini changamoto kubwa kwa wanaotaka mabadiliko ni kuikalia CDM kooni hadi inolewe kuelekea kushinda sasa hivi iko butu hadi inakera.
!

M. M

Hili ndilo tatizo la mtoto anayedekezwa, hataki kuambiwa chochote na hili litawaathiri sana CDM katika kujipanga ili waweze kupewa dhamana ya Uongozi.

Kwenye siasa hasa kwa chama ambacho haijawahi kutawala inahitaji Busara ya khalli ya juu sana hasa kusikiliza yale ambayo hautaki kuyasikia.

CDM na wanachama wake ,wengi hasa walliopo JF hawataki kusikia wakikoselewa. Hawataki ufisaid unaowagusa viongozi wao uhojiwe na mtakumbuka ya Chacha wangwe.

Cha msingi kwa sasa na takwimu hizi CDM inabidi watengeneza safu ya uongozi ambayo itaweza kuwasiaidia kushinda na siyo safu ya uongozi iliyopo kwa ajili ya kulipua mabomu tu na kusaka madaraka.

Nina muda wa kuwafunza CDM kama wakitaka kusikiliza na kujifunza.
 
To tell you the truth naamini hiyo asilimia 57 imejirudia mara nyingi sana tangu uchaguzi wa 2010. Kuna watu wengi ambao wameandikishwa kupiga kura hawapigi kura kabisa. Sasa hili si suala la "kuboresha daftari tu" bali ni suala la a. waliondikishwa kupiga kura wapo na b. kutafuta jibu kwanini hawaji siku ya kupiga kura. Kwa mfano, mtindo wa kuweka siku moja (hasa Jumapili - si kwa sababu ya dini bali sababu ya siku yenyewe) watu kupiga kura ni mzuri? Je kuna uwezekano wa kupiga kura mapema (early voting)?

Hapo kwenye red, unataka kura ziwe zinalala kituoni ili watu waendelee kupiga kura siku inayofuata? Kwi kwi kwi, kwa uaminifu upi? Labda kama neno UCHAKACHUAJI halipo tena.

Kwa ujumla mfumo wa uchaguzi ni tatizo kubwa. Haiingii akilini watu kuzunguka na M4C na operesheni nzito nyingi huku wakiweka kando mapambano ya kuuchonga mfumo wenyewe utakaoruhusu wao kushika dola. Lazima haya mambo yaende sambamba. Unaweza kuwa na umma ulioiva kabisa kwa ajili ya mabadiliko kama tulionao sasa lakini kama njia yenyewe ya kuleta mabadiliko (Kwa maana ya uchaguzi) imezibwa ni sawa na bure labda kuopt njia nyingine zisizo za sanduku la kura ambazo kwa kweli hakuna mtanzania atakayezitaka.
 
CHADEMA inatakiwa kweli kuwa chama cha siasa.Pale inapokemewa ikubali kujirekebisha na pale inaposifiwa ikaze buti kuendeleza mapambano.Misuguano isiyo na tija pia inakidhoofisha chama.Viongozi wakubali kukosolewa kwani binadamu unajifunza kila siku.Pia uongozi uache kuongea kwenye magazeti pale panapotokea mgongano,wanatakiwa maswala yote ya kiofisi yajadiliwe ndani na siyo magazetini.
 
Tatizo la takwimu (za NEC). CCM imekataliwa (na wananchi) japo inapendwa (na NEC). Chadema inapendwa (na wananchi) lakini (imekataliwa na NEC).

Naziita takwimu za NEC kwa kuwa hizi takwimu hazionyeshi uhalisia wa mapenzi ya watanzania wanaoweza kupiga kura. Kusingekuwa na M.M. alichokiita "Voter suppresion" kwenye chaguzi zilizopita ninaamini kabisa takwimu za matakeo zingekuwa tofauti na hizi zilizobandikwa hapa. Lakini NEC ndiyo inayotangaza mshindi na inatangaza mshindi kutokana na takwimu hizi. Hivyo we have to deal with it. CHangamoto kubwa iliyopo mbele yetu kama tunataka kushinda 2015 ni kukabiliana na mbinu zote za "Voter suppresion". Bila hivyo Chadema itaendelea kukua kwa kasi mioyoni mwa wapiga kura lakini takwimu zitabaki vilevile "zikiipenda CCM".
 
Nimesoma makala yote, hujasema sasa chadema ifanye nini kucounter hizo mbinu za CCM za kujibakiza madarakani hata kama inakataliwa? Lakini pia kukiri kuwa CCM haiwezi kuweka mfumo utakao uiondoa madarakani kunafanya malalamiko yako dhidi ya viongozi wa chadema kuwa hawana mikakati thabiti ya ushindi yasiwe na mashiko kwani inawezekana CCM inashindwa lakini inajibakisha kwa mbinu zake chafu? Lakini pia kutumia takwimu ambazo zimepatikana kwa mbinu chafu, haziwezi kuelezea ukweli na uhalisia wa kukubalika kwa CCM au kukataliwa kwa chadema! lakini cha msingi nasubiria jibu la sasa tufanye nini?
 
M. M

Hili ndilo tatizo la mtoto anayedekezwa, hataki kuambiwa chochote na hili litawaathiri sana CDM katika kujipanga ili waweze kupewa dhamana ya Uongozi.


Hapo kwenye nyekundu wewe na M. M. hamjasema kweli. Ebu niambieni CDM inadekezwa na nani wakati nguvu kubwa ya dola inaelekezwa kuikandamiza?

Sikujua kuwa uongozi kwa maana ya kupewa dhamana uliyoisema ni maamuzi nje ya wapiga kura. Ikiwa ndiyo maana, basi inabidi kuwe na mfumo wazi na halali wa kuheshimu maamuzi ya wapiga kura na siyo NEC, UWT etc.

Kwenye siasa hasa kwa chama ambacho haijawahi kutawala inahitaji Busara ya khalli ya juu sana hasa kusikiliza yale ambayo hautaki kuyasikia.

Ina maana chama ambacho kinatawala hakina sababu ya kutumia busara yo yote kusikiliza yale ambayo hakitaki kuyasikia. Hapo tukubali kuwa chama tawala hakitaki kusikiliza yale ambayo hakitaki kuyasikia kwa sababu hayaendani na sera ya KUTAWALA MILELE. Kwa sababu hiyo lazima wakabiliane na hali hiyo kwa mbinu mbali mbali.

CDM na wanachama wake ,wengi hasa walliopo JF hawataki kusikia wakikoselewa. Hawataki ufisaidi unaowagusa viongozi wao uhojiwe na mtakumbuka ya Chacha wangwe.

Mimi binafsi ni member wa JF nawaunga mkono wote wanaochambua mstakabali wa nchi yetu kutokana na utaratibu wa hovyo kidemokrasia tuliona. Kwa sababu hiyo nashauri tu kama ukosoaji huo una uzito na una nia njema ni busara ujumbe huo ukafikishwa kupitia mfumo wa chama kupokea ushauri. Ni vema tukakosoa na kuishia hapo kama Great Thinkers; nadhani hatuna haki ya kugeuza jamvi letu kuwa jukwaa la kulazimisha maamuzi ya chama bali ni wachagizaji tu. Kama vyama vitanufaika na ukosoaji wetu ni vyema kinyume chake hatuna haki. Ndiyo maana wamejitenga sana kujibu michango yetu ila naamini wanaifanyia kazi kwa sababu michango ni mingi na ina thamani fulani kwa anayeguswa nayo.

Mimi sitakubali kuhusisha/kukumbushwa issue ya Chacha Wangwe kwa sababu undani wake hujauweka hadharani. Hata ungeuweka hadharanu undani huo, ni bure kwa hali halisi ya sasa kwa sababu haimpi Chacha Wangwe fursa yo yote.

Cha msingi kwa sasa na takwimu hizi CDM inabidi watengeneza safu ya uongozi ambayo itaweza kuwasiaidia kushinda na siyo safu ya uongozi iliyopo kwa ajili ya kulipua mabomu tu na kusaka madaraka./QUOTE]

Hapa umefuja wadhifa wako wa JF kwa kufanya hukumu kwa matakwa yako badala ya hoja inayochambulika. Nakuona hapa na rangi zako za kuchukia uongozi wa CDM (nyekundu) kwa kuwapa sifa ya ulipuaji wa mabomu (blue). Kiuandishi hata kihekima umejishusha; kwa sababu jamvi hili tunatoa hoja balanced, kwani hayo mabomu hayajaharibu maadui wetu wa ufisadi na kuiamsha serikali? Lakini demokrasia inakupa uhuru wakuachana na CDM kama hawakidhi matakwa yako. Maana yake hata unapowakosoa hawatakusikiliza kutokana na hukumu uliyowahukumu.

Nina muda wa kuwafunza CDM kama wakitaka kusikiliza na kujifunza.

Nitawashangaa kama watakusikiliza au watakupa nafasi ya kuwafunza. Nakushauri fanya jitihada za kuwasikiliza CDM halafu utake kujifunza wanachokifanya; tafakari chukua hatua.

Hizi takwimu unatakiwa uzichambue jinsi zilivyo siyo jinsi unavyotaka. Pia jiulize hizi takwimu zimekusanywa kwenye mazingira gani na viashiria gani. Kwa baadhi yetu zilishashindwa kuwa takwimu zenye manufaa ya uhalisia bali ni takwimu za hovyo zisivyokidhi vigezo pamoja na kuwa zinaonyesha chama tawala hakifanyi vizuri. Vyama vya upinzani vinajitahidi kukabiliana na hali halisi katika mazingira yaliyopo; kwa hiyo wanachokipata wapinzani si haba.
 
Tatizo la takwimu (za NEC). CCM imekataliwa (na wananchi) japo inapendwa (na NEC). Chadema inapendwa (na wananchi) lakini (imekataliwa na NEC).

Naziita takwimu za NEC kwa kuwa hizi takwimu hazionyeshi uhalisia wa mapenzi ya watanzania wanaoweza kupiga kura. Kusingekuwa na M.M. alichokiita "Voter suppresion" kwenye chaguzi zilizopita ninaamini kabisa takwimu za matakeo zingekuwa tofauti na hizi zilizobandikwa hapa. Lakini NEC ndiyo inayotangaza mshindi na inatangaza mshindi kutokana na takwimu hizi. Hivyo we have to deal with it. CHangamoto kubwa iliyopo mbele yetu kama tunataka kushinda 2015 ni kukabiliana na mbinu zote za "Voter suppresion". Bila hivyo Chadema itaendelea kukua kwa kasi mioyoni mwa wapiga kura lakini takwimu zitabaki vilevile "zikiipenda CCM".

Hapo umenena Jembe Ulaya kutumia takwimu za tume ambazo zinatokana na mbinu chafu za ccm, ni kujidanganya, hapa ni kuanzisha movement ya wapiga kura kudemand uwazi wa daftari la wapiga kura na uandikishwaji wa wananchi wote waliofikisha umri wa kupiga kura, hii kazi siyo ya chadema ni yetu sisi wapiga kura, kupiga kura ni haki ya kikatiba, tufungue kesi ikibidi kudai haki hiyo iheshimiwe, kwanini tunyimwe kupiga kura kwenye nchi yetu kwa kisingizio eti huna kitambulisho cha kupigia kura?
 
Last edited by a moderator:
kichwa cha nazi. hizo data za slaa kashindwa anazo yeye ya josephine tu labda huko chumbani. sisi hatuzijui. kwa nini anaongea kwa maneno na asilete hata za pale kwao karatu tu? day dreamers. na mtaota sana tuu.

.......

Ni kweli dada ngwendu naona unamuonea wivu Josphine. Dr alikutosa nini? pamoja na kukulipia mahari kweli slaa ni mbaya
.
 
"Voter suppression?",vipi hii ya kununua shahada za kupigia kura tunaiweka kundi gani? Je kuna uwezekano kupata age category ya wapiga kura ili analau tujue ni watu wa umri gani wanashabikia chama kipi? Hata hivyo umetuamsha na pole sana sana kwa wale wasiopenda kusoma makala ndefu.
Hiyo Voter suppression ameitaja kama factor moja. Hata hizo ulizozitaja nazo ni factor pia lakioni yeye Mwanakijiji aliamua kuizungumzia hiyo moja tu ili kuonyesha kule kupinmga kwake kuwa kura zilichakachuliwa wakati wa kupiga na kuhesabu siku ya uchaguzi
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji haya madata umeyazoa kwenye ile website ya Tume ya uchaguzi inayofanya kazi kwa matakwa ya ccm? Mbona 2010 Dr slaa alishinda kwa kishindo!!!!! Nenda kakusanye data zilozokuwa kwenye vituo vya kupigia kura siyo kwenye hizo website za ccm
kichwa cha nazi. hizo data za slaa kashinda anazo yeye ya josephine tu labda huko chumbani. sisi hatuzijui. kwa nini anaongea kwa maneno na asilete hata za pale kwao karatu tu? day dreamers. na mtaota sana tuu.
 
nikupe mfano mwaka 2010 vyuo vilichelewa kufunguliwa hii iliwanyima haki wanafunzi wengi vyuo vikuu kupiga kura
 
Back
Top Bottom