Soko la Madini ya Dhahabu la Chunya Laongoza Tanzania Kuingizia Serikali Mapato.Geita na Kahama Zafuatia.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
44,488
51,308
Kwa mujibu wa data kutoka Tume ya Madini na Wizara ya Madini zilizowasilishwa Bungeni 2024 zimeonesha kwamba Soko la Madini ya Dhahabu la Chunya-Mbeya limechangia mabilioni kwenye Mapato ya Nchi na kuyapita masoko ya Mikoa Maarufu Kwa Madini ya Geita,Kahama na Mara.

Ikumbukwe kwamba Soko la Madini la Chunya linaendeshwa zaidi na wachimbaji wadogo ambapo Madini yenye thamani ya Zaid ya Bilioni 360 yaliuzwa na kuchangia Mapato ya Serikali Kwa zaidi ya Bilioni 25 za marhaba na ada za ukaguzi.
Screenshot_20240501-114636.jpg


Masoko mengine ambayo yanafanya vizuri ni

1.Chunya
2.Geita
3.Kahama
4.Mbogwe
5.Mara
6.Shinyanga
7.Songwe

My Take
Mbeya imejaaliwa Kila aina ya utajiri
Screenshot_20240503-111357.jpg
Screenshot_20240503-111853.jpg
Screenshot_20240503-111333.jpg
 
Hakuna faida yeyote tunayopata na hayo makusanyo.maana pesa zote zitapelekwa Dar es salaam au Zanzibar
Kuna haja ya kubadili kiasi sheria za madini Ili walau 5% ya pesa zote zibakie kwenye Halmashauri husika yanakotokea.

Inauma Sana Madini yanataoka.kwenu harafu hela Zinaenda Dodoma,Dar na Arusha.

Zanzibar pesa haiendi maana Madini sio jambo la Muungano
 
Nimekuwa naandika mara nyingi sana Kwa Serikali kuweka mgawanyo mzuri wa Rasilimali.Sio sawa Rasilimali za Mikoani kujenga Dar, Dodoma na Arusha pekee.
Choice kwa jinsi usimamizi wa rasilimali fedha ulivyombovu hata pesa asilimia Fulani ikabaki bado zitapigwa na watumishi wa halmashauri wakiongozwa na mkurugenzi.
 
Madini yanayoenda Kenya na Rwanda ukiyaona lazima umlilie mama tz,
WaTanzania wengi hawaju dhahabu inayo toka Kerende, Marera na Nyabichune ambayo inasoma hadi 20 grams per tani 1 huko wilayani Tarime ambapo ni kilometa 10 kutoka mpaka wa Kenya mazee....
Ebu jiulize dhahabu inayo patikana Mbogwe, Nyalugusu, Nyaluyeye, Katoro, Nyamakwenke, Segese, na kahama kwa ujumla na inasoma karibu 10 grams kwa tani 1.....
Aiseeeee....
Ebu ngoja ninyamaze tu
 
Back
Top Bottom