A
Anonymous
Guest
Kituo cha Afya kilichojengwa Kata ya Mkumbi, Halmashauri ya Mbinga Vijijini Mkoa wa Ruvuma kimechukua muda mrefu kukamilika, tatizo ni siasa na mizunguko kibao.
Kwanza tangu mradi uanze aliyekuwa Mtendaji wa Kata aliingia kwenye mgogoro na Diwani, Mtendaji akahamishwa.
Akaja Mtendaji mwingine na yeye hakumaliza hata nusu Mwaka, baada ya muda akaomba kuondoka, hivi sasa yupo Mtendaji mpya ila bahati yake ni kuwa amekuta maeneo mengi yamejengwa, pia Diwani hakuwa vizuri kiafya.
Hadi sasa wanatoa ahadi kila wakati ila hakifunguliwi.
Tunaiomba Serikali itusaidie kituo hicho cha Afya kifunguliwe kwa kuwa ili kupata matibabu inabidi twende hadi Mbinga Mjini ambapo kuna umbali na barabara sio rafiki na Zahanati iliyopo bado haikidhi mahitaji.