HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
69,530
94,996
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akiwa Dar es salaam leo amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais Dkt.Samia “Tunatarajia kuanzia mwisho wa mwezi huu wa pili zao la mchele litapungua bei”

Lengo la Serikali mchele ushuke bei.

======

Serikali yatangaza matazamio kushuka bei ya mchele

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa zao hilo kwa Taifa na pia Serikali imeondoa baadhi ya kodi ili zao hilo liweze kuongezeka kwenye soko.

Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo Dar es salaam leo ambapo amenukuliwa akisema “Tunatarajia kuanzia mwisho mwezi huu wa pili, wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu zao la mchele litapungua bei na Watanzania waweze kufikia zao hilo na kununua katika bei inayohimilika".
 
Ngoja sasa muanze kuletewa ma mchele yenye sumu, nakumbuka miaka ya 90s kampuni ya kina Mo Dewji ilileta mchele hatarishi kwa watu, serikali ya mzee Mwinyi ikajikoroga ikaupiga marufuku, lile sakata lake liliua watu wote walioshughulika na huo mchele kuanzia Long room hadi kwa wakemia wa nchi walioshughulikia.

Waliuawa vifo vya utata sana. Kwahio kuruhusu mchele toka nje ni fursa ya kuwaletea wananchi makanjanja na faida kwa wafanyabiashara na wala sio eti njia ya kupunguza makali ya bei ya mchele. Time will tell.
 
Tunapigwa na vitu vizito.
Mchele wetu, mahindi, maharage vimeenda wapi?

Njaa ni kali imefikia watoto wanaiba mandaz huko mbeya mkoa wenye chakula.

Nchi imekuwa ngumu
Yani tumeuza nje mchele wetu mtamu, sasa tunaagiza mchele kitumbo kama sio mchele wa mapembe unaopatikana Zanzibar. Lakini wakulima walinufaika, waliuza sana nafaka nje.

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Kunaanza kupambazuka ndio tunakumbuka shuka?!!!!!

Kwanini tusinunue kabisa mashuka ?!!! Na wale Magereza tuliowakataza kufanya shughuli kama hizi kwamba wasiingie kwenye biashara / uzalishaji kama hatuwezi kukidhi demand kwanini tusiwatumie?

Always three steps behind...
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akiwa Dar es salaam leo amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais Dkt.Samia “Tunatarajia kuanzia mwisho wa mwezi huu wa pili zao la mchele litapungua bei”
#MillardAyoUPDATES https://t.co/zSjVcUgWsD

Lengo la Serikali mchele ushuke bei
Wakulima wa Tanzania wataanza kulalamika, maana wanaogopa sana ushindani na bidhaa kutoka Nje!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Yani tumeuza nje mchele wetu mtamu, sasa tunaagiza mchele kitumbo kama sio mchele wa mapembe unaopatikana Zanzibar,
Lakini wakulima walinufaika, waliuza sana nafaka nje,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Mchele wako wewe na nani? Mchele ni mali ya aliyelima, ukitaka uwe mchele wako unaununua unaweka ndani
 
Waziri wa viwanda na biashara Ashantu Kijaji amesema serikali inatoa vibali kwa wafanyabishara wa hapa Tanzania ili waagize mchele tani elfu tisini ili kukabiliana na tatizo la mfumuko wa bei nchni.

Kwanza walifungua nchi kwa mbwembwe baada ya ziara ya rais Samia nchini kenya akawaruhusu wafanyabishara wakubwa wa nafaka wapeleke kenya kupitia mpaka wa wilaya ya rombo matani ya nafaka yakawa yanakwenda kenya , Somalia na Ethiopia hadi Eritrea usiku na mchana kutokea kwenye maghala makubwa ya wafanyabishara nchini na maeneo yanakolimwa mazao sasa wanawapa tena vibali vya kuagiza kutoa nje kuleta ndani

Katika kipindi ambacho bank ya dunia na shirika la fedha duniani wakishirikiana na shirika la chakula na kilimo walionya kuhusu njaa hasa baada ya kuibuka vita vya urusi na Ukraine vilivyozuia kupitia nafaka katika eneo la bahari nyeusi sisi hapa nchini Rais alisema mapema kuwa vyakula vitapanda bei bila kutoa nini kifanyike hivyo tukakosa mambo makuu matatu:

1.vyakula vyetu kupelekwa nje ya nchi ambako wao walikuwa na hali mbaya tangu corona kumbuka wao walifunga nchi na hali yao ya nusu jangwa

2.Rais hakusema nini serikali inachukua kwa haraka au muda mrefu kitu kilichofanya wafanyabishara kuuza kwa bei ya juu bila kuwa na utaratibu kama kwingineko duniani,mtu anaamka asubuhi anamua kupandisha bei tu ,maasfa biashara wamelala

3.Maeneo mengi hapa Tanzania mvua zimechelewa sana sambamba na mbolea kuchelewa,mvua zinaanza wakulima hawana mbolea walitakiwa kusubilia pia .

Tukiendelea kufanya majaribio ya maisha ya watanzania ipo siku tutajuta ,hakuna mjanja mbele ya njaa wafu hungana na kusahau siasa,dini wala kabila kupambana na adui yao mkuu njaa


USSR
 
Back
Top Bottom