Serikali iache kuingiza siasa kwenye mengine

baba aura

JF-Expert Member
Aug 5, 2023
233
356
Imekuwa kawaida sasa kwa serikali kuingiza siasa katika jambo linakalibia kufanikiwa au kufikiwa, tena viongozi wa kisiasa ndo wamekuwa mbele kudandia jambo.

Mfano, tumeona sekta ya michezo vilabu vyetu pendwa vimevuja jasho mpaka wanafikia hatua fulani ambayo inaweza kuipa mafanikio klabu husika basi anatokea mwanasiasa anaanza kuingiza siasa kwenye michezo na matokeo huja mabaya.

Haya sasa twende kwenye suala lililonifanya nije niweke Uzi hapa,

Kwa sasa serikali imeingiza mambo ya siasa kwenye sekta ya kilimo hasa cha mpunga na matokeo yameonekana sasa kwa gunia la mpunga kuuzwa elfu 70 na ikifika mwezi wa tano watu wengi watakuwa wanavuna hivyo bei itashuka mpaka elfu 50 hii ni hasara tupu.

Chukuliaa mfano
*Kukodi shamba kwa heka 500000 kwa 400000
*Kukatua 60000
*Kuvuruga kwa heka 60000
*Kupanda kwa heka, hapa inategemeana kama utakuwa unapima ishirini kwa ishirini na kila ishirini moja inaweza kuwa 7000 mpaka elfu 10000 na kwa heka moja kuna ishirini zipatazo 14 hivi
*Kung'olea kwa heka kupima ishirini ni 5000
*Kulinda ndege kwa heka ni 60000
*Kufyeka kwa heka, kupima ishirini 5000
*Kusomba kwa heka kupima ishirini 2000
*Kupiga mpunga kwa heka elfu 60000
*Usafirishaji kila roba 3000 Hii inategemea na umbali
*Ushuru wa mazao kila roba 1000

Halafu Serikali inasema mpunga uuzwe roba elfu 50 inahuzunisha sana na inawaumiza sana wakulima wa mpunga na hata kama ndo harakati za uchaguzi mjue mnafeli kabisa.

Ni hayo tu.
 
Kwamba kukodi shamba la kulimia mounga, gharama ndio ipo juu kiasi hicho?

Ni wapi huko?
Labda yale majaruba ya kisasa kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Mikoani kwenye majaruba ya kienyeji heka ni kuanzia elfu 50 - mpaka laki 2 kutegemea na wilaya
 
Back
Top Bottom