Tanzania yaishukuru IMF kwa msaada wa Dola Milioni 455.3 uliotolewa kwa awamu 3, yafanya tathmini ya kupewa awamu ya 4

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,450
8,268
1714739456795.png
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), amefungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (@the_imf ) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ili Tanzania iweze kupata fedha za awamu ya nne kupitia program ya Extended Credit Facility-(ECF), itakayowezesha kuendelea kuchachua na kuimarisha uchumi kupitia sekta za uzalishaji.

Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma kimehusisha timu ya wataalamu kutoka IMF walioongozwa na Bw. Harris Charalambos Tsangarides waliokuja kufanya tathmini na pia kujadili namna ya kuiwezesha Tanzania kupata fedha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha lake la Resilient and Sustainable Trust (RST).

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania inashukuru kwa msaada wa kiasi cha dola za Marekani milioni 455.3 zilizotolewa kwa awamu tatu za kwanza kati ya dola bilioni 1.1 ili kutekeleza miradi inayosaidia kuchochea maendeleo ya wananchi, kukuza uchumi jumuishi na kuiwezesha nchi kuhimili misukosuko ya kiuchumi inayoikabili dunia

“Tunaendelea kufanya kazi na wenzetu wa IMF kupitia programu ya ECF na sasa wamekuja kwenye misheni ya kusaidia Tanzania kuweza kunufaika na dirisha la Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi, programu hiyo ni mwendelezo wa programu za Shirika hilo za kuimarisha uchumi wa nchi wanachama wa Shirika hilo baada ya athari za UVIKO 19.“, alieleza Mhe. Dkt. Nchemba

Dkt. Nchemba amelihakikishia IMF kuwa Tanzania itaendelea kutumia fedha zilizotolewa kulingana na makubaliano yaliyopo na pia amewapongeza kwa uamuzi wa kutembelea vivutio kama Ngorongoro na amewaomba wakipata nafasi waweze kutembelea maeneo mengine kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro na Zanzibar.

Dkt. Nchemba aliishukuru IMF kwa niaba ya Serikali kwa msaada wake na miongozo katika utekelezaji wa program ya ECF kwa kuwa wamefanya jitihada kubwa katika kuhakikisha Tanzania inakidhi vigezo vya kupata fedha kutoka ECF kwa ajili ya kusaidia bajeti na changamoto zinazotokea duniani.
 
Hivi hao wanaotoa hiyo misaada huwa hawaelewi lugha anayoiongea CAG? Haiwezekani usaidie watu wafujaji na wezi
 
Back
Top Bottom