Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,626
- 32,042
Katika aliyofanya Rais SSH tangu achukue madaraka ni 'kuacha watu waonge' .
Rais alisema watu wakiongea viongozi wanaelewa nini kinaongelewa.
Katika kufungua uhuru wa maoni/habari uliofinyangwa miaka sita amefanya vizuri.
Kwa hatua hiyo Rais anapata faida ya ziada ya kuelewa kilichopo akilini na miyooni mwa jamii anayoisimamia kama kiongozi mkuu.
Mwezi April una matukio kadhaa yanayohitaji tuyaangalie kwa jicho pana kuyaelewa
Mkutano Mkuu wa CCM:
Uliandaliwa kumchagua makamu Tanzania Bara baada ya mzee Mangula kung'atuka. Komredi Kinana alichukua nafasi akitoka kwenye maumivu makali ya awamu ya tano ya kudhalilishwa illiyoshindwa kujali , kuthamini au kuheshimu kazi za Wazee na wanachama
Wazee wengi sana wa Chama walihudhuria mkutano wakiwa na furaha ikieleza jambo.
Kubwa ni kwa katibu mkuu wa zamani Yusuf Makamba kutema nyongo akisema ''.... wasamehe wewe ndio bosi wao sasa''
Makamba anamwambia Kinana awasamehe 'Timu JPM' iliyoongoza kwa mkono wa chuma
Komredi Kinana akishukuru wajumbe aliwaasa viongozi kutokuwa na majigambo, kuwa wanyenyekevu na kuwa watumishi. Ujumbe ulilenga JPM na timu yake ''inner circle''
Mkutano wa TCD:
Ni mkutano wa wadau wa Demokrasia. Katika yaliyojiri ni kusemwa wazi kwa utawala wa JPM, likifanywa na viongozi wa siasa, dini. wazee Wastaafu na Wasomi
Ni ujumbe ulioashiria nchi haikuwa katika mstakabali mzuri miaka michache iliyopita.
Ufunguzi wa Chuo cha CCM:
Tukio hilo limeambatana na uzinduzi wa vitabu vilivyomhusu Mwalimu Nyerere.
Washiriki walimweleza Mwalimu Nyerere kadri walivyomfahamu
Tukio moja ambalo wengi hawakuliona kwa urahisi au kulielewa kama lilivyotokea ni la mchangia mada mwandishi Aboubakar Lyongo aliyeongea kwa niaba ya vijana
Katika kuchangia Bw Lyongo alizungumzia udini, ukabila na ukanda akisema miaka ya karibuni tumerudi nyuma. Hakuna shaka Bw Lyongo alizunguzia utawala wa JPM
Mtoto wa Mwalimu Nyerere Bwa Makongoro (RC Manyara) alieleza kwamba Nyerere alipendwa kwasababu ya ''Ubinadamu'' .
Reactions (mwitikio) wa Wananchi ni makofi mazito ya dhati ya kukubaliana na Makongoro. Hapa palikuwa na ujumbe pia Katika yaliyolalamikiwa utawala wa JPM ni haki za binadamu
Rais SSH alipo ongea alipita kule kule alikoanzia Bw Lyongo tena akimnukuu.
Rais alisema tuna kazi ya kufanya kufuta mambo ya udini, ukanda na ukabila yaliyojitokeza miaka ya karibuni. JPM ananyooshewa vidole na aliyekuwa Msaidizi wake.
Je, bado kuna shaka ya tuhuma Udini, Ukanda na Ukabila?
Ukichukua matukio matatu ya mwezi huu, hadhra na watu walioongelea hakuna shaka miaka awamu ya tano ilipanda mbegu mbaya nchini
Jamii inaonyesha kutoridhishwana Taifa lilipopitia katika utawala wa Rais JPM kijamii
Serikali ya JPM imeonyooshewa vidole siyo na Wapinzani ambao huonekana kama 'wasema hovyo'' bali Wanachama wa CCM, viongozi wa Dini, Wazee Wastaafu na Wasomi
Kazi ya kuturudisha katika mstari si rahisi kwani 'mbegu' ilishapandwa na kuchanua.
Ingawa mbegu bado ni changa kuiondoa itachukua muda na jitihada za dhati kwetu sote
Rais SSH aungwe mkono, tuondoe na kuwazomea waliotaka kutupoteza
Tukemee yasijirudie tena kama yale ya 'kueleza kanda fulani itusubiri''
Hatuwezi kuponya majeraha kwa kukaa kimya au kusingizia mtu.
Jambo muhimu ni kuweka rekodi sawa na zisemwe wazi ili tujue ni akina nani , kwa njia gani wakifanya nini na kusaidiwa na nani walitaka taifa letu ligawanyike kwa misingi mibaya
Tusemezane