Tatizo la Maji shule ya Sekondari Same

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,618
4,363
Kwa wasioijua Same Sekondari ni moja ya shule Kongwe za Serikali Tanzania iliyoanzishwa mwaka 1952. Shule hiyo imekuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita (boys).

Kulikuwa na jitihada kadhaa za kutaka kuleta wanafunzi wa kike (wasichana) ila ikashindikana kutokana na tatizo kubwa la uhaba wa maji. Mimi mwenyewe ni Muhanga wa tatizo la maji kwani nilisoma shuleni hapo ambapo kulikuwa na tatizo kubwa kabisa la maji la kufanya wanafunzi waamke saa kumi ya alfajiri ili waende huko kituo cha relini kuomba kuchota maji kwenye bomba la watumishi wa kituo. Mara kadhaa tuliishia kula chakula cha usiku saa sita usiku na kuendelea... na kuishia kuoga hata mara moja kwa wiki kwa maji ya takribano lita tano (na joto lile la same!). Unaweza kutafakari mwenyewe huko chooni kulikuwaje?
Tatizo la maji shuleni hapo limedumu kwa zaidi ya miaka 30.

KILICHOSHANGAZA WENGI.....
Makamu wa Rais (Dct Mpango alifika Shuleni hapo tar 21 March 2024 na WANAFUNZI kumueleza tatizo la maji na kumuomba wachimbiwe Kisima. Makamu wa Rais aliguswa na hoja yao na kumuagiza Waziri wa maji atume timu kupima kama kuna maji wachimbe kisima.

Amini usiamini; siku ya pili gari la kuchimba maji lilifika Shuleni hapo na kuchimba Kisima na maji yakapatikana mengi tu na hivyo kumaliza tatizo.

Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa wanafunzi ila iliniumiza mimi ambaye nilikuwa (Kiongozi wa mazingira shuleni hapo - kipindi changu) na mateso niliyopitia ya kusimamia usafi pamoja na kuotesha miti na yote kukauka.

Najiuliza;
Inamaana wale wakaguzi wa Shule waliokuwa wakipita mara moja kwa kila mwaka au miaka miwili hawapati taarifa za matatizo sugu/hatarishi kwa wanafunzi hasa wa Bweni kama ukosefu wa maji vyoo nk na kuyapeleka kwa waziri husika? Wanafunzi waliosoma Shuleni hapo naamini hawatafurahishwa na habari hizi nzuri kutokana na mateso waliyopitia kwani tatizo hilo lilistahili kutatuliwa miaka ya 1990.

Naamini sio Same Sekondari pekee yenye Changamoto ya maji; zipo shule nyingine zenye changamoto kubwa ambazo hazijapata bahati ya kutembelewa na Viongozi wa juu....

Ningekuwa na nafasi; ningetamani kuzitambua shule tano za Sec kwa kila Wilaya zenye changamoto kubwa; zikifuatiwa na shule tano kwa kila mkoa zinazo ongoza kwa changamoto kubwa.......ningeanzia hapo kuzipatia suluhu..
 
Da nimesoma mwenge advance hapo singida ilikuwa ni mateso hakuna maji. Halafu hapo same kuna ticha nimesoma nae chuo alikuwa ananiambia kuwa hapo maji tizi kumbe kweli aise .
 
Back
Top Bottom