Serikali boreshini utalii wa Makumbusho ya Kihistoria na Utamaduni, wageni hawataki kuona wanyamapori tu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,936
46,687
Moja ya mambo ambayo huwa tunajifariji na kujidanganya nayo wakati wote katika sekta ya utalii ni suala la kuwa na vivutio vingi vya utalii tukimaanisha hasa mbuga na hifadhi za wanyamapori au maliasili iwa ujumla.

Ni jambo zuri kuwa na vitu hivi ila ni vyema tukajia hivi sio vitu vya kipekee "unique" kwetu tu. Mataifa mengi sana ya Simba, Tembo, Twitter, Nyati, Chui, Mamba n.k hifadhini au kwenye zoo.

Historia ndio kitu kinachoyatofausha mataifa na watu, watalii wengi wanavutiwa zaidi na Piramidi za Misri na Mafarao wao kuliko Simba wa Tanzania au mahali kwingine. Eiffel Tower ya Paris peke yake kwa mwaka inatembelewa na watalii zaidi ya Milioni 7 kiasi ambacho ni sawa na mara 4 ya watalii wa Tanzania kwa mwaka. Ukuta mkuu wa China "great wall of China" unatembelewa na watalii milioni 10 kwa mwaka.

Mifano ni mingi sana ila ni vyema kufahamu watu wenye pesa za kutalii wanavutiwa zaidi na historia zinazoonyesha ni kwa namna gani binadamu aliweza kubadilisha mazingira yake au maingiliano yake na jamii nyingine kipekee kuliko maliasili ambazo ziko kiasili tu.

Kinachotakiwa na kwetu sisi ni kui brand historia na makumbusho yetu ya kina Mkwawa, Mangungo, Mangi Meli, Kilwa kivinje, Tipu Tipu, vita vya Iddi Amin, wapigania uhuru wa Africa Kusini, uhuru wetu, n.k Binadamu wenye pesa za kutembea wanapenda sana kujua historia za sehemu tofauti sio kuangalia Simba tu ambao wanaweza kumuona kwenye zoo Marekani au Ulaya.
 
Naunga mkono hoja ,bila kusahau kujengwa fukwe za maana kuanzia Pwani ya Mtwara Hadi Tanga na Zile za kwenye Maziwa hasa Tanganyika na Nyasa Kuna fukwe nzuri na mandhari ya kuvutia sana.

View: https://twitter.com/mhdhamad/status/1783926319400534510?t=PtFgw4R_y_KBFUog-MvCMw&s=19
 
Back
Top Bottom