TAKUKURU Wala rushwa Serikalini ni wengi lakini wao wanahangaika na Mawakala

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
7,126
13,854
MOROGORO: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imebaini mbinu chafu zinazotumiwa na baadhi ya mawakala kuwaibia wateja wao pindi wanapohitaji kufanya miamala ya kuweka fedha kupitia akaunti zao za kibenki.
-
Mwakilishi wa Mkuu wa Takukuru mkoa huo, Christopher Mwakajinga amesema hayo Aprili 23, 2024 alipokuwa akitoa taarifa kwa umma ya utekelezaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia Januari 2024 hadi Machi 2024.
-
Mwakajinga amesema , uchunguzi uliofanywa na Takukuru mkoa uligundua kuwepo mawakala wasio waaminifu wanaopokea fedha toka kwa wateja wanaohitaji huduma ya kuwekewa fedha kwenye akaunti zao za kibenki.

Amesema Takukuru iligundua fedha hizo haziingizwi kwenye akaunti walizopewa na wateja wao na badala yake walikuwa wanatoa stakabadhi batili (Fake)za kieletroniki ili kuwaaminisha wateja wao kuwa wamewawekea fedha katika akaunti zao kitu ambacho hakikuwa kweli.

Amesema kuwa Takukuru mkoa ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni mawakala waliotambuliwa kwa jina la Juma Msuya na mwingine Jamhuri Yohana, na kufikishwa Mahakamani.

Mwakajinga amesema baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro Machi 18, mwaka huu na kufunguliwa kesi ya jinai namba 7110 ya mwaka 2024 na washitakiwa hao walikana shtaka lao na wako nje kwa dhamana.

Kutokana na tukio hilo Takukuru mkoa imetoa onyo kwa wakala yoyote kuwa asijaribu kufanya udanyanyifu wowote kwa lengo la kujipatia fedha kinyume na matakwa ya leseni yake aliyopewa na mamlaka husika kufanya biashara hiyo.

“Takukuru haitasita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani” amesisitiza Mwakajinga.

Imeandaliwa na John Nditi

Una maoni, tuandikie

Habari leo UPDATES


My TAKE


WALA RUSHWA SERIKALINI NI WENGI LAKINI WAO WANAHANGAIKA NA MAWAKALA. KAMA NCHI HATUWEZI KUSONGA MBELE
 
Hao wateja hawapati SMS ya BANK
Mkuu watanzania wengi ni FUNCTIONAL ILLITERATE. Wamesoma ila Elimu haiwasaidii. Wanachokijua ni KULALAMIKA tu.

Unapotuma/kuweka Hela kwa Wakala kuna njia nyingi za kujiridhisha kabla hujaondoka kwa wakala.

Kuna Mazingira mtu akiibiwa, unajua 100% ni uzembe wake na kuchukulia mambo kiwepesi.
 
TAKUKURU ni sikio la kufa. Hii ni taasisi moja ambayo haina FAIDA kwa Taifa letu. Nchi inaweza ku survive kwa kuwa na Polisi tu bila TAKUKURU na tusiathirike

Ila hatuwezi kama nchi tuka survive japo siku moja bila POLISI. Soma pia hapa:


Pamoja na kulalamikiwa sana Polisi bado ni chombo cha muhimu kwa wananchi.
 
Hii ipo kiwizi wizi na ni kazi ya polisi zaidi, labda takukuru walifanya baada ya kuambiwa polisi wamekula rushwa na kutochukua hatua (maelezo haysjitoshelezi) .
 
Back
Top Bottom