Shemsa Mohammed (Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu): Tusiwadharau Mabalozi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,028
973

Shemsa Mohammed (Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu): Tusiwadharau Mabalozi

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed amewataka viongozi wa Chama hicho kutowadharau viongozi wa ngazi ya chini wakiwemo Mabalozi ambao wamekuwa mstari wa mbele kushawishi wapiga kura kuchagua viongozi wa CCM kuunda serikali.

Aliyasema hayo katika Tarafa ya Itilima, kata ya Mwamapalala, kwenye mwendelezo wa ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa inayondelea katika mkoa mzima wa Simiyu kwa ajili ya kukutana na viongozi wa mashina, matawi na kata.

Ziara hiyo ambayo inalenga kuimairisha, kukagua uhai wa chama pamoja na kutatua changamoto za wananchi huku akiwasisitiza kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili waweze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

‘’Tusiwadharau Mabalozi kwenye mashina kwa sababu ndio wenye watu, viongozi wenzangu tuwatambue mabalozi ili waendelee kutusaidia kuunda serikali…nimekuja kusikiliza kero na kukagua uhai wa CCM’’ alisema Shemsa.

Mwenyekiti huyo aliwataka viongozi wa kata na vijiji kufanya vikao vya kamati ya siasa na pia kukagua utekelezaji wa Ilani ili waweze kuwaeleza wananchi fedha ambazo zimeletwa na serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Alisema Mwenyekiti wa tawi ana nguvu sawa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa na anatakiwa kufanya kazi za utekelezaji wa ilani kama wanavyofanya viongozi wa wilaya na mkoa ili kukisimamia Chama cha Mapinduzi.

Aliongeza kuwa viongozi wa mkoa hawatakiwi kufanya shughuli za matawi au kata na badala yake shughuli hizo zinfanywe na viongozi wa matawi huku akiwasisitiza kuwasimamia na kuwatambua mabalozi.

‘’Mwenye tawi hutaki kumjua balozi, tunaelimishana namna ya kufanya kazi….mimi Mwenyekiti nakutana na viongozi wa kata na matawi, katibu na Mwenyekiti wa CCM wilaya fanyeni vikao ili mshuke kwa wananchi’’ amesema.

Aidha, Shemsa alisema watahakikisha kuwa watasimamisha wagombea wanaokubalika katika jamii ili CCM iweze kushinda na kuendelea kuwatumikia wananchi.

MWISHO.

_MG_0102wqas.jpg
_MG_9999.jpg
_MG_9992.jpg
_MG_0080.jpg
_MG_0047.jpg
_MG_0035.jpg
_MG_0029.jpg
 
View attachment 2976730View attachment 2976731View attachment 2976732View attachment 2976733View attachment 2976734View attachment 2976735View attachment 2976736
CCM kwa sasa imekuwa kama kusanyiko la Mahasimu, wala siyo Chama Cha siasa.
Watu wamekuwa wakihujumiana Sana na kufanyiana uovu wa kila aina na hata wakati mwingine wanawekeana sumu.
 
Back
Top Bottom