Tamko la Umoja wa Kizazi cha kuhoji Tanzania (UTG) kuhusu suala Ben Saanane kutojulikana alipo

Yani hapa watanzania ndio mnanishangazaga sana! Hivi mpaka hapa mnamwambia nani maneno haya asiyejua kwamba hili ni tukio limefanywa na walio juu ya sheria na mwenendo mzima unaonesha kila kitu katika uhalisia wake?!

Hivi yanayotendeka Burundi mnadhani kuna aliyeyataka? Mnadhani kuna asiyetaka kufuata sheria?! Lakini huwa inafika mahala sheria inawekwa kando ili tatizo liondoke.

Siasa, mdomo, malalamiko hayataondoa hii hali tuliyoifikia sasa.
 
Tuna Watanzania wa ajabu sana, tunafanya mzaha na maisha ya watu??? Kweli? Kumbuka kama Leo yametokea kwa Ben usidhani kuwa Wewe Uko Salama, au Ndugu yako au yoyote yule!!! Haya chekeni Leo, furahini Leo ila kesho yenu nani anaijua????
 
Zingetangazwa Na chombo gani cha hbr kwa haraka km taarifa tu za mawasiliano Yake kutoka ktk kampuni ya simu aliyokua anatumia mpk sasa hazijapatikana sembuse kutoa taarifa za kupotea kwake?
Lakini mkuu hata Uongozi wa juu wa chadema kweli wameshindwa kutoa habari hii mpaka sasa huoni kuna tatizo hapo?
 
Naanza kuona CHILE YA AUGUSTINO Pinochet hapa tz,hivi kama hakuna mkono Wa ajabu kwa mini hata MTANDAO WA SIMU ALIYOKUWA ANATUMIA INASHINDWA KUTOA USHITIKIANO,HAPO NAANZA KUONA KUNA secretly MISSION,AU SIJARIBIWE KAANZA,!!!!!
 
Mungu anawaona mkuu ..mnaficha mtu na kuua wengine alafu mnakuja hapa kusingizia serikali makini kama hiii?hii kitu itawatafuna mno
Unajua tusiwe kama majuha. Tunapotoa hoja zetu tujaribu walau kushirikisha mbongo zetu.
 
Badala ya kuendelea kumpopoa mawe Ben ambaye pengine alishatangulizwa ahera, mjadala ungejikita zaidi kwenye facts zilizotajwa kwenye tamko husika - kwamba taarifa za kutooneka Ben zimeripotiwa polisi "jumatatu ya tarehe 05/12/2016 na kupewa RB namba TBT/RB/8150/2016"; kwamba kuna maiti siaba ziliokotwa mtoni na zikazikwa bila juhudi zozote za kuzitambua; kwamba media houses mbali mbali hazikulipa uzito wa kutosha tukio la kuokotwa maiti husika na kuhoji uzikwaji wake bila utambuzi; kwamba uongozi wa juu chadema haujaonesha msukuomo wa kutosha kutaka kujua alipo mtumishi wao nk nk
 
Lakini mkuu hata Uongozi wa juu wa chadema kweli wameshindwa kutoa habari hii mpaka sasa huoni kuna tatizo hapo?
Tatizo gani labda unaweza kulisema? Ni nani Mwenye dhamani ya kulinda Mali Na RAIA Wa nchi yetu? Maana km MTU kapotea watu Wa kwanza kutoa taarifa ni familia Yake na wamefanya hivyo tayari tena kwa kuripoti ktk vyombo husika. Na mkishatoa taarifa ktk vyombo husika Basi mnaviacha vifanye kz. Sizani km CDM wanayodhama ya utoaji taarifa... Na pia hili swala lazima wakusanye taarifa kamili Na wakija kutoa taarifa waje Na taarifa kamili.
 
Mbona taarifa yao inasema wamemtafuta mahosipatalini magerezani Ata ktk vituo vya Polisi?
Wanatafuta kiki tu wamea
Unajua tusiwe kama majuha. Tunapotoa hoja zetu tujaribu walau kushirikisha mbongo zetu.
Mkuu umenichekesha sana unajua niko kwenye kikao cha mambo flani flani sasa kila nikishika simu wananiuliza mkuu vipi leo mbona kila saa simu....imebidi niwaambie Lancanshire analeta sheeedah
 
Lakini mkuu hata Uongozi wa juu wa chadema kweli wameshindwa kutoa habari hii mpaka sasa huoni kuna tatizo hapo?
Tunakitaka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambayo ndiyo taasisi Ben Saanane aliyokua akiifanyia kazi, kuchukua hatua za kiridhisha dhidi ya suala hili. Zipo taarifa kwamba Chadema wanafuatilia jambo hili na watachukua hatua, lakini sisi kama UTG hatujaridhishwa na namna chama hicho kinavyochelewa kuchukua hatua. Ben amekua mtumishi wa Chadema wa muda mrefu, hivyo hatuoni kama ni sahihi kwa chama hicho kushindwa kutoa tamko lolote hadi leo, ikiwa ni siku 24 sasa tangu apotee.
 
CDM mmesha kosa ya maana ya kufanya!

Mnajiteka wenyewe na kuanza kupima upepo, wananchi
Hili tukio watali chuliaje yaani mnafanya mambo ya kitoto sana ili mradi tu rais aonekane anabana uhuru wa kuogea!

Wananchi sasa tumesha wachoka

Mnacho kifanya ni upupu
Wananchi wa wapi...??
 
Mamlaka husika ni ipi..??? Manake wanaohusika na Ben ni chama chake..!!

Polisi ni mamlaka inayohusika na usalama wa RAIA na mali zake. Serikali pia ni mamlaka. Kupitia uchaguzi wananchi(RAIA) wanatoa mamlaka yao kwa kiongozi wanayemchagua.
 
Ilo la kufukia maiti bila uchunguzi limenistua sana, na ndoivo watz tunafanyiwa na kufukiwa kama mizoga ya punda. Ukisema sana unakua mchochezi #TUNAMTAKA_BEN_AKIWA_HAI
 
Wamezunguka kote, hospitali, vituo vya polisi, magereza na hawakumkuta sasa wanaipa serikali huo muda ili iweje? Je kama amejichimbia gesti na jimama ni kosa la serikali? Au amekula hela ya mtu na wakamfanyizia ni kosa la serikali. Nyie wote ni wapumbavu tu.
 
Wamezunguka kote, hospitali, vituo vya polisi, magereza na hawakumkuta sasa wanaipa serikali huo muda ili iweje? Je kama amejichimbia gesti na jimama ni kosa la serikali? Au amekula hela ya mtu na wakamfanyizia ni kosa la serikali. Nyie wote ni wapumbavu tu.
Tunamtaka Ben-Rabiu akiwa mzima
 
Mwalimu Julius Nyerere aliyosema kuwa _"Binadamu wote ni ndugu, na Afrika ni moja. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuulinda, kuutetea na kuuthamini utu wa binadamu mwingine"._ Kwa maneno hayo ya Nyerere tunataka serikali ichukue hatua ya kumtafuta na kumpata Ndugu BenSaanane akiwa hai, na serikali ichukue hatua za kuridhisha dhidi ya miili ya watanzania wenzetu iliyookotwa hukoBagamoyo.
 
Back
Top Bottom