Nia ya Serikali ilikuwa nzuri sana kujenga Stendi ya Nyamhongolo ili iweze kuwahudumia wasafiri wote wanaoelekea upande wa Musoma, Sirari/Tarime, Bariadi, Maswa na maeneo yote ya upande huo. Serikali imeweka huduma zote zikiwapo Mabenki, Maduka, mahoteli, vyoo, ghorofa yenye vyumba vya kulala wageni n.k.
Leo nimetembelea katika Stendi hiyo niliyoyakuta yamenishangaza sana. Karibu asilimia 50 ya maduka yamefungwa kwa kukosa wateja. Stendi ina watu wachache sana utadhani uko stendi ya Misungwi.
Nilipowauliza kulikoni wakanieleza kuwa Serikali ingejenga stendi moja kubwa inayowahudumia wasafiri wote katika Jiji hilo na wazo la kujenga stendi mbili ya Nyegezi na Nyamhongolo halikuwa wazo jema. Kwa Mwanza Stendi ya Nyegezi ndiyo stendi inayojaza wasafiri kwa sababu wasafiri wote wanaoelekea njia ya Dar, Morogoro, Dodoma wanalala maeneo ya jirani na stendi na ni wengi hivyo stendi hiyo ina watu wengi kuliko stendi ya Nyamhongolo.
Ni vema Serikali ya Mkoa wa Mwanza ikawa na mpango wa kuhakikisha kuwa stendi zote zinapata mabus na abiria kwa kuhakikisha kuwa mabus mengine yanayoelekea Dar, Morogoro, Dodoma yanalala stendi ya Nyamhongolo vinginevyo stendi ya Nyamhongolo itaelekea kuwa mahame na wengi wa wafanyabiashara tayari wamekwishaihama.