Serikali ongezeni tozo zaidi, Wananchi wengi hawalipi kodi Tanzania. Wanaolipa kodi hawafiki Milioni nne

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,102
Usilalamike wakati wewe mwenyewe ukiambiwa haya taja vyanzo vipya vya mapato Tanzania hujui, Kama wewe kijana hapa JF na Wazee hamuwezi kutaja vyanzo vipya vya mapato ukiacha kodi za madini, Paye, Corporate Tax na VAT,

Namuunga mkono Mwigulu nchemba kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato vinavyotokana na mabadiliko ya teknolojia yaani Tozo

Tanzania ni Taifa la kushangaza sana, Watu wanaolipa kodi ni wafanyakazi wa sekta rasmi na wafanyabiashara waliosajiliwa tu, Wafanyakazi wanalipa kodi ya mshahara au kipato(PAYE) na ni rahisi kuwabana iwe sekta binafsi au Serikalini

Kuna wafanyabiashara kibao mitaani wanauza mboga mboga, Chips mayai hawajasajiriwa na wao wanatumia miundo mbinu ya barabara na zahanati lakini hawalipi kodi kabisa, Wao wanajua kusema chips yai elfu mbili, Katika elfu mbili kodi analipa wapi?

Wafanyabiashara wao ni kawaida kubanwa wanavyo leta malighafi ndani au wanaposafirisha, Hili kundi la wafanyabiashara bila kulipa wharfage pale Bandarini mzigo hautoki hata kidogo

Sasa watanzania waliobaki zaidi ya Milioni thelathini wanalipa kodi wapi? na tunawapata wapi?

Ukuaji wa teknolojia hasa Facebook, WhatsApp, na Internet kwa ujumla umefanya rahisi kutambua baadhi ya mapato ambayo awali hayakujulikana

Hawa watu Milioni thelathini wana simu na wanatumia pesa wakati wote, Yaani mtu unapokea pesa bure kama mshahara wa kawaida Halafu kodi hutaki kulipa

Ni muhimu serikali iweke kila atakaye tumia Tik tok, WhatsApp, Twitter, Instagram akiwa Tanzania akatwe asilimia 40% ya bundle lake na hili linawezekana kabisa

Ni muhimu serikali ikaongeze nguvu kazi kukusanya kwa hawa watu ambao wagumu kujisajiri rasmi kama vibanda vya mboga mboga na chips mitaani

Hakuna Maendeleo tutayapata kwa kutegemea kodi ya watu Milioni nne kwenye Taifa la watu zaidi ya Milioni thelathini na tano

Kama hujui vyanzo vipya vya mapato kaa kimya, Usilaume wakati wewe mwenyewe hujielewi na huna hoja za kuonyesha vyanzo vipya vya mapato

Lipa tozo kwa mustakabali wa Taifa lako na Vizazi vijavyo
 
Maendeleo yapi wamefanya kwa tozo za miamala.
Bila Tozo hiyo ahueni ya mafuta zaidi ya bilioni mia mbili kwa miezi miwili unafikiria zinatoka wapi?

Wewe unauza chips mayai hutaki kulipa kodi lakini kila wakati unailaumu serikali miradi haikamiliki
Lipa tozo kiongozi acha janja janja
 
Kodi tunalipa sehemu zote tukinunua vitu vyote tunakatwa vat
Wenzako wanaodai refund ya hiyo VAT au hujui

Sasa VAT inaweza lipa mishahara ya watumishi wa serikali zaidi ya bilioni mia tano kwa mwezi

Vat haitoshi, Taja vyanzo vipya vya mapato, VAT ipo kila siku
 
Kwa Rasilimali za nchi hii kodi ilipaswa kulipwa na.Wawekezaji pekee

Tanzania tuna kila kitu kasoro Vyama vya Upinzani tu
Rasilimali ipi unaongelea mkuu

Madini yanachimbwa na serikali inakusanya kodi na JPM alibadili sheria tunakusanya zaidi

Utalii, Mama amefanya Royal Tour na tunakusanya zaidi

Bahari na ziwani tunakusanya zaidi

Taja vyanzo vipya vya mapato mkuu

Wakati fulani nikiwa bungeni watu walilaumu tunategemea kodi ya bia tu, Kila mwaka kodi ya bia iliongezeka

Sasa taja vyanzo vipya kumsaidia Mwigulu na nchi yako, Bila kuwa na suluhisho la mambo bora ukae kimya

Achana na hearsay mkuu, Ongea kama upo field uhalisia
 
Mikakati mibovu na wanaobanwa kulipa kodi ni wafanyabiashara wa madaraja ya chin
Mikakati gani mkuu

JPM alibana baadhi ya watu tu mfano wafanyabiashara wasiofika Milioni tatu na hao ni wale wakubwa

Wewe na kibanda cha chipsi unalipa kodi wapi?

Kondakta wa Daladala analipa kodi wapi au anasepa na posho

Lazima wote tuwajibike ndio lengo la mada hii

Wanaolipa kodi ni wachache sana Tanzania hii
 
Bila Tozo hiyo ahueni ya mafuta zaidi ya bilioni mia mbili kwa miezi miwili unafikiria zinatoka wapi?

Wewe unauza chips mayai hutaki kulipa kodi lakini kila wakati unailaumu serikali miradi haikamiliki
Lipa tozo kiongozi acha janja janja
We juha kweli, hizo B100 mafuta yanapanda bei kila mwezi.
 
Rasilimali ipi unaongelea mkuu

Madini yanachimbwa na serikali inakusanya kodi na JPM alibadili sheria tunakusanya zaidi

Utalii, Mama amefanya Royal Tour na tunakusanya zaidi

Bahari na ziwani tunakusanya zaidi

Taja vyanzo vipya vya mapato mkuu

Wakati fulani nikiwa bungeni watu walilaumu tunategemea kodi ya bia tu, Kila mwaka kodi ya bia iliongezeka

Sasa taja vyanzo vipya kumsaidia Mwigulu na nchi yako, Bila kuwa na suluhisho la mambo bora ukae kimya

Achana na hearsay mkuu, Ongea kama upo field uhalisia
Kodisha bandari na mlima Kilimanjaro kwa WATU makini nakuhakikishia hakuna Mtumishi atalipa Paye wala Kitambulisho Cha Mjasiriamali
 
Umenena vema wananchi wengi hawalipi na wala hawana sifa ya kulipa kodi ila hao ndio wanaongoza kwa kulaumu na kutumia kodi kubwa za walipa kodi wachache.
Uzazi usio na mpango
Matumizi ya miundombinu
Huduma za afya wasio na sifa za kulipa kodi ndio wazaaji na watumiaji wazuri sana wa hospitar za serikal na wanataka wapate dawa na tiba buree
 
Kwa Rasilimali za nchi hii kodi ilipaswa kulipwa na.Wawekezaji pekee

Tanzania tuna kila kitu kasoro Vyama vya Upinzani tu

Nonsense. Kila nchi ina rasilimali na bado wanalipa kodi.

Unajua TZ haipo hata top 5 ya gold producers Africa, duniani haipo hata top 20.

Mbuga kila nchi zipo. Hatuna mafuta, natural gas inapatikana kila kona na yetu haina manufaa yeyote.

Mmemezeshwa ujinga mnaamini TZ tu ndo nchi yenye rasilimali wakati zipo kila kona na bado watu wanalipa kodi.

US ina mafuta, gold, natural gas, mbuga, milima, copper, bahari nk na bado kodi zinakatwa hadi mtu ukijamba tu. Same applies in Russia, China na Europe. Nenda South Africa tu hapo uone kama mnawazidi kwa rasilimali yeyote na uone wanavyokamuliwa kodi.

Bila kutanua wigo wa kodi mtaendelea kusubiri sana. Mleta uzi yupo sawa.
 
Wigo ndio hizo Tozo sasa mnalialia nini?
 
Back
Top Bottom