Dkt. Gwajima D
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 550
- 3,619
Tunaelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia hapo Mei 15, 2024 ambapo, nchi yetu tutaungana na zingine duniani kuadhimisha.
Familia ni chanzo cha jamii yetu hivyo, ni kiungo muhimu sana kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Malezi bora kwa watoto ndani ya familia ni chanzo cha jamii iliyo njema na yenye Baraka.
Lengo la maadhimisho ni kutathmini nafasi ya familia katika ustawi na maendeleo yao na mchango wao kwa taifa.
Mwaka 2024 maadhimisho yatafanyika kimikoa kwa kugusa ngazi ya jamii yaani Vijiji, Mitaa na Kata.
Changamoto za mifarakano katika familia imesababisha malezi duni na uangalizi hafifu wa watoto na matokeo hasi kwenye maendeleo na ustawi wa watoto mfano wa kike kuanza ngono katika umri mdogo na kupata mimba za utotoni. Wa kiume nao hujiingiza kwenye tabia hatarishi na kushindwa kutimiza ndoto zao.
Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 jumla ya mashauri 14,600 ya kifamilia yaliripotiwa yakiwemo ya migogoro ya ndoa 5,306 (36%), migogoro ya matunzo ya Watoto 5,944 (41%) na ya matunzo ya watoto wa nje ya ndoa 3,350 (23%).
Aidha, kati ya hayo, jumla mashauri 3,411 yalifikishwa ustawi wa jamii na kufanyiwa kazi ambapo, 1,642 (48%) yalipatiwa ufumbuzi na 443 yanaendelea kufanyiwa kazi. Yaliyopata rufaa kwenda mahakamani ni 921 na yaliyosalia 405 yalikabidhiwa kwenye mabaraza ya Kata na Mabaraza ya Jumuiya.
Hakika Maafisa Ustawi wa Jamii wameendelea kufanya kazi kubwa kuhusu utengamao wa familia. TUWAPONGEZE 🙋
Wito kwa viongozi wa Dini kutumia vipindi vya ibada kutoa ujumbe mahsusi kuhusu umuhimu wa malezi bora ya watoto katika kujenga familia imara na Taifa imara la Tanzania.
Wito kwa Wakuu wa Mikoa kupitia watendaji kuratibu elimu ya malezi chanya kwa watoto na wazazi au walezi ngazi za Jamii.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni "Tukubali Tofauti Zetu kwenye Familia; Kuimarisha Malezi ya Watoto."
.... kwa taarifa zaidi tafadhali karibu utembelee kurasa mbalimbali za wizara ya maendeleoyajamii online
Heri ya Siku ya Familia, jiandae, adhimisha kwa furaha wewe na familia yako 🙋🇹🇿