Suleiman S. Suleiman athibitishwa kuwa Mkurugenzi TAA

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,731
Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe amemthibitisha Bwana Suleiman Suleiman kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) kufuatia kuwezesha ukamatwaji wa mama aliyekuwa anasafirisha madawa ya kulevya kuelekea Maau, kiasi cha pipi 68 pamoja na nyara za serikali zilizokuwa zinatoroshwa na Mchina leo.

Kufa kufaana.
 
Safi sana Suleiman chapa kazi ingawa hiyo vita ni ngumu na kali kwa kuwa inahusisha wana, vigogo wa CCM
 
Huyu jamaa amesota miaka mingi akiwa anaigiza nafasi ya ukurugenzi wa mamlaka hii.
Hakika ni haki yake sasa kuwa confirmed.
 
Tutegemee dawa za kulevya na nyaraka za serikali zikiendelea kukamatwa isiishie leo tu,.
 
Tutegemee dawa za kulevya na nyaraka za serikali zikiendelea kukamatwa isiishie leo tu,.
Mimi ningekuma yeye ningekuwa najikumbusha kila iwapo asubuhi, kwamba cheo changu kimetokana na matukio fulani, kwahiyo ningekomalia hukohuko.
 
Mmmh! Pakajimy tumuombee tu kwa Mungu asibadilike!
Coz viongozi wengi huanza vizuri tu!
 
apunguze kuchomeka watoto wa vigogo kwa kuwapa ajira kinyemela bila kupitia utumishi...pia atoe wababaishaji ndan ya mamlaka,wazee wote waliopewa vyeo kiupendeleo lkn ufanisi wao 0 wapigwe chini..

watu wapandishwe vyeo kwa kuzingatia sifa sio kwa kujuana.hata nafasi za kusoma zisitolewe kwa kuangalia sura..
anyway hongera zake kwa kuwa anapiga kaz lkn watendaji weng wanamuangusha.
 
Hiyo Mamlaka kuna chalii yangu aliamua kuacha na kwenda kufungua kampuni yake,na sasa maisha yanasonga.
Imejaa kujuana sana,watu wanapeana vyeo na kupandishana madaraja kwa kujuana,kama huna mtu ndani ya mfumo wa Mamlaka andika umeumia,walimuweka dogo bench,wanakuja watu wasio ajiliwa ila ni ajira za mkataba,wanapewa safari za nje na masemina kibao...pamejaa watoto wa vigogo wa mamlaka walio na kazi za mkataba.
Wanabaniana mpaka posho na kupandishiana mishahara,wakubwa wanashinda nje ya nchi kutwa kucha,wengine hakuna.
Niliumia sana dogo kipaji chake kudhalauliwa,wapo watu humo na degree za Kampala University ya Gongo la Mboto kisa wanajuana na wakubwa ndani ya mamlaka basi ni tabu,wakamnyima dogo kujiendeleza,Huyo Suleiman kama amepewa ”meno“ kamili na Mwakyembe,basi aisafishe TAA,iwe ya kiuweledi,athamini wafanyakazi kwa weledi,malipo na mazingira mazuri ya kazi....iwe yenye sura ya kimataifa...wasiogope vijana....iliniuma sana.bwana mdogo kuacha kisa fitna,na kutokuwa na ”Godfather“
 
Back
Top Bottom