Shukrani kwa faraja kwenye Msiba wa Mama yetu Sophia Gwajima

Dkt. Gwajima D

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
577
3,822
Familia ya Advocate Gwajima, tunawashukuru Watanzania Wote kwa upendo na faraja kipindi chote cha kuuguza hadi msiba wa mama mzazi wa Advocate Gwajima (mume wangu) aliyejulikana kama SOPHIA GWAJIMA (mama mkwe wangu) na aliyezaliwa mwaka 1945 na kufariki tarehe 27 Machi, 2024 katika Hospitali ya Kitengule, iliyoko Tegeta, Dar Salaam na kuzikwa nyumbani kwake Kisesa, Magu, Mwanza tarehe 30 Machi, 2024.

Haikuwa rahisi kubeba msiba huu peke yetu bali imewezekana kutokana na upendo wa watanzania jambo ambalo limetupa heshima na faraja kiasi kwamba, hatuna la kusema zaidi ya AHSANTENI.

Shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuguswa na msiba huu na kumtuma mwakilishi wake aungane nasi katika safari ya mwisho ya mama yetu Sophia Gwajima.

Shukrani kwa Rais wa JMT Awamu ya 4 Mhe Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliongoza waombolezaji kutoa Heshima za mwisho tarehe 29 Machi, 2024 nyumbani kwetu Salasala akiambatana na mke wake Mhe. Mama Salma Kikwete (Mb).

Shukrani kwa Askofu Philipo Mafuja Magwano -AICT Dayosisi ya Pwani kwa ibada ya Heshima za mwisho tarehe 29 Machi, 2024. Shukrani kwa Shekh Mkuu na Mufti wa Tanzania Shekh Abubakar Zuberi kwa ushirikiano na dua katika msiba huu.

Shukrani kwa Mhe. Mwanaid Ally Khamis (Mb), Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalaghe pamoja na Wataalamu wote kwa ujumla, Vyuo na Taasisi zote chini ya wizara hii kwa upendo na ushirikiano wao.

Shukrani kwa Waheshimiwa Mawaziri wenzangu wote kwa upendo, umoja na ushirikiano.

Shukrani kwa Prof. Janabi, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wataalamu wote wa Hospitali ya Mloganzila kwa huduma na ushirikiano.

Shukrani kwa Dkt. Sebastian Kitengule Ganyaka (MD. MMed), Mkurugenzi wa Hospitali ya Kitengule iliyopo Tegeta, Dar es Salaam na mahsusi shukrani kwa Dkt. Jovina Lawrence Nkya (MD, MMed, Internal Medicine) kwa huduma na upendo mkubwa yeye na wataalamu wenzake kipindi cha kumuuguza Bi. Sophia Gwajima.

Siyo rahisi kuwataja wote ambao tungependa kuwashukuru bali kwa uchache; majirani zetu wote, ndugu, jamaa na marafiki, Mama Sophia Simba (Waziri Mstaafu), Uongozi wa Benki za Azania na Benki ya NMB, Uongozi wa UWT, Kamati ya Wanawake ya Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia na kwa Watoto, Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, Baraza la Ushauri la Wazee Taifa, SMAUJATA, FAGDI, SAWATA, MaleziNetwork, Chuo cha City College Mwanza Campus na rafiki zetu wote wakiwemo online duniani kote na kila mmoja.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa Neema ya tangu mwaka 2012 ya kuishi pamoja na Mzee Stiven Gwajima (Baba mzazi wa Advocate Gwajima aliyeitwa na Mungu mwaka 2019) na kumwacha mke wake Sophia Gwajima ambaye naye ameitwa na Mungu 27 Machi, 2024.

HAKIKA, maisha pamoja na wazazi hadi kuwazika ni Neema Adimu ya Mungu, tunamshukuru kwa Neema hii

Tumeuona mkono wa Mungu na Baraka za Mungu kupitia maisha yetu pamoja na wazee hawa. Tutaendeleza mema yote na kuzisemea heri za kuishi na wazee. Hakika, wazee ni tunu na uzee na kuzeeka hakukwepeki, ni Neema. Tukiwapenda na kuwathamini Wazee, nasi tutathaminiwa maana tumemuomba Mungu kila siku, atupe neema ya kuishi miaka mingi.

AHSANTENI WOTE, MBARIKIWE.

RIP Sophia Gwajima (Mayù) (Mama Mkwe), AHSANTE 🤲🙏🏽 kuniachia Mume mwema na Baba Mwema wa Familia). Tutakukumbuka Daima
2 Timotheo 4;7
IMG-20240331-WA0011.jpg
IMG-20240402-WA0006.jpg
IMG-20240402-WA0012.jpg
IMG-20240331-WA0007.jpg
IMG-20240331-WA0066.jpg
IMG-20240331-WA0065.jpg
IMG-20240331-WA0067.jpg
IMG-20240401-WA0065.jpg
IMG-20240402-WA0017.jpg
IMG-20240402-WA0020.jpg
IMG-20240402-WA0007.jpg
IMG-20240402-WA0011.jpg
IMG-20240331-WA0129.jpg
IMG-20240402-WA0014.jpg
IMG-20240331-WA0008.jpg
IMG-20240331-WA0014.jpg
IMG-20240331-WA0036.jpg

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Attachments

  • IMG-20240402-WA0012.jpg
    IMG-20240402-WA0012.jpg
    88.8 KB · Views: 6
  • IMG-20240402-WA0028.jpg
    IMG-20240402-WA0028.jpg
    45.4 KB · Views: 5
Familia ya Advocate Gwajima, tunawashukuru Watanzania Wote kwa upendo na faraja kipindi chote cha kuuguza hadi msiba wa mama mzazi wa Advocate Gwajima (mume wangu) aliyejulikana kama SOPHIA GWAJIMA (mama mkwe wangu) aliyefariki tarehe 27 Machi, 2024 katika Hospitali ya Kitengule, iliyoko Tegeta, Dar Salaam na kuzikwa nyumbani kwake Kisesa, Magu, Mwanza tarehe 30 Machi, 2024.

Haikuwa rahisi kubeba msiba huu peke yetu bali imewezekana kutokana na upendo wa watanzania jambo ambalo limetupa heshima na faraja kiasi kwamba, hatuna la kusema zaidi ya AHSANTENI.

Shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuguswa na msiba huu na kumtuma mwakilishi wake aungane nasi katika safari ya mwisho ya mama yetu Sophia Gwajima.

Shukrani kwa Rais wa JMT Awamu ya 4 Mhe Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliongoza waombolezaji kutoa Heshima za mwisho tarehe 29 Machi, 2024 nyumbani kwetu Salasala akiambatana na mke wake Mhe. Mama Salma Kikwete (Mb).

Shukrani kwa Askofu Philipo Mafuja Magwano -AICT Dayosisi ya Pwani kwa ibada ya Heshima za mwisho tarehe 29 Machi, 2024. Shukrani kwa Shekh Mkuu na Mufti wa Tanzania Shekh Abubakar Zuberi kwa ushirikiano na dua katika msiba huu.

Shukrani kwa Mhe. Mwanaid Ally Khamis (Mb), Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalaghe pamoja na Wataalamu wote kwa ujumla, Vyuo na Taasisi zote chini ya wizara hii kwa upendo na ushirikiano wao.

Shukrani kwa Waheshimiwa Mawaziri wenzangu wote kwa upendo, umoja na ushirikiano.

Shukrani kwa Prof. Janabi, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wataalamu wote wa Hospitali ya Mloganzila kwa huduma na ushirikiano.

Shukrani kwa Dkt. Sebastian Kitengule Ganyaka (MD. MMed), Mkurugenzi wa Hospitali ya Kitengule iliyopo Tegeta, Dar es Salaam na mahsusi shukrani kwa Dkt. Jovina Lawrence Nkya (MD, MMed, Internal Medicine) kwa huduma na upendo mkubwa yeye na wataalamu wenzake kipindi cha kumuuguza Bi. Sophia Gwajima.

Siyo rahisi kuwataja wote ambao tungependa kuwashukuru bali kwa uchache; majirani zetu wote, ndugu, jamaa na marafiki, Mama Sophia Simba (Waziri Mstaafu), Uongozi wa Benki za Azania na Benki ya NMB, Uongozi wa UWT, Kamati ya Wanawake ya Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia na kwa Watoto, Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, Baraza la Ushauri la Wazee Taifa, SMAUJATA, FAGDI, SAWATA, MaleziNetwork, Chuo cha City College Mwanza Campus na rafiki zetu wote wakiwemo online duniani kote na kila mmoja.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa Neema ya tangu mwaka 2012 ya kuishi pamoja na Mzee Stiven Gwajima (Baba mzazi wa Advocate Gwajima aliyeitwa na Mungu mwaka 2019) na kumwacha mke wake Sophia Gwajima ambaye naye ameitwa na Mungu 27 Machi, 2024.

HAKIKA, maisha pamoja na wazazi hadi kuwazika ni Neema Adimu ya Mungu, tunamshukuru kwa Neema hii

Tumeuona mkono wa Mungu na Baraka za Mungu kupitia maisha yetu pamoja na wazee hawa. Tutaendeleza mema yote na kuzisemea heri za kuishi na wazee. Hakika, wazee ni tunu na uzee na kuzeeka hakukwepeki, ni Neema. Tukiwapenda na kuwathamini Wazee, nasi tutathaminiwa maana tumemuomba Mungu kila siku, atupe neema ya kuishi miaka mingi.

AHSANTENI WOTE, MBARIKIWE.

RIP Sophia Gwajima (Mayù) (Mama Mkwe), AHSANTE 🤲🙏🏽 kuniachia Mume mwema na Baba Mwema wa Familia). Tutakukumbuka Daima
2 Timotheo 4;7
View attachment 2951411View attachment 2951413View attachment 2951416View attachment 2951417View attachment 2951418View attachment 2951419View attachment 2951421View attachment 2951422View attachment 2951423View attachment 2951424View attachment 2951425View attachment 2951426View attachment 2951427View attachment 2951429View attachment 2951430View attachment 2951431View attachment 2951432

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Ahsante sana kwa Shukrani Mhe. Waziri. Tumezipokea , Mama yetu Sophia aendelee kupumzika kwa Amani na Mungu aendelee kuwatia nguvu ninyi kama familia katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mama.
 
Back
Top Bottom