SoC03 Siku moja nitamwambia Rais...

Stories of Change - 2023 Competition

Sweya Makungu

JF-Expert Member
Jun 11, 2023
481
560
Siku moja nitamwambia Rais.

Anaandika Mwl. Makungu m.s
0743781910

Anayecheka kupita kiasi na anayelia kupita kiasi wote hutoa machozi...

Kwahiyo uamuzi ni wake,
" Anazika au Anasafirisha" ..

Mhe. Rais nakusalimia kwa jina imani, "Philosophy (Love of Wisdom).
Natamani siku nikikuona nikukumbushe mambo machache yafuatayo..

- Licha ya Absalomu mtoto kipenzi wa mfalme Daudi kuanzisha vita ya kumpindua baba yake mpk akaikimbia ikulu na yeye kulala na wake 10 (masuria) wa baba yake , Bado mfalme Daudi aliagiza Absalomu asiuwawe ( Anampenda kupita kiasi ) .. Aliyemuua Absalomu ni kamanda wa jeshi la mfalme Daudi kwa kulipinga agizo la mfalme kwa maslahi ya nchi.

Hii maana yake ni nini? Mhe. Rais , Pengine unalipenda Sana taifa na huna kisasi na mtu yoyote lkn wasaidizi wako wanaweza wakatekeleza mabaya kwa uwazi au kwa usiri kinyume na maagizo yako ili kukulipia wewe kisasi kwa maslahi yao au kwa maslahi ya nchi . Uamuzi ni wako kuwaacha au kuliombolezea taifa kwa uchungu km mfalme Daudi ..

- Mfalme Suleiman hakuizungukia dunia ili kwenda kuistaajabia dunia na uzuri wake . Bali wafalme wa dunia waliizungukia Israel ili kwenda kuustaajabia ufalme wa mfalme Suleiman wenye hekima kupita kiasi na utajiri wenye ukwasi .
Hii maana yake nini? Mhe rais ifanye Tanzania kuwa kimbilio la wafalme wa dunia kujifunza maarifa ya kipekee ya kisiasa kiteknolojia na kiuchumi na siyo sisi kuwakimbilia wao..

-Mfalme Farao wa misri alimkabidhi Yusufu (bwana ndoto) mamlaka amri na madaraka yote juu ya nchi . Kwa neno la Yusufu kila kitu ktk nchi kilitekeleza majukumu yake na chochote kilichokatazwa kwa neno la Yusufu kilikoma .. Mfalme Farao hakuingilia wala hakujihusisha na kitu chochote kile tena juu ya kuendesha nchi . Alimkabidhi Yusufu mamlaka yote isipokuwa kiti chake tu cha enzi.. na taifa la misri lilipata mafanikio makubwa Sana nyakati hizo..
Hii maana yake nini?

Si kwamba Farao alikuwa ni kiongozi mjinga , bali alitambua uwezo wa mtu anayemzidi yeye uwezo ndani ya nchi na akampa mamlaka ya kumsaidia kuiendesha nchi. Kwahiyo wakati mwingine mhe rais unapounda serikali yako usiangalie majina ya vimemo wala uteuzi wa kulipana fadhila , angalia watu wenye uwezo mkubwa hata Kama wanakuzidi wewe uwezo . Ili ulete Mapinduzi na mabadiliko makubwa ktk taifa na vizazi vyote vitakukumbuka Kama Mao Tsetung wa China au Mahatma Ghandi wa India ..

- Kilichomuua Yesu siyo ndoto yake wala siyo ubaya wake . Kilichomuua Yesu ni ndoto ya baba yake na wema wake wa kutaka kuupindua ufalme mbaya akiwa ndani ya eneo la utawala la ufalme wenyewe . Ufalme mbaya ulipoasi kule mbinguni ulipigwa vibaya na ukatupwa duniani ukaja kuanzisha ufalme wake mpya duniani .

Kwa hiyo Yesu alipokuja duniani na wao wakataka kumuonesha kuwa hapa ulipokanyaga umeingilia ufalme wetu usiokuhusu (Kama hauamini kasome maagizo ambayo shetani alikuwa anampa Yesu kule nyikani kwa siku 40)..
Hii maana yake nini? Ndoto ya baba yako ni ndoto za waasisi wa mataifa ya Afrika kutaka kuiunganisha Afrika kuwa taifa moja lenye nguvu kiuchumi kisiasa na kijeshi. Na wakoloni ndiyo wafalme wabaya. Kwahiyo utakapotaka kuitimiza hii ndoto kuleta Mapinduzi ya Afrika utakuwa umegusa maslahi ya watu wabaya kwny ufalme wao . Ni heri ukutane na shetani Lucifer asiye na rangi kuliko kukutana na shetani mweupe mwenye roho nyeusi... (Maneno haya nilimwambia Magufuli July 2019 ktk andiko langu)..

- Mordekai (mtu wa Mungu muisrael) alipompenyeza mpwa wake kuwa miongoni mwa mabinti bikra watakaolala na mfalme Ahasuelo wa nchi ya Uajemi (nchi ya ugenini utumwani- kwa Sasa inaitwa Iran ) bila watu kugundua kuwa siyo wa taifa hilo , alikuwa akiongozwa na maono kuwa mpwa wake ndiye atachaguliwa kuwa malkia wa taifa.. Alifanya hivyo kwa maslahi ya mbeleni ya taifa la Israel ambalo wakati huo lilikuwa utumwani. Binti huyu (Ester) baadae ndiye alikuja kuwa mkombozi wa taifa kule utumwani maana tayari alikuwa ameushikilia moyo wa mfalme..
Hii maana yake nin? Katika nyanja za kimahusiano ya kimataifa sisi km taifa maono yetu ni yapi?
Je mabalozi tunaowatuma nje kuiwakilisha nchi ni watu wenye ushawishi mkubwa kiasi gani kwa tawala za huko kwa maslahi ya taifa letu? Je wameyabeba maono na dira za taifa letu huko wanakoenda kwa maslahi ya mbele ya taifa? Unapoteua mabalozi teua vichwa . Maana wanawakilisha aina ya akili iliyopo nchini..

-Ufalme wa mfalme sauli wa Israel na ufalme wa mfalme Nebukardreza wa Babeli - taifa ambalo lilikuwa na bustani zinazoelea angani ( kwa Sasa linaitwa Irak) , haukuanguka kwa sbb walikuwa ni wafalme dhaifu au wenye jeshi dhaifu . Bali Walianguka kwa sbb ya kujiinua na kumkufuru Mungu ..
hii maana yake nn? Ulipoingia madarakani kuna watumishi wa Mungu walikuonya "kamwe usije ukajifananisha na Mungu au kuwaruhusu watu kukufananisha na Mungu " . Kemea wale wajinga walioandaa mabango na kukufananisha ww na " Utatu Mtakatifu"..
Mhe rais wengi tunatenda dhambi ni wazinzi na walevi , lkn nakwambia hakuna dhambi mbaya km kujifananisha na Mungu..

- Mfalme Daudi alipozini na mke wa mtu (mke wa Huria) na kuhakikisha mume wake ( Huria) amefia vitani ili yeye amuoe yule mwanamke ,aendelee kumfaidi kwa uzuri wake, Mungu alimpiga Daudi.. Kwahiyo mhe rais kamwe usicheke kwa sababu umewaumiza watu . Cheka kwa sababu watu wamejaribu kukuumiza lkn wameshindwa .. Maana kicheko chako cha ubaya kikizidi Sana mwisho wake utatoa machozi ..

- Mfalme Suleiman siku moja alihuzunika Sana na akaandika aya moja ktk kitabu cha muhubiri akisikitika baada ya kuitazama Israel na fahari yote aliyoijenga . Akasema " tazama jinsi ilivyo ubatili , mfalme anajuaje km sabaha wake ( mrithi wa ufalme wake) atakayefuata atakuwa na akili ya kuyaendeleza mazuri yote aliyoyaanzisha yeye au atakuwa mpumbavu wa kulibomoa taifa na kufanya yoote yaliyoanzishwa kuwa ni kama ubatili tu na kujilisha upepo?

Hii maana yake nini? Mhe. Rais weka dira ya taifa itakayofanya mrithi wa kiti chako kuendeleza mazuri yote yatakayokuwa kwenye dira ya taifa na siyo mtazamo wake yeye binafsi .. Maana huwezi kujua km sabaha wako atakupenda au atakuchukia .. vinginevyo mazuri yote uliyoyaanzisha yatakuwa ni sawa na ubatili mtupu na kujilisha upepo..

Mhe. Rais uamuzi ni wa kwetu .
Je! Tunazika au Tunasafirisha?

Mwl. Makungu m.s
0743781910
 
Kwanini usinukuu simulizi za mababu zetu wabantu...Unanukuu simulizi za wayahudi????? Au wewe sio mbantu
Bila shaka nimejitahidi kunukuu maarifa niliyonayo ili kujenga picha ya ninachoshauri. Hadithi za wabantu mababu hazipo ktk mfumo rasmi . Pengine tungezipata ktk mfumo wa elimu na dini ningeweza kuzisemea.. ningekuwa pia na maarifa ya Waarabu ningeweza pia kutoa mifano . Kikubwa ni ushauri wa kujenga.
 
Bila shaka nimejitahidi kunukuu maarifa niliyonayo ili kujenga picha ya ninachoshauri. Hadithi za wabantu mababu hazipo ktk mfumo rasmi . Pengine tungezipata ktk mfumo wa elimu na dini ningeweza kuzisemea.. ningekuwa pia na maarifa ya Waarabu ningeweza pia kutoa mifano . Kikubwa ni ushauri wa kujenga.
Umekosa uzalendo kwa kushindwa kunukuu nukuu za kibanru na kukimbilia za wageni...Dini zililetwa na wakoloni ni aibu kutotumia mifano ya asili yako...Waafrika bado hamjitambui....Ushauri wangu ni kwamba jaribu kuenzi asili yako ya kibantu
 
Back
Top Bottom