Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,770
- 10,660
Wakuu, sote tumeshuhudia wiki za usajili wa vishindo ambao umetikisa jiji kama sio nchi kwa ujumla wake. Naweza kusema matukio makubwa ya kisiasa yameweza kutulizwa na muingiliano wa mambo ya usajili wa hivi vilabu viwili.
Tatizo linakuja upande wa marketing, sielewi wamepangaje hesabu zao. Lakini kwa timu ya Yanga ambayo ndiyo imeongoza kwa vibe la nguvu kutokana na kusajili kwa wingi, huku wakiratibu matukio ya kupokea wachezaji kwa umakini mkubwa, walitarajiwa kutumia msimu huu KUPIGA PESA. How? Kama ilivyokuwa kauli ya HAKIKISHA HUISHIWI BANDO kwenye Instagram tulitarajia pia waseme USIKOSE JEZI YA MUKOKO AIRPORT!!
Ni kwa nini kampeni ya mapokezi ya mastaa hawa haikuenda na biashara ya jezi? Ni aibu mpaka sasa jezi rasmi hazijatambulishwa ili wadau ambo damu zineachemka kweli kweli wazichangamkie. Basi sawa, wakati wa mapokezi klabu haikuwa tayari, vipi wakati huu wa kuelekea kikeke cha wiki ya mwananchi, kwa nini mpaka sasa hakuna jezi? Ingekuwa vema kwamba wapenzi wanahamasishwa kuvaa jezi mpya na kuujaza uwanja ili kuupamba, lakini akili zimelenga kuionyesha Simba kwamba wao wana wakazi uwanja wengi!! Hivi ni nani ameturoga?
Yaani mpaka sasa ilitarajiwa mitaani kuwe na mashindano ya kuvaa jezi mpya, lakini hatulioni hilo!! Tunasubiri mpaka pale mzuka wa wapenzi upoe, ndipo tuanzishe kampeni maalumu ya VAA JEZI. Hakika hapa Yanga imefeli sana. Kwa mtindo huu msolla ataendelwa kutangaza kuchangia bakuli tu badala ya kuhamasisha wadau wanunue products kuiunga mkono timu!?
NANI KATUROGA?