TANZIA: Mwanachama mwenzetu, PakaJimmy amefiwa na mwanae ajali ya basi Arusha

Inaumiza sana.. Mungu awatie na awatie nguvu na kuwapa faraja wafiwa wote!
 
Mkuu PJ pole sana kiongozi. Mungu awae uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Wana Arusha naombeni sana sana tu ubebe huu msiba kama wetu sote. Umoja ni nguvu.
 
Jamani, pole kwa Jimmy na fsmilia kwa ujumla.
Usiache kutuelekeza tuhudhurie mazishi
Arusha wing tunasikitika kutangaza kifo cha mtoto wa member mwenzetu PakaJimmy kilichotokea leo hii kwa ajali ya basi la shule,ni kati ya wale wanafunzi wa Lucky Vincent...

Ni msiba mzito mno mno kwa mzazi yeyote kumpoteza mtoto hasa katika mazingira kama haya ya ghafla,unaagana na mwanao vizuri asubuhi ghafla unasikia amezimika kama mshumaa. Msiba upo nyumbani kwake kwa mromboo, PJ rafiki zako tuko nawe katika hili,

Ni majonzi makubwa mno... Arusha wing tunaungana na wote waliokumbwa na msiba huu mkubwa,Mwenyezi Mungu awatie nguvu,tuko pamoja kwenye hili...

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe...

Baada ya baadhi ya kuomba no ya mchongo tunaomba michango yote ielekezwe kwa 0754288808 jina la usajili ni Pamela Lyamuya... No hii ndo imeteuliwa na Arusha wing kupokea michango

Cc Preta Filipo marejesho LiverpoolFC n.k
 
Back
Top Bottom