Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
Wakuu
Jana RPC wa Mbeya Bwana Ahmed Msangi ambaye pia kama mnamkumbuka alikuwa mtuhumiwa baada ya kutekwa na kuteswa ikiwa ni pamoja na kung'olewa kucha kwa koleo kwa Dr Stephen Ulimboka alitoa kituko cha mwaka ambacho wenye akili wanajua kuwa ni kuendeleza msaada wa kuisaidia ccm.
Nakumbuka hata tukio la kutekwa kwa Dr Ulimboka walitafuta exit na kujitahidi kuihusisha Chadema na tukio hilo ndipo mtego ukaanza kutegwa wa kumhusisha John Mnyika na madai kwamba ndio alitumiwa na Chadema kumshawishi Dr Ulimboka ili madaktari wagome kwa kuwa huduma ni mbovu na vifaa vya tiba vilikuwa haba.
Kituko cha jana cha RPC Msangi tunajua kuwa ni njia ya kuelekea tunako kujua kama ambavyo wamekuwa wanafanya hivyo siku zote. Walianza na ugaidi tukashinda kesi zote mbili, mahakama ikawaonya kuwa kutumia neno ugaidi litafukuza watalii wa nje maana hakuna hata shtaka lenye sura ya ugaidi. Jana RPC mzima anasema manati, visu na T shirt mpya ya chama ni zana za kivita!
Kwa akili ya RPC Msangi ni sawa na kutegemea siku moja kuona uwanja wa taifa manati, bendera na T shirt za Chama zikitumika kama zana za kivita! Kwa akili hiyo hiyo kina mama wenye visu majumbani nao wana zana za kivita za kuchinjia Nyanya na vitunguu, vijana wawinda ndege wenye manati au ukiwa na manati nyumbani ni sawa na kumiliki AK47 maana ni zana za kivita sawa na kumili KIFARU au bunduki.
Baada ya ugaidi kukwama, na hili la manati na kisu kukwama nadhani baadae tutasingiziwa kumiliki KIFARU au kombati tunazo vaa tutaambiwa ni mali ya jeshi na hivyo tuanze kuvaa mashati ya Bahama na suruali za mchelemchele.
Naweza tu kwa Sauti maana jamaa wanaposingizia zana za kivita wanasahau kuwa wauwaji wa ndugu zetu albino hawajakamatwa na waliomuua Mwangosi wako nje na Kamuhanda aliyekuwa RPC na kushuhudia mauwaji hayo kupandishwa cheo achilia mbali yule kada wa ccm aliye mchinja Msafiri Mbwambo kwa mashine ya kukatia mbao na baadae kutoroka akiwa mikononi mwa polisi mwenye silaha ya kivita naye yuko mtaaani ana dunda.