Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Bossless

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
1,381
2,929
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.

Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.

Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.

Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.

basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..

Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.

Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.

Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.

Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!

Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.

Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.

Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .

Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.


Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .

Itaendelea...........

Muendelezo bonyea link hizi.

Sehemu ya nne
Sehemu ya tano

Sehemu ya sita
Sehemu ya saba

Sehemu ya nane
Sehemu ya tisa

Sehemu ya kumi
Sehemu ya kumi na moja





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom