Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,042
- 10,581
Ndugu wanabodi, nchi za Ethiopia, Eritrea, Kenya na sasa Uganda zimevamiwa na baa la nzige (locust) ambao ni wadudu waharibifu sana wa mazao. Kiufupi, nzige wana uwezo wa kula hekta 100 za mazao kwa muda wa saa zisizozidi 3. Uharibifu waliofanya kwenge mazao Kenya na Uganda hausemeki, ni njaa tu mwaka huu.
Uganda na Kenya ni majirani zetu, si ajabu ndani ya wiki hii nzige hao wakavuka mpaka na kufika maeneo ya mpakani kama Mara, Kagera na Kilimanjaro. Mpaka naandika uzi huu sijasikia tahadhari yoyote wala tamko lolote hususani kutoka wizara ya Kilimo na chakula na ofisi ya waziri mkuu (kitengo cha maafa).
Ama tunasubiri nzige wafike ndipo tujiandae? Itakua too late. Tumejiandaaje kama nchi kukabili janga na la nzige?
Nawasilisha
Sent using Jamii Forums mobile app