Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 10,607
- 18,298
Ripoti ya Utafiti ya Taasisi ya Reporters Without Borders (RSF) iliyotolewa Mei 3, 2024 imeonesha #Tanzania imeshika nafasi ya kwanza kati ya Nchi zinazolinda Uhuru wa Vyombo vya Habari upande wa Afrika Mashariki
Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 143 kwa Mwaka 2023 hadi 97 huku #Kenya ikishika nafasi ya 102 kutoka 116 na #Somalia ikiwa nafasi ya 141
Baadhi ya vigezo vilivyotumika ni misingi ya Kisheria, hali ya kiuchumi, hali ya kisiasa, usalama wa Wanahabari
Nchi 10 Bora katika ripoti hiyo ni Norway, Denmark, Sweden, Uholanzi, Finland, Estonia, Ureno, Ireland, Switzerland na Ujerumani