Serikali ikipeleka Trekta kila kijiji itapendeza

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,331
12,647
Kwa kuanzia Serikali na Benki ya Kilimo iwapatie wanavijiji matrekta ya bure au ya mkopo ili kubadilisha kilimo chao cha jembe la mkono. Sasa hivi wanavijiji wamehamasika kulima kwa matrekta lakini hayapo vijijini na hata kama yakipatikana ni ya kugombania na kwa bei ya juu kati ya sh. 40,000 na 60,000 kwa eka.

Angalaau basi kila kijiji kipatiwe trekta moja kubwa litakalosaidiana na yale ya watu binafsi kwenye kilimo. Kupewa trekta ni bora kuliko kuliko kupewa pesa.
 
Wazo zuri, hata kuanzia vijiji kumi Trecta moja. Malipo baada ya mauzo. Itaongeza sana ufanisi, mapato na kurahisisha kazi ya kilimo kwa wakulima wengi.

Wanaweza kuingia ubia na kampuni binafsi kusupply hizo tractors na kuzifanyia ukarabati.
 
Kitu cha kumilikiwa na watu wengi huwa ni shida sana kukisimamia. Trekta moja kijiji kizima sijui watajipangaje kumlimia kila mtu. Mafuta ataweka, service yake na matengenezo pia atagharamia nani?

Suluhisho ni kuwawezesha wanakijiji kupata soko la uhakika Kama la korosho ili waweze kukopesheka na kupata uwezo wa kununua kila mtu lake.
 
Ni hivi, linakuwa linamilikiwa na kampuni binafsi, yenyewe ndio itakuwa inafanya ukarabati, na kutunza kumbukumbu kuhusu matumizi, mafuta kama vile unavyokodisha gari na kutumia kwa masaa kadhaa kutoka avis.

Tofauti malipo yanaweza kuwa hapo hapo au baada ya kuuza mazao.

Tukisubiri, tutasubiri muda mrefu sana hata kama kuna soko la uhakika wachache wanauwezo wa kununua individually.
 
Akili kama hii uliyonayo wewe inahitaji dhamira na kukubali kushauliwa
 
Akili za kijamaa utazijua tu. Unataka upewe badala ya kununua.

Hopeless
 
Toa maoni yako, tuwasaidiaje wakulima maskini?

Acha kukariri, ujamaa, ubeberu, ujima, labels.

Ili tufike tunapotaka kwenda tunahitaji / tutahitaji combination of different systems, policies and ideas modified accordingly to suit our specific needs.

Tunahitaji common sense, ubunifu na kuwa pragmatic, kufanya kile kinachotakiwa kuwasaidia na kuwainua watu wetu bila kujali silly labels.

Tunaongelea kuwapa hand-up siyo hand-out, kwa kipindi kifupi miaka miwili, mitatu mpaka wawe na uwezo wa kusimama imara wenyewe kwa miguu yao miwili.

Hizi unajua kiasi cha ruzuku, misaada inayokwenda kwa wakulima wa Ulaya?

Swali muhimu ni:- Does it works for our people, in this context, at this moment in time?

Targeted, flexibility, fluidity, creativity, what works, common sense should be key words. If facts change, policies, systems should also change to accomodate and reflect new facts.
 
Akili kama hii uliyonayo wewe inahitaji dhamira na kukubali kushauliwa

Kufanikiwa kwenye issue ni lazima serikali ishirikiane na sekta binafsi, wataalamu (e.g SUA), kampuni kubwa na kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji.

Mfano unaweza kuongea na Kampuni kama Massey Ferguson, Kubota, John Deere, waje kufungua kiwanda hapa, na serikali itatununua trecta / kukodisha 1000 kwenye miaka mitano ijayo. (maongezi kuhusu terms /conditions of the deal)

Upande wa serikali unaweza kuwapa ardhi ya bure kwa miaka kadhaa (E.g Special Economic Zone). Tax holiday kama miaka mitano hivi hadi warudishe gharama za investment yao, unafuu kwenye corporation tax na kodi zingine. Hao hao wenyewe wanaweza kufanya repair, na kusambaza matreka vijijini wakishirikiana na serikali.

Hichi kiwanda kinaweza pia kupata wateja kutoka nchi zingine za East, Central and Southern Africa. Kutakuwa na faida nyingine kama ajira kwa watanzania na kujifunza utaalamu, serikali kupata kipato,

Hawa wakulima wakisimama watalipa kodi kubwa kwa sababu kipato chao kimeongezeka, mazao yatakayouzwa nje yataleta foreign currencies, umaskini utapungua sana.

Inawezekana kama Rwanda wameweza kufanya dili na Volkswagen kwanini tusiweze kufanya dili na kampuni kama John Deere, kubota au Massey Ferguson?
 
Kwa kuanzia Serikali na Benki ya Kilimo iwapatie wanavijiji matrekta ya bure au ya mkopo ili kubadilisha kilimo chao cha jembe la mkono. Sasa hivi wanavijiji wamehamasika kulima kwa matrekta lakini hayapo vijijini na hata kama yakipatikana ni ya kugombania na kwa bei ya juu kati ya sh. 40,000 na 60,000 kwa eka.

Angalaau basi kila kijiji kipatiwe trekta moja kubwa litakalosaidiana na yale ya watu binafsi kwenye kilimo. Kupewa trekta ni bora kuliko kuliko kupewa pesa.

Watayauza yote kuiba spea kuuza srap na hakuna kitakachofanyika
 
W
Kufanikiwa kwenye issue ni lazima serikali ishirikiane na sekta binafsi, wataalamu (e.g SUA), kampuni kubwa na kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji.

Mfano unaweza kuongea na Kampuni kama Massey Ferguson, Kubota, John Deere, waje kufungua kiwanda hapa, na serikali itatununua trecta / kukodisha 1000 kwenye miaka mitano ijayo. (maongezi kuhusu terms /conditions of the deal)

Upande wa serikali unaweza kuwapa ardhi ya bure kwa miaka kadhaa (E.g Special Economic Zone). Tax holiday kama miaka mitano hivi hadi warudishe gharama za investment yao, unafuu kwenye corporation tax na kodi zingine. Hao hao wenyewe wanaweza kufanya repair, na kusambaza matreka vijijini wakishirikiana na serikali.

Hichi kiwanda kinaweza pia kupata wateja kutoka nchi zingine za East, Central and Southern Africa. Kutakuwa na faida nyingine kama ajira kwa watanzania na kujifunza utaalamu, serikali kupata kipato,

Hawa wakulima wakisimama watalipa kodi kubwa kwa sababu kipato chao kimeongezeka, mazao yatakayouzwa nje yataleta foreign currencies, umaskini utapungua sana.

Inawezekana kama Rwanda wameweza kufanya dili na Volkswagen kwanini tusiweze kufanya dili na kampuni kama John Deere, kubota au Massey Ferguson?
Well said Mkuu, Tanzania tunaiatamia ardhi bila kufaidika nayo. Ardhi ina thamani kubwa kuliko madini, mbuga na viwanda. Pesa iliyotumika kuzuusha ukuta mererani sijui ingetosha kununua matrekta mangapi na kuyagawa kwenye vijiji. Chuo cha kilimo cha sokoine kimejaa wababaishaji ambao hawajalisogeza taifa mbele japo hata kwa sm 1. Tanzania ingeweza kuwa ghala la chakula katika ukanda Wa east and central Africa.
 
Hapo Mererani sidhani kama walitumia pesa nyingi sana sababu ni JKT ndio waliojenga huo ukuta. Btw hao hao JKT pia wanaweza kufundishwa mbinu sahihi za kilimo cha kisasa na wataalamu wa SUA (kuchagua mbegu, bora, Irrigation, how operate and repair tractors, mbolea sahihi, jinsi ya kupata masoko ya ndani na nje) wakitoka hapo wanaenda kuwafundisha wakulima nchi nzima.

Anyway it is not too late. Muhimu kuchagua vipaumbele sahihi vinavyoweza kulikomboa taifa na kuwasaidia watu wengi kwenye muda mchache.

Uwezo tunao wa kufanya mapinduzi kwenye secta ya kilimo tukijipanga vizuri na kuweka mikakati madhubuti, kiasi kwamba ndani ya miaka kumi tukawa ghala la chakula katika ukanda wa East, Central and Southern Africa na labda dunia nzima.

Mahitaji ya mazao ya kilimo yanaongezeka na yataongezeka sana tu duniani kutokana na kukuwa kwa idadi ya watu kila mwaka na kuongezeka kwa kipato kwa watu wengi duniani. Opportunities are immense.

Kwanza ni kufanya maamuzi, pili kupanga mikakati ya kufikia hayo malengo, tatu mipango madhubuti ya kutekeleza haya malengo.

Serikali inaweza kuwaalika wananchi, wataalamu na wadau wote wenye maoni jinsi ya kufikia na kutekeleza hayo malengo watoe maoni yao. Pia inaweza kujifunza kwa nchi nyingine kama Brazil, Argentina, India, Thailand, Japan, China, Russia, South Africa, Spain, Italy etc.

Serikali inaweza kutumia mitandao, kutengeneza website, kwa barua, emails, au uso kwa uso. Muhimu kuwasikiliza wadau wote na kuchukua yale mapendekezo mazuri zaidi. Inawezekana ni kujipanga tu.

Nimeangalia takwimu za UN kuhusu uzalishaji wa chakula Duniani Tanzania ni ya tano kwenye maharage, ya tatu kwenye viazi vitamu, ya pili kwenye katani hapo hata hatujaanza kujaribu. Je tukiamua kufanya kwa dhati, kiukweli tutafika wapi?
List of largest producing countries of agricultural commodities - Wikipedia
 
Back
Top Bottom