Siku moja kabla ya kifo chake Mafisango aliteketeza milioni 10 kwa starehe,cha ajabu hakuwa amejenga kwao

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,267
36,623
Marehemu asemwi vibaya ila huyu mwamba alinifurahisha sana.
Mmoja kati ya viungo bora kabisa wa enzi zake,siku moja kabla ya kifo chake,Isnsil Aden Rage akimpatia milioni zaidi ya kumi kama sehemu ya ada ya usajili wake.

Mafisango akaita marafiki zake wakaitumbua aswaa,ilikuwa ni kuhama bar tu mara mikocheni mara masaki mara kinondoni,mara paaa ajaki hii hapa

Tukaenda msibani aisee ni uswazi kama Tandale hakuna hata pa kufunga hema.

Naandika haya nikiwa bujumbura baada ya kuonyeshwa mjengo wa yule mzee wetu Saidoo,ni mjengo hata huko Tanzania hakuna mchezaji au celebrity anaweza kuumiliki.
 
Walikuja kukuomba sehemu ya kuweka msiba?
 
Kwa hiyo milioni kumi ndio angejenga hekalu kama la Saido? Wala sishangai hayo ndio maisha ya Wakongo wengi,hata ukienda Kinshasa au mji wowote mkubwa wa Kongo ukikutana na Mkongo njiani au sehemu ya starehe jinsi alivyovaa na starehe afanyayo halafu ukienda kuona anapoishi ni mbingu na ardhi.
 
"pesa yake matumizi, hakuna elfu 10 iliyoandikwa ni ya mfuko wa cement wala tofali"😂

"Hakujenga baba kipindi cement mfuko sh 2, kiwanja unajikatia, nijenge mie cement 18000" 😂😂

"Tumia pesa ikuzoee" 😂

"Dunia tunaoita, sijengi, nitajengewa nyumba yangu ya milele nandugu jamaa na marafiki "

🤣😂😂
 
Naandika haya nikiwa bujumbura baada ya kuonyeshwa mjengo wa yule mzee wetu Saidoo,ni mjengo hata huko Tanzania hakuna mchezaji au celebrity anaweza kuumiliki.
Saidi Ntibazonkiza amecheza ligi ya Uholanzi (Eredivisie) kwa misimu minne yaani 2006 -2009 akiwa na Nijmegen Eendracht Combinatie (NEC), Pia amewahi kucheza ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) na timu ya Caen msimu mmoja 2015/16 kabla ya hapo alikuwa ligi kuu ya Uturuki (Super Lig) msimu wa 2014/15 na Akhisarspor Kulübü.

Jaribu kuangalia vizuri hii career yake utalinganisha na mchezaji aliyekuwa analipwa Tshs. 30M as a signing fee miaka hiyo? Mishahara mikubwa mikubwa kidogo ililetwa na Yusuf Manji tena miaka chini ya 2012 Simba na Yanga Tshs. 5M ulikuwa mshahara mkubwa sana. Hapo unampa mchezaji na kagari ka Tshs. 20M plus signing fee Tshs. 25M. Mshahara kwa mwezi Tshs. 3M.
 
Back
Top Bottom