Serikali ya Tanzania inapaswa kuilinda sana nch ya Burundi

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
696
1,874
MPANGO WA RWANDA KUITAWALA BURUNDI ILI KUINGIA KONGO KUPITIA ZIWA TANGANYIKA NA NAFASI YA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA MEDALI ZA UJASUSI NA INTELIJENSIA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA

BY LUGETE MUSSA LUGETE.

"Ndugu Mheshimiwa Rais tunapaswa kuilinda Burundi kwa hali na mali ili isiangukie mikononi mwa Rwanda kwa sababu tutakosa udhibiti wa ziwa Tanganyika kupitia Burundi na kuifanya Rwanda kutanua njia za kuingia Kongo kutoka Ziwa Kivu mpaka Ziwa Tanganyika"

Hiyo ilikuwa sehemu ya ripoti fupi ya
Brigedia Generali Francis Mndolwa kwa Raisi kupitia kwa mkuu wa majeshi wakati huo Generali George Waitara , ripoti hiyo ilimfanya Hayati Benjamin William Mkapa kumteua Brigedia Francis Mndolwa Kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi kuanzia mwaka 2003 mpaka mwaka 2010.

Kuna sababu zaidi ya 20 Mimi Lugete Mussa Lugete mchambuzi wa siasa za Kimataifa, Mwanahistoria na Mwanamajumui wa Afrika na Mtanzania wa kawaida nitatoa sababu sita kwanini serikali ya Tanzania inapaswa kuilinda Burundi ili isichukuliwe na Rwanda.

Mosi; Rwanda inataka kujitanua na kuongeza njia mbalimbali za kuingia Kongo hasa kupitia ziwa Tanganyika ambalo Tanzania ina umiliki wa asilimia 46% ,Kongo asilimia 41% na asilimia zilizobaki ni za Burundi na Zambia. Rwanda anataka kudhibiti mji wa Uvira Kongo ambao ni kando kando ya ziwa Tanganyika hata hivyo njia za utoroshaji wa madini kupitia ziwa Kivu zina changamoto kadha wa kadha kutokana na hali ya kusua sua kwa uhusiano kati ya Rwanda na Uganda yaani uhusiano huo umekuwa ukiyumba na kustawi yaani hauweleweki. Hivyo Rwanda anaitaka Burundi au kutafuta kiongozi wa Burundi atakayemtii ili apate njia ya kuingia Kongo bila kuingiliwa na Uganda. Rwanda anaitaka Burundi kupitia Cibitoki mpaka Bujumbura.

Pili; Raisi wa Rwanda Generali Paul Kagame na wasaidizi wake James Kabarebe,Fred Ibingira na Patrick Nyamvumba wanaamini Kwamba serikali ya Burundi imekuwa ikiitii sana Tanzania na kukejeli maagizo kutoka Kigali. Hivyo ni lazima Burundi itawaliwe na Rwanda ili kuendelea kulinda maslahi mapana ya Rwanda nchini Kongo kupitia Ziwa Tanganyika.

Tatu; Ulinzi na Usalama wa ziwa Tanganyika ni jukumu kubwa la Tanzania. Ikumbukwe Kwamba Waasi wa Red Tabara wakiongozwa na Alexis Sinduhije ambao wanaungwa mkono na serikali ya Rwanda ili kufanya mapinduzi nchini Burundi hutumia ziwa Tanganyika kufanya uhalifu kama utekaji wa mitumbwi na maboti ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na Burundi wanaopeleka Biashara zao Uvira,Kalemie na Bukavu Kongo ,tangu mwaka 1996 ujambazi umeongezeka eneo la ziwa Tanganyika kwa kifupi uharamia umekuwa mkubwa ukiachilia Kwamba Jeshi la Tanzania linafanya dolia ya ziwani kutoka Manda Kerenge Kigoma Kusini mpaka Rusolo Kagunga mpakani mwa Burundi na Tanzania ziwa Tanganyika. Hivyo kama serikali ya Tanzania ikimuachia Kagame aichukue Burundi tutapata hasara kubwa. Kagame anaweza kutekeleza mipango miovu kwa taifa letu pendwa Tanzania hasa ugaidi, uasi na uhalifu kwenye maeneo ya ukanda wa ziwa Tanganyika kuanzia Kongo mpaka mkoa wa Kigoma.

Nne; Nadharia ya ujenzi wa dola ya Bahima haikubaliki. Ndugu zangu Watanzania kwa miaka mingi Rwanda imekuwa ikijifananisha na Israel mfano mavazi ya jeshi la Israel na matendo mengi : Dola ya Bahima ni ndoto ya muda mrefu ya Watusti kutaka kusimika viongozi wenye itikadi zao katika nchi zote za maziwa makuu, nadharia hiyo ya kipuuzi inabebwa na Raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni na Raisi wa Rwanda Paul Kagame. Kufanya hivyo ni kutafuta uimara wao ambao ni wachache dhidi ya wabantu ambao ni wengi. Mpango wao ni kutaka Kuigawa Kongo Kuwa nchi mbili yaani kuzaliwa kwa taifa jipya la Mashariki ya Kongo ili liwe taifa la Watusti yaani Bahima. Tangu Generali Laurent Nkunda Batware akiwa jeshini Kongo kabla ya kuasi alikuwa akihubiri itikadi za Bahima ambazo zimejaa ukabila na ukanda. Burundi ni taifa la kimkakati kwa Rwanda na Tanzania hivyo kama taifa hatupaswi kuipoteza Burundi mikononi mwa madhalimu. Kama ambavyo Israel ni taifa dogo kijiografia lakini lilifanikiwa kunyakua maeneo ya waarabu baada ya vita ya mwaka 1967 maeneo kama Ukanda wa Gaza,Ukingo wa Magharibi,Sinai na Golan Heights yalibebwa na Israel na mpaka Sasa hivi Israel inaendelea kuchukua maeneo ya waarabu kwa kuungwa mkono na Marekani na washirika wake. Hivyo Rwanda Ina mpango wa kuichukua Burundi,Kongo, maeneo ya Tanzania hasa Wilaya ya Ngara na Biharamulo na maeneo mengine ya kimkakati.

Katika hotuba yake August 2023 Paul Kagame aliwaambia maafisa wa kijeshi Rwanda kwenye chuo cha mafunzo ya kijeshi Nyakinama alisema kwamba nanukuu

"Rwanda ni taifa dogo kijiografia kama ilivyo Israel lakini mataifa jirani wanaiogopa Israel na sisi tunapaswa Kuwa kama Israel"

Raisi Kagame aliendelea kutoa mifano wa hadithi na ngano za Kinyarwanda hasa ile ya mgomba mdogo ulioangusha mgomba mkubwa " hii ni itikadi wanayoihusudu waasi wa RPF wakati wanatoka Uganda kuingia Rwanda kuuangusha mgomba mkubwa yaani serikali ya Meja Generali Juvenile Habyalimana na utawala wa Kihutu chini ya mtandao wa Akazu.

Tano; Kama Burundi itaangukia mikononi mwa madhalimu wa Rwanda kutakuwa na vita kubwa Burundi na Tanzania tutaelemewa na wakimbizi hasa mkoa wa Kigoma, wakimbizi,uasi, ujambazi,uhaba wa chakula na kusambaa kwa silaha za magendo. Wote tunakumbuka Kwamba tangu mwaka 1961 baada ya kuuawa kwa waziri mkuu wa kwanza wa Burundi Prince Louis Rwagasore tulianza kupokea wakimbizi, mwaka 1966 Generali Michel Micombero akafanya mapinduzi nae akapinduluwa na Generali Jean Baptiste Bagaza kabla na yeye kuja kupinduliwa na Generali Pierre Buyoya. Hivyo serikali ya Tanzania inapaswa kuilinda Burundi ili isichukuliwe na Rwanda kuepuka Wakimbizi.

Burundi Kuna Watusti wachache ambao kwa mujibu wa serikali ya Rwanda wanaonewa na kubaguliwa na serikali ya Chama cha CNDD_FDD ndio maana serikali ya Rwanda imekuwa ikidhamini vikundi mbalimbali vya waasi nchini Burundi ambavyo vinaipinga CNDD_FDD.

Ni utamaduni na itikadi yetu Watanzania kupinga Magenge ya kihuni na serikali za kidhalimu. Kama tulivyompiga Nduli Idi Amin Dada na kutengeneza njia kwa Kagame na Museveni kupata madaraka sasa ni muda muafaka kuwasema viongozi hao hadharani ili dunia ijue mipango yao miovu. Serikali ya Tanzania haipaswi kuidharau Rwanda hata kwa bahati mbaya. Tunapaswa Kuwa macho kwa sababu adui huwa hatoki mbali. Kuidharau Rwanda kutokana na udogo wa jiografia yake ni kujidanganya na katika kanuni za ulinzi ni kosa kubwa. Mwaka 1904 serikali ya Urusi chini ya Mfalme Tsar Nicolaus II walipoteza vita dhidi ya Japan na Urusi ilipoteza udhibiti wa eneo la Manchuria huko China.

Sita; Kuilinda Burundi katika medali za ujasusi na intelijensia ni kumbana Rwanda ili asipate njia nyingi za kuingia Kongo. Tunapaswa kuwalinda Wakongo ambao wamekuwa wakimbizi wa nchi yao kutokana na rasilimali zao zinazoporwa na mabeberu kupitia vibaraka wao ikiwemo serikali ya Rwanda.

Hizo ndizo sababu za kwanini ni muhimu kwa serikali ya Tanzania kuilinda Burundi na kuisaidia dhidi ya hujuma za Rwanda.

Mpango wa Rwanda kuipora Burundi......

Mwaka 1985 uhusiano kati ya Marekani na serikali ya Generali Joseph Desire Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu Wa Zabanga uliyumba moja kwa moja wakati huo shirika la Ujasusi la Marekani kupitia ubalozi wao Kampala Uganda ulikuwa na majina mawili juu ya nani wa Kuwa Raisi ajae wa Rwanda baada ya CIA kutoridhishwa na serikali ya Rwanda ambayo ilikuwa ikiitii maagizo kutoka Paris Ufaransa. Ikumbukwe Kwamba Meja Generali Juvenile Habyalimana alikuwa kipenzi cha Paris. Meja Generali Juvenile Habyalimana alifanya mapinduzi ya Rwanda mwaka 1973 dhidi ya muasisi wa Rwanda Gregory Kayibanda na chama chake cha PARMEHUTU.

Kulikuwa majina mawili Paul Kagame na Emmanuel Fred Gisa Rwigema hata hivyo CIA walivutiwa na Paul Kagame kipindi hicho NRA wakiwa msituni kupambana ili kuichukua Uganda. Mwaka 1987 Uganda ikaangukia mikononi mwa NRA baada ya Generali Tito Lutwa Okelo kukimbia ikulu ya Kampala. Rwigema hakuwavutia Wamarekani Kwa sababu alikuwa na msimamo mkali hivyo Mwaka 1990 CIA walimpa ufadhiri Paul Kagame kwenda Marekani kusoma ujasusi na udunguaji ndio maana shirika la Ujasusi la Ufaransa DGSE linadai Kwamba huenda Paul Kagame alilipua ndege iliyowabeba Marais wa Rwanda na Burundi mwaka 1994 kwa sababu RPF hawakuridhika na makubaliano ya mkataba wa Arusha.

CIA walimpika Kagame ili kuja Kuwa Raisi wa Rwanda kwa maslahi mapana ya Marekani na washirika wake kuendelea kuihujumu Kongo. Kwa bahati mbaya Serikali ya Tanzania iliingia kwenye mtego wa Marekani wa kumuondoa Madarakani Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu Wa Zabanga na kuruhusu uongozi dhaifu wa Laurent Desire Kabila ambao ulichangia vifo zaidi ya Wakongo milioni sita kuanzia Operesheni Banyamulenge mpaka Operesheni Kitona ( First and Second Congolese Civil war).1996_2003.

Wakati Kagame anaandaliwa na CIA Kuwa Rais wa Rwanda nchini Burundi Pierre Buyoya alifanya njama za kumuua Rais mteule wa Burundi Melchior Ndadaye October 1993 kufuatia ushindi mnono alioupata Ndadaye dhidi ya Buyoya kwenye uchaguzi mkuu wa Burundi.Hali ilikuwa mbaya kiusalama nchini Burundi na baadae ukawekwa uongozi wa mpito kutoka kwa Francois Ngeze mpaka kwa Mwanamama Sylvie Kinigi na hatime Cyprien Ntaryamira akawa Raisi wa Burundi.

Katika makubaliano ya Arusha yaliyoanza mwaka 1993 ili kumaliza migogoro ya kisiasa Rwanda na Burundi na pia kati ya serikali ya Rwanda na waasi wa RPF Watusti ambao walikuwa Uganda, Kagame na Museveni hawakuridhishwa na makubaliano hayo kwa kile kinachoitwa makubaliano ya upande mmoja.

Baada ya hapo mauaji ya kimbari Rwanda yalifuata na Burundi kulikuwa na vita kati ya serikali ya Pierre Buyoya ambaye alinufaika na kutunguliwa kwa ndege iliyowabeba Marais wa Rwanda na Burundi hivyo kifo cha Rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira kilikuwa fursa kubwa kwa Pierre Buyoya na mwaka 1996 Buyoya alirudi Madarakani kwa mara ya pili na kuanza kuwapiga waasi wa CNDD-FDD akiwemo Hayati Pierre Nkurunzinza,Generali Leonard Nyangoma na Hussein Rajdabu ambao walikimbilia Mashariki mwa Kongo kuweka makazi na mafunzo ya kijeshi.

Paul Kagame na waasi wa RPF waliichukua Rwanda na kumaliza mauaji ya kimbari na walianza mpango wa Kongo. Kagame aliamua kumtanguliza mbele Rais wa Rwanda wa mchongo Pasteur Bizimungu ambaye alikuwa Rais wa mchongo wa Rwanda kuanzia mwaka 1994 mpaka mwaka 2000. Kagame alimtua Bizimungu kujiimarisha kupitia ujasusi wa kidola na kiuchumi na baadae mwaka 2000 akamuondoa madarakani kwa kumpa tuhuma mbalimbali ikiwemo rushwa na ubadhilifu wakati huo Kagame akiwa makamu wa Rais na waziri wa Ulinzi .

Kikwazo kikubwa kiliibuka mwaka 2003 baada ya serikali ya Tanzania kusuluhisha mgogoro wa Burundi ambapo Hayati Benjamin William Mkapa alimuomba Pierre Buyoya kujiuzulu na Kuundwa serikali ya mpito nchini Burundi ya mkataba wa miezi 18 kati ya Chama tawala cha Domitien Ndayizeye FRODEBU na miezi 18 mingine ya Pierre Nkurunzinza kupitia chama cha siasa cha CNDD-FDD ambapo zamani walikuwa waasi.

Baada ya Nkurunzinza kuchukua nchi akawa hana maelewano mazuri na Rwanda na kuanzia hapo serikali ya Paul Kagame ikaanza kumuandama ili Kumtoa Madarakani hata hivyo mpango huo haukufanikiwa licha ya Rwanda kufadhili makundi mbalimbali ya waasi nchini Burundi na majaribio kadhaa ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Pierre Nkurunzinza kuanzia mwaka 2003 mpaka mwaka 2020 Rwanda imejaribu kufanya mapinduzi nchini Burundi zaidi ya mara nane na yote yamekuwa yakinaswa na Shirika la Ujasusi la Tanzania T.I.S.S kwa kushirikiana na Jeshi la Tanzania. Jaribio maarufu ni la mwaka 2008 na 2015 ambapo Meja Generali Godefroid Niyombale alishindwa kumpindua Rais Pierre Nkurunzinza kutokana na mpango kabambe wa Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa ushirikiano wa T.I.S.S na JWTZ.

Tangu aingie madarakani Generali Evarist Ndayishimiye ambaye alipewa nchi na Pierre Nkurunzinza Rwanda imeongeza vurugu na mbio za kuiangusha Burundi kwa kuwaunga mkono waasi wa Red Tabara na jamii za Watusti wachache wanaoishi Burundi. Serikali ya Tanzania inapaswa kumlinda Rais wa Burundi dhidi ya hujuma na udhalimu wa Rwanda.

Nini kifanyike ili kudhibiti hali ya usalama ukanda wa maziwa makuu.Mimi Lugete Mussa Lugete mchambuzi wa siasa za Kimataifa na Mwanahistoria napendekeza yafuatayo.

Mosi; Jumuia ya Afrika Mashariki inapaswa kumuonya Rwanda na Uganda kuhusu mgogoro wa Kongo kwa kuwaambia ukweli pia serikali ya Tanzania ndio inaongoza kwa nguvu na ushawishi ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki.

Pili; Serikali ya Tanzania inapaswa kuwaua waasi wa Red Tabara kutoka Burundi wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda hasa wanapotumia ziwa Tanganyika kuingia Kongo.

Tatu; Serikali ya Tanzania na Kongo wanapaswa kuja na mipango kabambe katika ulinzi shirikishi wa Ziwa Tanganyika.

Nne; Serikali ya Kongo inapaswa kusitisha Operesheni Shujaa na Uganda kwani kwa zaidi ya miaka mitatu hakuna kilichofanyika kwa sababu Uganda ni mnufaika wa madini ya Kongo na Uganda haiwezi kuwaadhibu waasi wa M23 na vikundi vya kigaidi Kongo vinavyoungwa mkono na serikali ya Rwanda.

Tano; Serikali ya Kongo inapaswa kuboresha Jeshi lake na mfumo wa intelijensia ili kupambana na majasusi wa Rwanda nchini Kongo ambao wamekuwa wakilihujumu taifa la Kongo kwa kuuza habari Rwanda.

Sita; Umoja wa Afrika lazima utumie mbinu zote kwa kushirikiana na Jumuia za kikanda ili kumaliza migogoro ya kisiasa ndani ya Afrika. Mabeberu wamekuwa wanufaika wakubwa wa migogoro ya Afrika ili kuendelea kuinyonya Afrika.

Hitimisho;Mimi Lugete Mussa Lugete Mtanzania wa kawaida naamini Kwamba;Umoja na mshikamano wa Jumuia ya Afrika Mashariki ni kama Mwamba imara ambao hakuna dhoruba linaloweza kuubomoa; Umoja na mshikamano ni kama nyota angani zinazotuongoza kuelekea mustakabali wa Jumuia yetu ya Afrika Mashariki. Ni ngumu kujenga Jumuia ya Afrika Mashariki yenye kufuata misingi ya usawa,utu,na haki Ikiwa kuna wanachama wanafiki na Ndumilakuwili.Hivyo basi Ushujaa wangu Mimi Lugete Mussa Lugete ni matokeo ya kusema na kuandika ukweli,Kuwa na msimamo,kupigania haki ili kutengeneza hazina ya thawabu kwa Mwenyezimungu. Bora nife nikiwa askari wa haki kuliko Kuwa Sultan mwonevu .Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Jumuia ya Afrika Mashariki,Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki Burundi dhidi ya hujuma,hila na njama ovu za Rwanda.
 
Duuu!! We Mrundi ni nusu Kichaa kabisa. Jamani, hivi Mirembe bado inafanyakazi vizuri? kwa kweli huyu Nesi inabidi awahishwe maaneka naona hari imejirudia tene upyaaaa.
 
Mambo kule(DRC) yanaenda kwa kupiga dili.
Unapeleka majeshi kulinda amani kule,lakini wakifika kule wanapiga dili tu.
MONUSCO ndio hawa wanafukuzwa.
Jeshi la EAC lilipelekwa kule likafukuzwa.
Hili jeshi la SADC nalo pia litafukuzwa.
Kwa sababu hawa wakienda kule wanapiga dili tu. Hawafanyi kitu chochote kuimaliza vita.
Ndio nilikuwa nawasikia wanajadili leo.
There ain't nothing going on there.
Just stalemate,and stasis,and impasse.
Hakuna mawazo ya kuimaliza ile vita na kuyaondoa mateso ya wananchi.
Halafu Rishi Sunak kapata kutoka kwenye muswada aliokua anautafuta wa kupeleka wakimbizi Rwanda.
Inaelekea Jeshi la SADC lilipofika likasema Hawa Wazalendo waweke silaha zao chini,sisi tutapigana na M23.
Lakini wamekataa kuwa disarmed.
Kwa hiyo sasa Wazalendo wameruhusiwa kushiriki katika mapigano,lakini zinatumika subtle means kuwaletea restrictions.
 
Back
Top Bottom